MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

MAMBO YAKO HUKU!

Posted by Bob Sankofa on April 7, 2008

Ushasikia FotoBaraza? Hebu Bonyeza kwenye hiyo picha hapo juu uone kitatokea kitu gani?

Posted in Uncategorized | Leave a Comment »

FATMA NA MAMBO YA FESTIVE COLLECTIONS

Posted by Bob Sankofa on March 7, 2008

sauti-day-3-146.jpg
Fatma Amour wa lebo ya mitindo ya Famour kesho usiku katika hoteli ya Move n Pick atafanya onesho la mitindo ya kazi zake alilolibatiza jina la Festive Collections. Wewe umepanga kwenda wapi kesho? Basi katika mitoko yako anza na huu. Njoo na shilingi elfu ishirini za kiingilio, uje kuona mambo mazito ya dada Fatma.
modelsbc.jpg
Hawa ni wanamitindo watakovaa nguo za Famour kesho pale hotel ya Move n Pick. Usikose kumuunga dada Fatma mkono.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

SASA BAADA YA HAPA NINI KINAFUATA?

Posted by Bob Sankofa on March 7, 2008

picture-049_wafadhili.jpg

Abdi Simba, mmoja wa wamiliki wa taasis ya Flame Tree, waandaaji wakubwa wa maonesho haya akiongea jambo na mama wa Benki ya Kenya (mama aliyetoa pesa za ufadhili). Hapa nadhani mama alikuwa anamuuliza jamaa kuwa ana mpango gani baada ya onesho hili.

 Katikati ni mkurugenzi wa kampuni ya utayarishaji filamu ya Savannah na aliyewahi kuwa mkurungenzi mkuu wa Zanzibar International Film Festiva, Imruh Bakari.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

NYONGEZA YA MAONESHO

Posted by Bob Sankofa on March 7, 2008

picture-025_mauzo.jpg
Kama huna uwezo wa kununua sanaa (Vinyago) kubwa-kubwa za kina dada hawa basi unaweza ukanunua poster za moanesho haya kwa shilingi elfu tano au kwa kina mama unaweza kununua vifaa vya urembo vinavyotokana na miti kama bangili, hereni na mikufu. Ni namna fulani ya kujiwekea kumbukumbu kuwa ulihudhuria maonesho haya. Pili ndio alikuwa mezani jana.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

UMECHEKI HIZI?

Posted by Bob Sankofa on March 7, 2008

picture-027_wageni.jpg
Baadhi ya wageni wachache wakiangalia baadhi ya kazi za kina dada wasanii wachongaji. Kazi zinafurahisha kwa kweli.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

KARIBU MGENI

Posted by Bob Sankofa on March 7, 2008

picture-010_karibu-mgeni.jpg

Mwandale Mwanyekwa, msanii na  muandaaji mshiriki wa maonesho haya akiwakaribisha wageni waliofanikisha uwepo wa maonesho haya kwa kutoa fedha. Mwenye nguo ya bluu ni mama kutoka Benki ya Kenya na huyo mzungu ni mfadhili toka Ubalozi wa Uswizi. Wafadhili hawa wameahidi mbele ya hadhira kwamba msaada wao hautaishia kwenye maonesho haya, watasaidia kina dada hawa kuanzisha chama cha Wasanii Wanawake Tanzania.

Dada mwenye mtoto pale nyuma ni Pili, msanii mshiriki, na yule mwenye kilemba cha buluu bahari ni Pudenciana, msanii mshiriki vilevile.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Kazi, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania | 2 Comments »

MAONESHO YAKO WAZI

Posted by Bob Sankofa on March 7, 2008

picture-003_yamefunguliwa.jpg

Hatimaye yale maonesho ya Wasanii Wachongaji Wanawake wa Tanzania yamefunguliwa rasmi jana usiku. Hawa ni baadhi ya wageni waliofanikiwa kuwaunga mkono dada zetu. Maonesho yako wazi hadi tarehe 26 mwezi huu. Ukitoka kazini pita pale Makumbusho ya Taifa siku moja uone kinachoendelea.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

KILABU CHA USHAIRI CHAPATA UGENI

Posted by Bob Sankofa on March 5, 2008

img_0241_3_1.jpg
Jumanne ya mwisho ya mwezi wa uliopita kile kilabu chetu cha ushairi japa Bongo kilitembelewa na mwandishi mkubwa wa vitabu vya riwaya toka kule Afrika ya Kusini. Mwandishi huyu anakwenda kwa jina la Ms. Koenings. Wanachama walifurahia nafasi hiyo kwani waliweza kumuuliza mwandishi huyu maswali kadha wa kadha.
 img_0239_1_1.jpg
Koenings akisoma sehemu ya kitabu chake alichotoa hivi karibuni. Kitabu kinakwenda kwa jina la “The Blue Taxi”.
Picha kwa hisani ya kamera ya simu ya kiganjani ya Sandra Mushi.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

“MGUU SAWA ” KWA MAONESHO

Posted by Bob Sankofa on March 5, 2008

img_9177_mwandale2.jpg

Mwandale Mwanyekwa, msanii mwanamke wa fani ya uchongaji, akimalizia moja ya sanaa zake nyingi zitakazojiri pale katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kuanzia siku ya Tarehe 7 asubuhi. Maonesho yanafunguliwa kesho usiku lakini watakaojiri kesho ni wale waliopewa kadi za mwaliko tu halafu kwa muda wa wiki tatu zijazo yatakuwa wazi kwa Watanzania wote. Kiingilio BURE.

img_9648_mwandale1.jpg

Sanaa inapakwa mafuta, nafikiri hii ni namna fulani ya kuongeza thamani ya sanaa hii maana baada ya kupakwa mafuta kazi hii huwa inang’ara kwelikweli.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fotografia, Kazi, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

WASANII WACHONGAJI WANAWAKE TANZANIA

Posted by Bob Sankofa on March 4, 2008

womensculpturepostersmall2.jpg
Tarehe 7 ya mwezi huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kutakuwa na maonesho ya sanaa ya uchongaji wa vinyago. Maonesho yatadumu kwa muda wa wiki tatu, hiyo ni hadi tarehe 26 ya mwezi huu wa tatu. Karibu uwape sapoti kina dada. Wasanii wenyewe ni Mwandale Mwanyekwa, Pili Mtonga, Hawa Jarufu na Pudenciana Mwamalumbili. Kwa taarifa zaidi soma posters zilizosambazwa jiji zima, hadi kule visiswa vya karafuu nako wanazo habari pia. Kila la heri!

Posted in Africa, Art, Bongo, Fotografia, Kazi, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

KAZI NA DAWA

Posted by Bob Sankofa on February 10, 2008

sauti-day-3-001_wadau.jpg

Ni dhambi kufanya kazi muda wote na kusahau kula. Hapa niko na wadau wangu walioko hapa tamashani. Tuko kwenye mgahawa wa mwanamuziki maarufu, marehemu Freddy Mercury. Unamkumbuka? Aliimba ule wimbo maarufu wa “Zanzibar, ooh Zanzibar, Beautiful Island, ooh Zanzibar”, umekumbuka sasa eeh, :-), poa sana. Freddy alikuwa ni mmoja wa watu waliokufa kwa Ukimwi miaka ile ya mwanzoni kabisa ugonjwa huu ulipoingia. Hakuona haya, alijitokeza hadharani na kuusema ukweli kuhusu hali ya afya yake.

Napenda kuwashukuru wote mnaotuma maoni lakini kwa sasa niko na mchakamchaka kidogo siwezi kujibu maoni ya mtu mmojammoja. Nikipata wasaha nitajibu. Baadae kidogo.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | 5 Comments »

BRING THE NOISE

Posted by Bob Sankofa on February 10, 2008

sauti-day-3-149_bring-the-noise.jpg

British Council waliwahi kuandaa shindano la kutafuta wanamuziki watakaounda bendi iitwayo Bring the Noise, katikati ya mwaka jana. BC walifanikiwa lengo lao na kutoka Tanzania mwanamuziki aliyeshinda shindano hilo alikuwa ni Paul Ndunguru (kushoto kabisa, mwenye gitaa). Nchi zingine zinazounda bendi hii ni Uganda, Kenya, Uingereza, Nigeria na nyingine nimesahau 🙂

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

WAPI IMEWASILI ZANZIBAR

Posted by Bob Sankofa on February 10, 2008

sauti-day-3-105_zavara.jpg

Hatimaye ule mradi wa British Council, Words and Pictures (WAPI), umeletwa hapa visiwa vya karafuu jana. Zavara ambaye ni mmoja wa waendeshaji wakuu wa mradi ule alikaribishwa jukwaani kuuelezea vyema mradi ule. Kulia kwake ni dada Karola Kinasha na kushoto kwake ni dada Rose.

Posted in Uncategorized | Leave a Comment »

MALOUMA MINT OULD MEIDAH

Posted by Bob Sankofa on February 10, 2008

sauti-day-3-065_malouma2.jpg

Anatokea kule Mauritania. Nilipomwangalia jana akifanya muziki wake nikagundua kuwa huitaji kuwa robo tatu uchi jukwaani ili upendwe na washabiki wako. Nikagundua pia kuwa wanamuziki wengi wa kike ukiacha Malouma wanatuuzia miili yao na si muziki wao. Mama huyu anaimba kiwa amevaa baibui muda wote na haombi makofi kwa washabiki, yeye ni dozi juu ya dozi tu.

sauti-day-3-065_malouma1.jpg

Malouma ni binti wa mwanamuziki mwingine maarufu kule Mauritania, Moktar Ould Meidah na pia ni mjukuu wa mghani mashairi, Mohamed Yahya Ould Boubane.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MAURICE KIRYA

Posted by Bob Sankofa on February 10, 2008

sauti-day-3-027_kirye1.jpg

Alikuwepo pia mtoto wa nyumbani, Moses Kirya. Namwita mtoto wa nyumbani kwa sababu anatoka Afrika Mashariki. Alifanya nyimbo kama tano hivi lakini iliyowakosha watu ni ile inayokwenda kwa jina la “Boda-Boda”. Boda-Boda ni usafiri wa pikipiki wa kule nchini Uganda. Pikipiki kule zinaitwa boda-boda kwa sababu kukiwa a foleni zinachepuka na kupita vichakani.

sauti-day-3-047_kirye2.jpg

Hawa ni baadhi ya mashabiki wa bwana Kirya wakifuatilia kwa makini ujuzi wa jamaa wa kupiga gita na kuimba kwa madaha.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

NATIONAL TAARAB ALL STARS

Posted by Bob Sankofa on February 10, 2008

sauti-day-3-002_wazalendo.jpg

Jana tulikuwa nao hawa kwenye majira ya saa kumi na robo hivi. Ni wenyeji wa hapa Zanzibar na ni wakongwe wa muziki wa mwambao, taarab. Katika wote waliosimama kuimba katika kikundi hiki huyu dada ndiyo alinikosha sana kwa uzalendo wake, cheki anavyoitukuza bendera ya nchi yake.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | 2 Comments »

ERIC, MTOTO WA NYUMBANI

Posted by Bob Sankofa on February 9, 2008

sauti-day-2-132_eric-wainaina.jpg

“Ukitaka chai ewe inspector, nenda Limuru”, hayo ni maneno ya Erick Wainaina na bendi yake ya Mapinduzi toka katika ule wimbo wake wa “Nchi ya Kitu Kidogo”. Jamaa ana vionjo fulani kama vya Lokua Kanza halafu mashairi yake yameathiriwa sana na falsafa za kimapinduzi za Mau Mau. Haogopi kusema kweli kwenye nyimbo zake, anazo nyimbo za mapenzi pia lakini nazo zinakufanya ufikirie pia.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

MZUKA!

Posted by Bob Sankofa on February 9, 2008

sauti-day-2-120_mzuka.jpg

Huyu ni mcheza dansi wa Kouyate, hapa Ngoma Iongeayo inafanya kazi yake na dada kapandisha mzuka. Wanasema ngoma ni kiungo cha mawasiliano kati ya mwanadamu na Muumba wake ndio maana mkoloni alipoingia Afrika alipiga marufuku kwa kusema kuwa ngoma ni ushenzi. Ajabu leo wao ndio wachezaji wakubwa wa ngoma zetu, sisi wenyewe bado tunaziona ni za kishenzi 🙂

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

NGOMA IONGEAYO

Posted by Bob Sankofa on February 9, 2008

sauti-day-2-117_ngoma-iongeayo.jpg

Wanaita Talking Drum, sisi tunaita Ngoma Iongeayo. Ukiwauliza watu wa kule Afrika Magharibi, kama mpiga ngoma huyu wa bendi ya Kouyate, watakwambia kuwa bila kutumia lugha za kibinadamu tunazozifahamu watu wanaweza kuwasiliana kwa midundo ya ngoma hii. Ni kweli ngoma hii ikipigwa unazisikia kabisa silabi.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

N’FALY KOUYATE

Posted by Bob Sankofa on February 9, 2008

sauti-day-2-112_nfaly-kouyate1.jpg

Nafikiri muziki wa Afrika Magharibi ni wa aina yake kutokana na kiburi cha wasanii wake kugoma kabisa kutekwa na vifaa vya muziki vya ughaibuni.

sauti-day-2-112_nfaly-kouyate.jpg

Kouyate anatoka Mali lakini kwa sasa anaishi nchi mbalimbali za Ulaya ila ukisikiliza anavyolivurumisha kora unaweza ukasema jamaa ametoka Mali leo asubuhi.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

SECKOU KEITA

Posted by Bob Sankofa on February 9, 2008

sauti-day-2-049_sekou-keita.jpg

Anaishi Ulaya kwa sasa lakini ni mzaliwa wa Senegal. Anapiga Kora na pia kwa mara ya kwanza jana nikaona mtu anapiga kora pacha, hili ni kora lenye milingoti miwili kwenye mtungi mmoja.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

BLACK ROOTS

Posted by Bob Sankofa on February 9, 2008

sauti-day-2-010_black-roots.jpg

Hawa ni kati ya wenyeji kadhaa wa hapa Zanzibar wanaojumuika katika tamasha hili la kimataifa ili kuwafanya wageni kujisikia kuwa kweli wako Zanzibar. Wanachanganya vionjo vya muziki vya bara na pwani.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

SAKAKI MANGO

Posted by Bob Sankofa on February 9, 2008

sauti-day-2-002_sakaki-mango1.jpg

Jana ilikuwa ni siku ya pili hapa tamashani. Aliyefungua mshikemshike wa jana alikuwa ni Sakaki Mango, Mjapani anayeishi Tanzania na kupiga muziki wa kigogo.

sauti-day-2-007_sakaki-mango2.jpg

Muziki wa Kigogo ni moja ya miziki michache ya Kitanzania iliyobaki ambayo pia iko hatarini kupotea. Sasa kwa sababu Watanzania hatuwezi kuhifadhi vilivyo vyetu Sakaki anatusaidia.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

NIMEMFUMA TENA

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

 sauti-2-047_nimemfuma-tena.jpg

Tuko hapa Zanzibar na guru wa blogu za Kibongo, kaka Issa wa Michuzi. Hapa yuko migongoni mwa watu akijaribu kupata shoti ambayo wapiga picha wengine hapa ni ngumu kuzipata. Huo ndio unaitwa upiga picha, upate picha tofauti na jicho la mtu wa kawaida linavyoona mambo. Basi na mimi nikambaruza hii katika harakati zake.

Wakati mwingine, ngoja tukaendelee kukamata matukio.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

HUYU NI DADA WA BASSEKOU

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-2-157_amkosha-bi-kidude-2.jpg

Kwa sababu kaka yake hana muda wa kuimba basi dada anaziba pengo hilo. Dada anaimba…

sauti-2-157_amkosha-bi-kidude.jpg

…kukuhakikishia kuwa dada anaimba cheki Bi. Kidude alivyoshindwa kutulia kitini mwake hadi kuamua kumpa hongera zake. Ukipewa hongera na Bi. Kidude ujue kiwango chako si cha mchezo.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

BASSEKOU KOUYATE & NGONI BA

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-2-139_bassekou-kouyate-ngoni-ba-2.jpg

Anatoka Mali, chombo pekee cha mzungu anachotumia awapo jukwaani ni kipaza sauti. Vyombo vyake vyote kuanzi vile vya nyuzi hadi ngoma anatengenezea nyuma ya ua wa nyumba yake.

sauti-2-139_bassekou-kouyate-ngoni-ba.jpg

Bassekou anajua kizungu lakini ni kile cha Wafaransa ambacho wengi wetu hapa hatukistukii kwa hiyo huwa hana muda wa kuongea sana muda mwingi yeye anatwanga saundi tu.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

AHMED EL SALAM

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-2-094_ahmed-el-salam-2.jpg

Ni mwanamuziki toka Afrika ya Kaskazini, makazi yake kwa sasa ni Ulaya, Ufaransa. Bendi yake ni ya watu wa tatu lakini muziki wao ni habari nyingine, ni mzito wa kufa mtu.

sauti-2-094_ahmed-el-salam.jpg

Ahmed katika hisia kali.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Poetry, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

HAPA NDIO ‘HOME’ BWANA

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-2-067_maulidi-ya-home.jpg

Jamaa wanajiita Maulidi ya Home ya Mtendeni. Ni sehemu ya utamaduni wa watu wa Zanzibar. Huwezi kuzungumzia muziki wa jukwaani bila kuwataja mara mbili-tatu hawa jamaa. Wanapiga madufu na kuimba. Uchezaji wao ni huku wakiwa wameketi kitako. Safi sana.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MRISHO AENDELEZA LIBENENGE

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-2-048_mrisho-2.jpg

Nilishasema mshairi wa hapa nyumbani, Mrisho Mpoto, baada ya kusota sana hatimaye sasa anaanza kula matunda ya uvumilivu wake. Jamaa ni mtu wa kujinafasi kwenye majukwaa ya kimataifa tu sasa.

sauti-2-066_mrisho-1.jpg

Cheki anavyomuenzi somo yake, marehemu Mzee Shaaban Robert kwa kumwaga ubeti mmojawapo wa lile shairi lake la “Titi la Mama”

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Poetry, Safari, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

TAARAB INA MAMBO MENGI

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-2-041_taarab-na-mauno.jpg

Taarab ya kisasa si kuketi kitini tu na kuitikia mashairi kuna swala zima la kunengua pia. Cheki jamaa macho yalivyowatoka wakati dada akifanya ile kitu mashabiki wengi wanapenda, kung’unyuka.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »