MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for November, 2007

KAZI ZA MWANZO KABISA ZA TMH

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

film-screening.jpg

Kabla hata ya kuzinduliwa rasmi TMH wameshafanya kazi nyingi za kusaidia watoto yatima wanaoshi katika mazingira magumu, tena si jijini Dar pekee, hadi vijijini wameshakwenda. Wanamitindo wanaounda shirika lile, kwa kushirikiana makampuni kadhaa ya kibiashara na vyombo kadhaa vya habari, wamefanikiwa kutengeneza filamu fupi inayoonyesha kazi kadha wa kadha ambazo wameshazifanya katika harakati zao za kuhakikisha watoto yatima nao wanapata japo nafuu ya maisha. Hapa walikuwa wakituonesha filamu ile.

Advertisements

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

UZINDUZI WA TMH – HOTUBA

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

speech-guest-of-honor.jpg

Naibu Waziri wa Ulinzi, mzee Aboud, akitoa hotuba ya uzinduzi wa Tanzania Mitindo House huku baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba hiyo na paparazi wakihangaika kukamata kumbukumbu za kila jambo lililojiri katika hafla ile fupi iliyofanyika Coral Beach Hotel, Msasani.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

WANAMITINDO WA TMH

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

designers_tmh.jpg

Hawa ni baadhi ya wanamitindo wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Mitindo House ambao wameungana ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu baada ya kuachwa yatima na wazazi wao waliofariki kutokana na gonjwa la Ukimwi. Shirika linaundwa na wanamitindo saba na ukumbini siku hiyo walikuwemo wanne, watatu walikuwa nje ya Jiji na nchi kwa shughuli za kikazi, kwa mfano Masoud Kipanya wa kampuni ya mitindo ya KP, alikuwa Dodoma.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

TANZANIA MITINDO HOUSE YAZINDULIWA

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

cake_tmh.jpg

Hatimaye siku ya Jumamosi ya tarehe 23, shirika lisilo la kiserikali (NGO) linalokwenda kwa jina la Tanzania Mitindo House (TMH) lilizinduliwa rasmi pale hoteli ya Coral Beach, Msasani. THM ni NGO inayoundwa na wanamitindo wa Kitanzania, wakiongozwa na Khadija Mwanamboka (mwenye kitenge pichani).

Wanamitindo hawa wanaamini kwamba jamii imewapa sapoti kubwa sana kufikia mafanikio yao na kwa hivyo wanawajibika kurudisha kitu kwa jamii. Wanamitindo hawa wameungana na kuanzisha shirika hili ili kusaidia watoto walioachwa yatima, na wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na gonjwa la UKIMWI. Hadi siku ya uzinduzi shirika lilikuwa na watoto 30, walio katika mazingira mgumu kupindukia, ambao inawasaidi kwa hali na mali.

Mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Ulinzi, mzee Aboud (anayekata keki). Pia alikuwepo balozi wa Palestina (mwenye nguo nyeupe). Wanaoshudia ukataji keki kwa nyuma kule ni baadhi ya wanamitindo wengine wa shirika hilo. Tarehe1/12/2007 shirika limeandaa onesho la mitindo linalokwenda kwa jina la RED RIBBON FASHION GALA pale hoteli ya Move n Pick ambapo wanamitindo wataonesha kazi zao na asilimia 95 ya pesa zitakazopatikana zitakwenda kuchangia malezi ya watoto wale wanaoishi katika mazingira magumu. Tiketi za onesho ni TSHs. 100,000 kwa kichwa. KARIBU!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

USIKU MWINGINE WA USHAIRI

Posted by Bob Sankofa on November 23, 2007

poetry.pngDear Lovers, (of poetry I mean! what did you think?)

Poetry nite is here once more. We meet on Tuesday 27th NOVEMBER 2007, from 19H00 at A Novel Idea Slipway. Theme for the nite is “GROWTH”.

Swahili poems are strongly encouraged, or a poem in any language for that matter. We shall listen as you read, and probably ask for a translation.

We love to sit on the floor, so please bring a mat or cushion along, plus that friend who could get inspired somehow.

COME TO POETRY NITE
“Come one, come all,
Come read, or discuss,
the magical bliss,
of poetry’s kiss…

Come grab and munch,
Sip on wine or punch,
while we sit in a bunch,
on a big round couch…

All faces are happy,
broad and shiny,
lovely and ready,
To knock down poetry…

all the same thou,
if I were you Lou?,
Or Lisa Patlou?,
I wouldnt miss out,
on poetry nite…”

by Clara Swai
@2007

* Reminding each member to contribute TShs. 3,500/= for refreshments and drinks.
* Also visit our blog at http://fananiflava.blogspot.com for more insight into what we are all about.
* Mucho gracias to “A Novel Idea” staff and management, for sharing their space and time with us all. We
continue to enjoy the 10% discount on any book purchase

Asanteni,

Clara

co co coordinator

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

UTASHEREHEKEA WAPI NA VIPI UHURU WETU?

Posted by Bob Sankofa on November 23, 2007

independencedayinvitation.jpg

Kule Helsinki washajipanga na hii.

Posted in Africa, Bongo, Siasa, Tanzania | Leave a Comment »

HIVI BONGO MMEBAKIZA KITU KWELI? – MIHAYO

Posted by Bob Sankofa on November 23, 2007

michezo-kwa-watoto.jpg

Kaka Mihayo wa Finland ametuma nyingine tena, anasema, “Wadau hapa Finland katika kila ghorofa zinapoishi familia za Kifini ni lazima kuwe na sehemu ya kucheza watoto kama hii, sina hakika kama pale kwetu Da’Slama tumebakiza maeneo ya wazi kama haya maana nasikia kila kiwanja kina mmiliki binafsi na wote wanazo ramani mikononi, tayari kujenga kitu fulani na si kiwanja cha michezo. Sina shaka ndio maana hata kwenye michezo kimataifa huwa hatuwiki kabisa. Wenye mamlaka mtueleze iwapo Bongo tumebakiza japo kimoja kama hiki.”

Posted in Africa, Bongo, Fotografia, Kimataifa, michezo, Photography, sports, Tanzania, Wadau | 1 Comment »

MANZESE YA FINLAND – MIHAYO

Posted by Bob Sankofa on November 22, 2007

manzese-ya-finland.jpg

Kaka Mihayo wa Finland katutumia hii, anasema “Wadau mambo vipi? Nawatumia msongamano huu wa vijumba ambavyo Wafini wanapenda kuishi wakati wa kiangazi tu, kwa wakati kama huu wa baridi havina mtu ndani, maana hapa Helsinki karibia asilimia 80 ya watu wanaishi kwenye flats (magorofa yenye familia nyingi), sasa wakati wa kiangazi ukiwadia ndio wanapenda kubadlisha maisha kwa kuhamia humu. Wadau eneo hili halina mitaa, na nyumba hizi ni kama nyumba zetu za afrika, ambazo huwa wanazisimanga kwamba zimepitwa na wakati, kwa mfano vyoo viko nje, bomba la maji nje na pia wanapikia mara nyingine nje. Ni hayo tu kaka”.

Kaka Mihayo tunashukuru kwa sura mbadala toka Ughaibuni, tushirikishe zaidi kwa yanayojiri hapo Helsinki.

Posted in Fotografia, Kimataifa, Photography, Vijimambo, Wadau | 2 Comments »

NIKO KENYATTA

Posted by Bob Sankofa on November 21, 2007

niko-kenyatta.jpg 

Niko njiani kurejea nyumbani, nimeiba tarakilishi ya mtu mara moja kurusha hii. Niko uwanja wa Ndege wa Kenyatta, nasubiri ndege ya saa kumi jioni, namwambia mshikaji wangu hapa kando kuwa nimechoka kishenzi kusubiri, . Unajua ananijibu nini? Eti ninunue ndege yangu binafsi. Anyway, sitaki kuandika sana maana huyu niliemuomba tarakilishi ametoa macho kishenzi kuangali naandika nini, watu wengine bwana! Baadae kidogo.

Posted in Africa, Fotografia, Kimataifa, Photography, Safari, Tanzania | 3 Comments »

ZIWA VICTORIA KWA HUKU

Posted by Bob Sankofa on November 20, 2007

jinja-ziwa-victoria.jpg 

Nimefika Jinja. Ni mji umepooza kidogo lakini umepangika. Majengo yake mengi ni ya kikoloni hivi. Sina mpango sana na majengo yao nawahi moja kwa moja ufukweni mwa Ziwa Victoria. Ajabu sana, sehemu kubwa ya ziwa hili iko kwetu pale Mwanza lakini ni mara yangu ya kwanza kuliona ziwa hili, nikiwa ughaibuni lakini. Linavutia, ni ziwa hili linalotufanya watu wa Afrika ya Mashariki kuwa wamoja zaidi.

Posted in Africa, Fotografia, Kimataifa, Photography, Safari, Tanzania | 1 Comment »

MTERA YAO

Posted by Bob Sankofa on November 20, 2007

mtera-yao.jpg 

Kabla hujaingia Jinja mjini unakutana na bwawa hili kubwa la kuzalisha umeme, hii ndiyo Mtera yao. Hii ni sehemu ya mto Nile. Picha hii kidogo ilete mtafaruku maana hii ni moja ya zile sehemu wanaita NO PHOTO ZONES, ukionekana na kamera balaa. Polisi walitusimamisha ikabidi kuomba sana msamaha tena kwa Kiswahili (ambacho hawaelewi sana) ili mazungumzo yawe mafupi. Walituachia baadae.

Posted in Africa, Fotografia, Kimataifa, Photography, Safari | 2 Comments »

CHALINZE YA HAPA

Posted by Bob Sankofa on November 20, 2007

chalinze-ya-hapa.jpg

Ukiwa unaelekea Jinja kuna sehemu moja, jina sikufanikiwa kulipata, ni sehemu poa sana. Hapa ni kama vile pale Chalinze kwa watu wanaokwenda Morogoro au Kilimanjaro. Kuna hawa wafanayabiashara ya chakula wanauza kila aina ya chakula unachotaka wewe, zaidi nyama na ndizi za kuchoma. Yani hata ukitaka bata mzima, ngoma buku tano tu ya Kiganda, chini ya dola tatu za Kimarikani. Gari likitia timu tu kituoni jamaa hao kwenye madirisha.

Posted in Africa, Biashara, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Photography, Safari | Leave a Comment »

WANJA LAO LA NESHNO

Posted by Bob Sankofa on November 20, 2007

wanja-lao.jpg

Jamaa hapa Uganda walishatupiga bao zamani kishenzi kwa swala la wanja la neshno, wanaliita Mandela National Stadium. Wanja lao liko nje kidogo ya jiji la Kampala. Sasa wanaimarisha miundo mbinu ili iwe rahisi kufikia uwanja huo kwa magari mengi zaidi kwa wakati mmoja.

Posted in Africa, Burudani, Fotografia, Kimataifa, michezo, Photography, Safari, sports | 1 Comment »

MATOKE

Posted by Bob Sankofa on November 19, 2007

matoke.jpg 

Ukifika na kuondoka Uganda bila kula Matoke ni sawa na kutofika nchi hii na wenyeji wako watajisikia vibaya kwelikweli. Hakuna aina ya chakula kinachozalishwa kwa wingi katika nchi hii kama matoke na ni biashara kubwa sana inayopeleka mkono wa Waganda wengi kinywani. Hivi chakula kikuu cha Tanzania ni nini tena vile?

Posted in Africa, Biashara, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari, Tanzania | 1 Comment »

BODABODA

Posted by Bob Sankofa on November 19, 2007

bodaboda.jpg 

Usafiri wa pikipiki, maarufu kama bodaboda hapa Uganda ni almaarufu kwelikweli. Usafiri huu ni maarufu kwa sababu unawafikisha abiria wanakotaka kwenda kwa haraka. Barabara za hapa Kampala ni nyembamba na zina makorongo mengi kwa hiyo magari yanakwenda taratibu na kwa kusongamana sana. Ukitaka kufika ofisini au nyumbani kwa haraka chukua bodaboda, zinapita hadi uani mwa nyumba za watu. Tatizo zinabeba mtu mmoja tu kwa wakati kwa hiyo kama uko na my wife wako umeumia.

Posted in Africa, Burudani, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari | Leave a Comment »

WAFIA DINI

Posted by Bob Sankofa on November 19, 2007

kanisa-la-wafia-dini.jpg 

Hili ni kanisa la Wafia Dini wa Uganda, liko Kampala. Kanisa hili limejengwa kuwakumbuka watu 22 ambao walitiwa kiberiti wakiwa hai na Kabaka kwa kosa la kumpokea Yesu kama Mfalme wao wa Mbinguni na kuuasi utwala wa Kabaka. Wakristo huja kuhiji hapa wakitembea kwa mguu toka Nairobi na hata Afrika ya Kati. Mambo ya dini tuyaache kama yalivyo.

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Kimataifa, Photography, Safari | Leave a Comment »

HEKALU LA BAHAI

Posted by Bob Sankofa on November 19, 2007

hekalu-la-bahai2.jpg

Dini kubwa kabisa katika Uganda ni ile ya Wakristo, lakini nchi inatoa fursa ya kuamini na kuabudu dini yeyote uipendayo ilhali huvunji sheria za nchi zilizowekwa. Basi hapa kuna hekalu kubwa kabisa katika Afrika la dini ya watu wa Bahai. Sikuruhusiwa kupiga picha ndani ya hekalu. Hekalu hili ni kivutio kikubwa sana hapa Uganda.

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Kimataifa, Photography, Safari | Leave a Comment »

IKULU YA KABAKA

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

kabaka-nje.jpg 

Naelekekea Jinja lakini mwenyeji wangu ananiambia haitakuwa vyema kwenda huko kwanza kabla ya kupita kwenye himaya ya Kabaka ama Mfalme Mutesa na nduguze na kutoa salamu pale. Basi tunaingia hapa kupata historia ya siasa za Uganda kabla na baada ya ujio wa watu weupe katika nchi hii nzuri.

kabaka-ndani.jpg

Hapa ni ndani ya Ikulu ya himaya ya Kabaka. Tunaambiwa Kabaka Mutesa alikuwa na wake 85 tu. Jamaa aliruhusiwa kuoa katika koo zote kasoro ile aliyokuwa akitoka mama yake mzazi. Lakini kuna kitu kinanishtua, Wafalme karibu wote wa himaya hii ya Buganda walikuwa wakifariki vijana wadogo kabisa, hakuna aliyezidi miaka 55. Hapakuwa na Ukimwi kipindi hicho kwa hiyo mimi nahitimisha kwa kusema labda vifo vile vilisababishwa na kufanya ngono sana na hivyo kupoteza nguvu nyingi mwilini, totoz 85 si mchezo ati.

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari, Siasa, Tanzania | 1 Comment »

MIUNDO MBINU

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

flyovers.jpg 

Naweza sema hadi sasa, Dar imewapiga bao Kampala kwa barabara nzuri lakini kuna hatari baada ya miaka mitano kama hatutafanya kitu hawa jamaa watasawazisha na kuongeza mabao kadhaa. Jamaa si kwamba wanaota tu kuhusu barabara za ghorofa, tayari wanafanya kitu. Yote hii ni harakati za kupunguza msongamano wa magari ili uchumi ukue haraka.

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari, Tanzania, Teknolojia | Leave a Comment »

KAMPALA FULL MISHEMISHE

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

kuchomekeana-tu.jpg 

Nilikuwa nadhani Bongo ndio inaongoza kwa kuchezeana rafu barabarani (uendeshaji mbaya). Kampala ni zaidi, hadi baiskeli na waenda kwa miguu “huchomeka” mtu wangu. Kila mtu anawahi sehemu fulani. Dereva wangu ananiambia  hapa gari lako linaweza kukamatwa na kusamehewa kwa makosa mengine yote lakini si makosa ya kutokuwa na breki na honi mbovu. Vitu hivyo viwili ni lazima viwe vizima ama sivyo ni mwendo wa faini tu. Hapa ni katikati ya Kampala, naelekea Jinja.

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari | Leave a Comment »

WANAMKUTANO WA TELEVISHENI NA MAZINGIRA

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

mkutano.jpg

Mataifa kumi na sita ya Afrika kila mwaka hukutana kujadili nguvu ya televisheni katika kutoa elimu ya mazingira kwa umma. Mwaka huu tumekutana hapa Uganda na mwakani tunakutana tena kule Sierra-Leon. Hawa ni wahudhuriaji wa wa mkutano huo. Wale wazungu wawili, wakinamama, ndio watoa fedha wenyewe, huyo wa kiume ni Mreno wa Msumbiji. Naupenda mkutano huu kwa sababu suti na tai sio lazima

Posted in Africa, Filamu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari, Tanzania | Leave a Comment »

NIKO KAMPALA

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

niko-kampala.jpg

Niko hapa tangu tarehe 14 jioni. Kama nilivyosema hapo awali niko hapa kuhudhuria mkutano mkubwa wa Watu wa Jumuiya ya Madola lakini pia niko hapa kuhudhuria mkutano wa Televisheni na Mazingira. Basi hawa jamaa wa Televisheni na Mazingira walikuwa wametutupa mahala fulani ambako kupata mtandao ilikuwa ni ndoto. Eti walitaka tuweke mawazo yetu yote kwenye mkutano.

Uganda, mara yangu ya kwanza hapa. Nchi poa sana, milima, miti ya kutosha na mvua za kutosha pia. Naweza kutembea hata saa saba ya usiku bila wasiwasi. Watu hawalali hapa. Poa sana, tatizo ni kuwa wanasiasa wamekuwa “wakiibaka” nchi hii tena na tena.

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari | 1 Comment »

MAELEZO TAFADHALI

Posted by Bob Sankofa on November 13, 2007

li12.jpg

Linda, dada wa Richard ambaye ni mshindi wa shindano la Big Brother Africa II, akiwa na Tatiana, mshiriki wa shindano hilo toka Angola mara baada ya kidingi Riki kushinda mamilioni ya fwedha pale Kusini. Swali; Je inawezekana tunavyodhania tulio wengi juu ya mahusiano ya washiriki hawa ndivyo ama lah? Naona mtoto anakubalika hadi kwa Jakaya (Tanzania). Kama kuna mwenye maelezo tafadhali tudondosheeni, yawe na TBS lakini, yasiwe ya kubunibuni 🙂

Picha na http://www.issamichuzi.blogspot.com

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Kimataifa, Photography, Tanzania, Vijimambo | 6 Comments »

HODI HODI KAMPALA

Posted by Bob Sankofa on November 12, 2007

39499420img_0211.jpg

Haya wadau na marafiki wa Uganda, ni wakati mwingine wa mikutano na kukutana. Nitakuwepo jijini Kampala kwa mkutano wa Jumuiya ya Madola pamoja na mkutano mwingine wa masuala ya Televisheni na Mazingira kuanzia keshokutwa, 14/11 hadi 21/11. Susan Bamutenda nitafurahi sana ukinipeleka mtaa huu kwenda kukutana na Waganda pamoja na kupata matoke na halafu baada ya hapo, Uganda by night. Sanaa Gateja nitapenda sana kutembelea duka la sanaa zako, Andrew Mwenda tukutane kwa kikombe cha chai (nimestaafu mvinyo kwa muda 🙂 na tuzungumzie siasa kidogo). Hodi hodi Kampala!

Picha kwa msaada wa Google

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography | 2 Comments »

MIJIHELAAAAA!

Posted by Bob Sankofa on November 11, 2007

richies.jpg

Sioni aibu hata kidogo kusema blogu zina nguvu kubwa sana katika kubadili upepo wa matokeo ya kitu fulani. Kwanza ilikuwa Juma Nature juzijuzi pale kwenye tuzo za muziki za Channel O, akanyakua ile kitu kwa nguvu ya kura ya wadau. Halafu leo usiku, baada ya kampeni ya kutosha tu, Richard ametutoa tena kimasomaso pale Kusini. Ameondoka na kitita chao cha dola 100,000/=, HONGERA RICHARD! Napenda pia kuzipongeza blogu hasa ile ya kaka Michuzi na kaka Jeff kwa shughuli pevu ya kuhamasisha wadau kunyuka kura. Siwezi kuacha kuwapongeza pia wadau wa blogu zote za kibongo.

PAMOJA!

Picha kwa msaada wa http://www.issamichuzi.blogspot.com

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Kimataifa, Photography, Sherehe, Tanzania | Leave a Comment »

NA MALKIA WA NGWASUMA NI…

Posted by Bob Sankofa on November 11, 2007

malkia-wa-ngwasuma-ni.jpg

Ketura Kihongosi ndie Malkia wa miondoko ya Ngwasuma. Fainali ilikuwa juzi usiku pale Diamond Jubilee Hall, ule ukumbi mkubwa. Sikufanikiwa kukamata tukio lile laiv maana wakati huohuo nilikuwa kule kwenye ukumbi wa VIP kukamata tukio la Mbunifu Bora wa Redd’s. Lakini hujakosa chochote, bonyeza hapa kwenda blogu ya Bongo Celebrity ukaone mchuma aliojishindia dada. Picha hii nilimpiga kwenye nusu fainali za mchuano huu mwezi September mwaka huu. Dada alionyesha kila dalili ya kushinda tangu mwanzo kabisa. Hongera sana Ketura!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Tagged: | Leave a Comment »

KIKWETE HEBU NJOO TUUZE SURA KIDOGO

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

familia-na-rizwan.jpg

Hili ndio lilikuwa snepu la kufungia usiku wa jana. Hapa tulikuwa tuko kwenye harakati za kukamata usafiri tayari kurudi makwetu, mara Rizwani huyo. Nikamwambia my better half (mwenye kilemba), “Kama hatuwezi kupiga picha na ze prezident himselifu kwa nini tujivunge kunyuka na ze boi himselfu?” Hatukujiuliza mara mbili, fasta tukamkamata jamaa na kunyuka hii. Ze boi iz luk laik faza kabisa 🙂 . Huyo dada wa kizungu ni mmoja wa wadau wa blogu hii ambaye huitumia kujifunza maneno kadha ya Kiswahili kila siku, anaitwa Thea.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | 4 Comments »

IRENE UKO JUU!

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

familia-na-irene.jpg

Huwezi kuzungumzia vicheko, furaha na chereko za shughuli ya jana ya Mbunifu Bora wa Redd’s bila kumtaja Irene Kiwia. Dada na timu yake ndio alikuwa mratibu mkuu wa shughuli nzima. Kabla ya shughuli kufanyika hatukuweza kabisa kula nae snepu maana alikuwa anazunguka kama pia. Foto hili tumenyuka nae baada ya mchakamchaka wa kufa mtu. Kushoto kabisa pale ni my better half, Mwandale Mwanyekwa (the best female sculptor in town), halafu Irene (with a winning smile), halafu mshikaji wangu wa miaka tele, Freddy Halla (the cartoonist of all time), na halafu mimi niko kwa nyuma kule katika harakati za kuhakikisha na mimi natokea kwenye msenepu huu wenye watu muhimu. Hapo nilipo usinione natabasamu, nimesimamia vidole gumba vya mguu, Irene ni mrefu mno, nimetokea lakini.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | 5 Comments »

SAGANDA APATIKANA

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

freddy-na-chris.jpg

Yani nakwambia jana full vituko, full furaha, full vicheko pale Diamond Jubilee. Saganda amezoea kuwatesa watu na urefu wake. Kwa kifupi ni kuwa ni watu wachache sana ambao wanalingana na huyu bwana kwa kimo. Sasa akabugi stepu akidhani urefu ni sawa na ukubwa wa mwili, mara kikatokea kifaa hiki, Chris (mwenye kofia) jamaa ni kipisi cha mtu. Saganda akaanzisha ubishi kuwa yeye anamwili mkubwa kuliko Chris, tukasema tusiandikie mate wakati wino upo. Tukawaweka pamoja ili wapimane, cheki mambo hayo. Saganda anaweza kubishana hata na radio kwani bado haamini kuwa yeye ni kibonde kwa Chriss 🙂

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

K-LYN NA WASHKAJI

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

ntuyabaliwe2.jpg

Vyombo vya habari noma sana, huwa vinakuza watu kupita maelezo kiasi kwamba hata ukikutana na watu wale wanaokuzwa kivile unaweza ukaogopa hata kuwasalimia. K-Lyn, mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo na ambaye pia amewahi kuwa Miss Tanzania, alikuwepo jana kwenye shughuli ya Redd’s. Basi nikajipitisha mara ya kwanza nikitaka kula snepu lakini nikasita kwa kuhofia kutolewa nishai, nikarudi mara ya pili nikatabasamu kidogo na yeye akatabasamu, sikuchelewa nikabaruza hii. Dada hana makuu kabisa, akanipa ruhusa ya kubaruza foto zingine kama tano hivi, nimeziweka maktaba kwa matumizi ya baadae.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »