MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for September, 2007

PIGIA KURA FILAMU YA “PLAY YOUR PART”

Posted by Bob Sankofa on September 29, 2007

Juzi niliandika kuwa filamu yangu ya “PLAY YOUR PART” imependekezwa kuwa moja ya filamu zinazoshindania tuzo kubwa kabisa ya filamu za sinema Afrika, tamasha linafanyika London. Tafadhali bonyeza hapa usome habari ile. Kwa bahati nzuri siku hizi mambo yamebadilika sana, wanaochagua mshindi wa tuzo ile ni watu kama wewe amabo wanapiga kura kuichagua filamu wanayotaka ishinde tuzo ile.

Hivyo basi, ninakuomba wewe mdau wa blogu hii ubonyeze hapa halafu kwenye ukurasa ule kuna kundi linaitwa “BEST DOCUMENTARY FEATURE” pale utaiona filamu ya “PLAY YOUR PART” amabyo hadi sasa ndiyo yenye kura nyingi zaidi ya filamu shindani toka Zambia na Uganda.

Naomba uipigie kura “PLAY YOUR PART” kabla giza halijaingia na unisaidie kumwambia na rafiki yako apaige kura pia ili Filamu na Tanzania vitoke kimasomaso. Endelea kupiga kura kila siku hadi tarehe 6/10. Asante.

PAMOJA!

Advertisements

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Filamu, Fotografia, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania | 6 Comments »

TREALA LA FILAMU MPYA YA KIBIRA

Posted by Bob Sankofa on September 29, 2007

Kaka Josiah Kibira, yule mtengenezaji wa filamu za Bongoland ametutumia hii leo asubuhi kupitia ukurasa wa CHANGIA.

Anasema, “Kaka Sankofa na wadau wote wa blogu na filamu, pokeeni hii tafadhali. Hii ni trela ya filamu ya Afrika MAshariki iliyotengenezwa na watu wa Afrika Mashariki. Ni filamu ya aina yake iliyotengenezewa pale Dar es Salaam kiangazi kilichopita. Vipaji na viwango vilivyo onyeshwa na waigizaji wa Kitanzania ni vya hali ya juu mno na vina nafasi kubwa ya kubadili mtazamo wa dunia ya filamu. Hebu cheki hiyo trela hapo juu”

Unaweza pia kumtembelea Kibira na timu yake hapa http://www.kibirafilms.com

Uongozi wa Mwenye Macho unakushukuru sana kaka Kibira kwa kushirikiana nasi sehemu ya uhondo huu.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Filamu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania, videokasti | Leave a Comment »

UNADHANI UNAMCHUKIA BWANA “KICHAKA”?

Posted by Bob Sankofa on September 28, 2007

bush.jpg

Niliwahi kudhani kuwa mimi ndiye mtu anayechukia siasa chafu za Joji “Kichaka” kuliko watu wote duniani, halafu akatokea Ndesanjo Macha ambaye ndiye aliyeanzisha jina hili la “Kichaka” akimaanisha jina la pili la bwana Joji, yaani Bush. Sasa leo katika pita pita yangu katika kurasa za www.facebook.com nikakutana na wapiga picha wanaomchukia “Kichaka” mara mia zaidi ya Ndesanjo.

Cheki picha hii halafu uitafsiri kwa makini, Kichaka hapa ni kama anakuuliza, “Vipi msomaji, na wewe unataka huduma hii?” 🙂 .

Picha imetengenezwa na kuunganishwaunganishwa kwenye Photoshop. Huyu aliyetengeneza ni ‘mtambo’ kwelikweli. “Kichaka” umeiona hii? Hatochelewa kusema blogu hii ni ya ‘kigaidi’ akiiona picha hii.

Cheki hii pia,

kichaka.jpg

Posted in Africa, Art, Fotografia, Kimataifa, Photography, Sanaa, Siasa, Teknolojia, Vijimambo | Leave a Comment »

ULALE PEMA PEPONI MZEE KADUMA

Posted by Bob Sankofa on September 27, 2007

kaduma.gif

Picha hii ni kipande cha filamu ya “Harusi ya Mariamu”, ili kupata shahada yangu ya kwanza katika maswala ya filamu za Kiafrika ilinibidi kutumia filamu hii kujibia maswali ya mtihani wa filamu.

Kushoto ni Profesa Amandina Lihamba, mwalimu wangu wa somo la uongozaji wa filamu na michezo ya jukwaani (Directing) pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni msanii mkongwe wa fani ya maigizo Tanzania, marehemu mzee Godwin Kaduma. Kwa mujibu wa habari zilizosambaa kwa kasi mchana wa leo katika jiji la Dar es Salaam ni kuwa Mzee Kaduma ametutoka, ametutangulia mbele ya haki. “Mwenye Macho” inaungana na wadua wote wa fani ya sanaa na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja ama nyingine katika kuomboleza kifo cha baba wa sanaa ya maigizo Tanzania, Mzee Kaduma. Mola Ametoa, Mola Ametwaa…

Picha kwa msaada wa Google Search Engine

Posted in Africa, Art, Bongo, Elimu, Filamu, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

HODI HODI LONDON, LEICESTER HADI COVENTRY

Posted by Bob Sankofa on September 27, 2007

zafaa_header.jpg

Ukiangalia ukurasa wa “Mimi ni Nani” hapa bloguni utaona kuwa kazi moja wapo ninayofanya ni kutengeneza filamu. Kwa maana nyingine mimi ni mtengeneza filamu. Mwaka jana nilipata bahati ya kutengeneza filamu fupi ya dakika kumi na tatu inayokwenda kwa jina la “Play Your Part” kwa ushirikiano wa shirika lisilo la kiserikali la White Ribbons Alliance Tanzania. Filamu ile inahusiana na swala zima la afya ya uzazi salama kwa mama na mtoto. Bofya hapa kusoma zaidi kuhusiana na filamu ile na pia unaweza kuitazama filamu hiyo kwenye ukurasa huohuo.

Filamu ya “Play Your Part” imechaguliwa kushindania tuzo za Annual African Film Academy Awards (ZAFAA, 2007), kama filamu fupi bora. Tamasha litafanyika pale London, UK kwa siku sita, yaani tangu tarehe 2 hadi saba. “Mwenye Macho” kama kawaida itakuwepo kuwakilisha, nadhani mambo ya mtandao hayatakuwa kama ilivyokuwa kwenye Digital Indaba pale Kusini. Nimealikwa kwenda kupokea zawadi ile kwa niaba ya timu nzima iliyoshiriki katika uandaaji wa filamu ile.

Napiga hodi kwa wenye jiji la London, kaka Freddy Macha lazima twende kikombe kupata kikombe cha kahawa ya Brazil.

Baada ya siku zile sita pale London nitaomba kuwatembelea wadau pale Leicester tupate mvinyo kidogo na kubadilishana mawazo. Sitakomea hapo, Rabia na Amulo, nakuja Coventry, nataka kukutana na wadau wangu hapo kwa masaa machache kabla ya kurejea tena Leicester tayari kwa kurudi kwa Jakaya tarehe 13/10.

Wadau wa miji mingine mtanisamehe, nimepewa likizo ya siku kumi na nne tu kibaruani kwangu, ila msikonde nina viza ya miezi sita na tayari kuna wadau wameshanialika kwenye sikukuu ya Noeli kwenda kuchezea barafu kwa hiyo tutaonana mwezi wa kumi na mbili.

Posted in Africa, Art, Burudani, Filamu, Fotografia, Kimataifa, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania | 3 Comments »

“WAPI” IMEWADIA TENA

Posted by Bob Sankofa on September 27, 2007

wapi.jpg

Yawaletea

Wasanii wa sauti ya handaki(undeground), Katika harakati.
Madjei, ma emsii, machata, mabreka ,michoro mbali mbali, ushairi,ngoma, maigizo na usanifu mitindo.

Mahali: British Council, Dar Es Salaam
(maelekezo: Samora na Ohio, mkabala na Steers kati kati ya jiji)

Jumamosi, 29-09-2007 mida; saa 6 -mchana-hadi 11 jioni

Mada ya mwezi: Amani Tanzania, Baraka au Laana?

Mgeni wa Mwezi: Jenerali Ulimwengu

karibuni wote- kiingilio BURE

wapi.jpg

Jukwaa la harakati za ukombozi kwa kutumia sanaa

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Filamu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Siasa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

USHAIRI MURUA NA MVINYO MURUA

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

img_3096.jpg

Dada Neema Kambona, binti wa mmoja wa wanasiasa wa mwanzo Tanzania, Oscar Kambona, naye alikuwepo kusema machache. Ninaposema tungo murua huambatana na mvinyo murua nadhani unanielewa sasa. Tazama picha hii kwa makini utaelewa ninamaanisha nini. Inasemekana hata wanafalsafa wa miaka hiyo walihitaji mvinyo kidogo ili kuwawezesha kufikiri zaidi ya wanadamu wa kawaida.

Mkutano wa mwezi ujao utafanyika tarehe 30/10, palepale Slipway, utakuwa ni mkutano wa kukata na shoka kwani Kilabu kinatimiza miaka miwili tangu kuundwa kwake. Tafadhali njoo wewe na rafiki yako, njoo na tungo ama bila tungo, yote ni heri. MVINYO UTAKUWEPO!

Picha na: Bob Sankofa
Mahali: Slipway, Dar es Salaam

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kimataifa, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 2 Comments »

MZEE WA PAPO KWA HAPO

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

img_3110.jpg

Sunday, jamaa ni mshairi matata sana. Ana kipawa kikali sana katika swala zima la kuibuka na tungo za pao kwa hapo. Tofauti na wengine, yeye alifanya mashairi mawili, la kwanza ni “Like the saying Goes…” na kisha akafanya “Fear and Fear Itself”. Hili la pili alilitunga tukiwa tumekaa pale kilabuni.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MAKOSA NI MAPITO

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

img_3113.jpg

Claire (yule dada aliyemhamasisha Gladys kutunga tungo yake) amekuja na shairi lake liitwalo “Experiment”. Yeye anaamini makosa katika maisha ni sawa na mapito au majaribu ambayo mtu hapaswi kuyakwepa bali kupambana nayo. Anamaliza, ni kama vile tumepigwa ganzi, tungo maridhwawa hasa. Haya Claire ni lini tena wenda Epidor? Inaelekea ni mahala safi sana pa kutafutia stimu za kufanya tungo, tunamuuliza, anatabasamu na kupiga funda la mvinyo.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

KILA MTU ANAWEZA…

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

img_3102.jpg

Tulikuwa na Gladys Fahari pia. Gladys anatuambia kuwa alihamasika kuandika tungo yake baada ya kukutana na Claire (Dada wa kizungu, mmoja wa washairi tutamuona punde) pale Epidor, bila shaka mkutano ule lazima ulikuwa na mvinyo -) . Gladys pia anatuambia hii tungo anayoghani hapa sasa, “Mistakes”, ni tungo yake ya kwanza katika maisha yake aliyoiandika mwaka mmoja uliopita baada ya kuja hapa kilabuni. Inapendeza, huwezi kuamini kuwa hiki tunachokisikia hapa kinatoka kwa mtu ambaye hii ilikuwa ni tungo yake ya kwanza. Kila mmoja wetu anaweza.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

TUNGO YAKO NI TASWIRA YAKO

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

img_3123.jpg

Carol, huyu mrembo, kama ilivyo mimi, naye ni mgeni hapa kilabuni. Anaghani tungo yake aliyoitunga mwenyewe, inaitwa “The knowing smile”. Nasikiliza tungo hii halafu namwangalia dada huyu, halafu tabasamu lake kisha najisemea moyoni, “Laiti angejua kuwa shairi hili ni taswira yake… basi tu!” Tungo yake ni nzuri sana kwa kweli, nzuri kama yeye mwenyewe alivyo mzuri.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

HADITHI FUPIFUPI

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

erick.jpg

Upande wa kulia kabisa ni Eric ambaye alitusomea hadithi fupi inayokwenda kwa jina la “The Butterfly”. Kumbe mkutano ule haukomei kwenye ushairi pekee, hata hadithi fupi zina nafasi yake pia. Eric alipomaliza kusoma hadithi yake akatuacha na fundisho kuwa maisha ni mapambano – na mapambano yale yana nia moja tu, kutufanya kuwa watu bora zaidi, inatufunza kuwa na moyo wa kujaribu. Mwenye fulana nyekundu ni Nassos, halafu Natasha na mwisho Clara.

Picha na: Bob Sankofa
Mahali: Slipway, Dar es Salaam

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

USHAIRI – MSICHANA NA NAMBARI 8

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

clara.jpg

Clara Swai, huyu ni mmoja wa waratibu wa jumuiya ya washairi wa bongo. Hapa alikuwa anaghani tungo yake inayokwenda kwa jina la “A Girl and the Number 8”. Ni tungo iliyojifumba kiasi na inamchambua kwa undani mwanamke tangu akiwa na umri wa miaka 8 hadi 68.

Picha na: Bob Sankofa

Mahali: Slipway, Dar es Salaam

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kimataifa, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

JUMUIYA YA WASHAIRI WA BONGO

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

img_3105.jpg

Hii ni Jumuiya wa washairi wakiwa wameketi ndani ya duka la A Novel Idea wakisikilizishan tungo zao. Kile kiti pembeni ya yule mzugu mwenye kaptura ni cha kwangu mimi, kama umeangalia kwa makini utaona kwa chini kuna bilauri ya mvinyo 🙂 . Naam Ushairi murua huambatana na mvinyo murua.

Tatizo ukiwa mpiga picha ni vigumu kutokea kwenye picha zako, nimetamani sana kutokea kwenye picha za mkutano huu lakini haikuwezekana.

Picha na: Bob Sankofa
Mahali: Slipway, Dar es Salaam

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kazi, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 3 Comments »

USIKU WA USHAIRI

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

img_3085.jpg

Kila Jumanne ya mwisho ya mwezi washairi wanakutana pale katika duka la vitabu la Novel Idea, Slipway, Dar es Salaam. Washairi wanaghani tungo zao na wengine wanasikiliza, kisha wanajadili tungo zile na kuzungumza na watunzi kuhusu kilichopelekea kutungwa kwa tungo zile. Kila mkutano huwa na kauli mbiu, kauli mbiu ya mwezi huu, yaani tarehe 25/09, ilikuwa ni “MAKOSA” au kwa kimombo”MISTAKES”. Jana ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria mkutano ule na katu sitoacha.

Picha na: Bob Sankofa

Mahala: Slipway, Dar es Salaam

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

KUTANA NA JOKATE – VIPAJI MIA MIA

Posted by Bob Sankofa on September 26, 2007

img_3046.jpg

Unamfahamu Jokate? Wamfahamu vipi?

Mrembo, mwanamitindo, msimamizi wa shughuli (MC), mtu maarufu, Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, mrembo aliyevutia sana mbele ya kamera (Miss Photogenic) kwenye shindano la Miss Tanzania mwaka 2006. Unafahamu nini zaidi ya hayo?

img_3065.jpg

Ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ila kuna hii moja sikuwahi kuifahamu hadi hivi juzi, Jokate pia ni mdau mkubwa katika swala zima la utengenezaji wa matangazo ya radio, sauti yake inauzwa kwa gharama ya aina yake.

img_3052.jpg

Jokate akiwa katika studio za MFDI – TZ na mmoja wa maprodyusa wanaoheshimika Tanzania, Hermis Bariki (Hermy B). Hapa wanapitia script za tangazo la Coca-Cola, tangazo hili litaanza kuruka maredioni muda si mfupi.

Mwenye Macho inapenda kumpongeza Jokate kwa kung’amua vipaji alivyonavyo na kuvitumia ipasavyo.

Picha na: Bob Sankofa
Mahali: Studio za MFDI – TZ

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Photography, Sanaa, Tanzania | 4 Comments »

HONGERA MICHUZI

Posted by Bob Sankofa on September 25, 2007

Blogu mama ya fotografia Tanzania, www.issamichuzi.blogspot.com leo inatimiza miaka 2 tangu kuazaliwa kwake pale Helsinki, Finland. Baba yake, Issa Michuzi akafanya kila jitihada kuhakikisha mtoto yule anabaki na Utanzania wake japo kazaliwa ughaibuni. Leo mtoto wa Michuzi anazungumza Kiswahilikuliko hata waliozaliwa Tanzania na watu wanamsikiliza na kumtazama kwa jicho la matamanio ya ajabu. Mtoto wa michuzi ni jicho la Watanzania walio wengi hasa wale waishio ughaibuni ambao wasingependa kupoteza taswira ya nyumbani.

Kaka michuzi amefanya pia mahojiano ya maadhimisho haya kule kwenye blogu ninayoiheshimu mno ya Bongo Celerity, bofya hapa ucheki ameosha vipi kinywa. Msemo wa “waosha vinywa” ni msemo uliorutubishwa kwa kiwango kikubwa sana na blogu ya Michuzi.

Mtembelee Michuzi na umpe hongera zake. Sherehe hii ya kuzaliwa kwa mtoto wa michuzi itadumu kwa siku saba.

Picha kwa hisani ya http://www.bongocelebrity.com

Posted in Africa, Blogu za Kiswahili, Bongo, Fotografia, Kazi, Photography, Tanzania, Teknolojia | Leave a Comment »

USHAIRI! USHAIRI! USHAIRI!

Posted by Bob Sankofa on September 24, 2007

Hi fellas,
It’s that time where we meet again for Poetry. Tomorrow nite, Tuesday 25th of Sep. 2007 from 19H30 onwards, at A Novel Idea – Slipway.Theme for the nite is “MISTAKES”.

Bring a poem, bring a friend along, lets have fun once more with lots to drink and digest!

I would love to remind you of the following:-members contribute at least Tshs. 3,500/= per person per nite, to cover refreshments.-A treasurer has to be appointed-

Visit our blog at www.fananiflava.blogspot.com for an insight of what we are all about-Lets consolidate ideas for our 2nd anniversary slam jam function

Be there!

See ya!

Co co coordinator

Clara

Pichani ni Linda Gabriel, mshairi toka Zimbabwe. Picha hii tumetumiwa na Linda.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Elimu, Mikutano, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

WAJINA NISHAI KISHENZI

Posted by Bob Sankofa on September 24, 2007

Mambo si kalinye  kwa sana (sio mazuri) huko kwa mzee Bob Mugabe (Zimbabwe). Mshikaji wangu Sue toka Cape Town amenitumia hii leo. Jamaa alitembelewa na washkaji zake toka ughaibuni akajitutumua kuwatoa kwa chakula cha mchana. Mabulungutu haya anayoacha katika picha hii ni tip kwa mhudumu aliyewahudumia, bili ameshalipia.

Uchumi wa Zimbabwe unazidi kuanguka siku baada ya siku na inasemekana kuwa zimebaki siku chache mno kwa watu wa Zimbabwe kuacha kutumia pesa kwani thamani yake imeparaganyika kabisa, biashara itabidi ziendeshwe kwa ule mtindo wa kubadilishana bidhaa na huduma (Barter Trade).

Mzee Bob anasema na bado, hata “wakubwa” wambane vipi bado atakomaa nao tu. Kuna tetesi kuwa katika jamii ya watu wa Zimbabwe kwa sasa kile kinachoitwa “Tabaka la watu wa kawaida” hakuna tena. Kuna matabaka mawili tu, yani “Matajiri” na “Masikini”. Yote hii ni kutokana na mchezo wa siasa chafu. Mugabe ndiye bwana mkubwa pekee Zimbabwe imepata kuwa naye toka uhuru mwaka 1980.

 

Posted in Africa, Biashara, Fotografia, Kimataifa, Photography, Siasa | Tagged: , , , , , , , | Leave a Comment »

UNATAKA KUWA TAJIRI FASTAFASTA?

Posted by Bob Sankofa on September 20, 2007

malaika.jpg

Nimetumiwa hii sasa hivi kwa njia ya barua pepe, eti wanasema huyu ni Malkia wa Pesa, Malkia wa Utajiri. Eti ukiwatumia rafiki zako sita unaowapenda picha hii unakuwa tajiri wa kutupa ndani ya siku 4 na iwapo utaituma kwa rafiki zako kumi na mbili unampiku Bill Gates ndani ya siku mbili tu, kudadadeki. Jamaa anasema “Hatanii”, sijui nani kamwambia anatania.

Sasa mimi nikaona isiwe tabu, naitupa hapa bloguni ili niwe tajiri ndani ya sekunde kadhaa maana hapa nina marafiki 200 wanaotembelea karibu kila siku. Hata nikiwa tajiri kublogu siachi 🙂

Haya sasa wadau, let’s get rich kirahisirahisi! Kiukweli ni kuwa hiyo message haijanimuvuzisha kabisa ila nimependa utundu wa jamaa kwenye swala zima la matumizi ya Photoshop (hii ni program ya kurembesha picha). Jeff unaweza kutengeneza kama hii.

Posted in Fotografia, Photography, Sanaa, Vijimambo | 2 Comments »

TANGAZO! TANGAZO! TANGAZO!

Posted by Bob Sankofa on September 20, 2007

Je wewe ni msanii, Huna kundi, Ungependa kutoka kisanaa?

Majibu yako yote yanajibiwa na YAMOYA ART GROUP, kundi la ki-Tanzania kwa kushirikiana na THE SUNY kutoka Kenya.

Wanatafuta wasanii wenye vipaji ambao hawajawahi kuigiza sehemu yoyote ili waandaliwe kwa sanaa ya maigizo ya filamu.

Kikubwa ni nidhamu na kujituma.

Wanapatikana Club Afri Center, Msimabzi center, mkabala na Lamada Hotel,Ilala.

Mwisho wa kupokea wasanii ni tarehe 25/09/2007. Njoo wewe, yule na wao. Usimsahau rafiki yako!
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0713 364 175 au 0755 217 383 e-mail justinkasyome@yahoo.com.

Karibu YAMOYA ART GROUP, tujenge mapinduzi ya kweli ya sanaa ya Tanzania inayokua kwa kasi.

Posted in Africa, Bongo, Filamu, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MUNGU KUBURUZWA MAHAKAMANI

Posted by Bob Sankofa on September 19, 2007

suing_godsffembeddedprod_affiliate79.jpg

Seneta Ernie Chambers wa jimbo la Nebraska kule Marekani amesonga kwenye vyombo vya habari na kusema lazima ampeleke Mungu mahakamani na ikiwezekana atamtupa lupango kabisa. Naandika habari hii nikiwa uvunguni mwa meza maana hii habari nzito, “Kumshitaki Mola!!!”. Mbona sisi hata kumshitaki rais hatuwezi?

Kwa nini Chambers kaamua kumburuza Rabuka kwa Pilato? Anadai eti Mungu amewafanyia watu wa jimbo lake matishio ya kigaidi na pia amesababisha vifo kibao kwa kuleta mafuriko na vimbunga vilivyofanya uharibifu mkubwa sana kwa watu wake. Kwa mantiki hiyo eti Mungu ni lazima atinge “Kisutu” ya pale Nebraska haraka iwezekanavyo.

Bwana mi naogopa kuendelea kuandika hii kitu, hebu endelea kusoma mwenyewe kwa kubofya hapa

Posted in Kimataifa, Photography, Siasa, Vijimambo | 2 Comments »

MISS NGWASUMA – MCHUJO

Posted by Bob Sankofa on September 19, 2007

 washindi.jpg

Basi mnamo majira ya kama saa saba usiku hivi ‘maji’ na ‘mafuta’ yakajitenga wazi. Mchujo ukaanza na hatimaye katika dada wale 24 waliokuwa wameingia kwenye nusu fainali hii 14 wakapigwa chini na kumi wakasonga fainali. Mshindi wa shindano hili litafanyika pale Diamond Jubilee tarehe 9/11/2007, blogu hii itakuwepo kuleta yanayojiri kama ilivyo kawaida. Mshindi katika fainali ataaga adha ya kubanana kwenye madaladala, atazawadiwa gari aina ya Mark II yeneye thamani ya shilingi za Kitanzania milioni kumi. Picha hii ni baadhi ya akinadada wakisikiliza kwa makini nani kapita na nani katupwa nje. Bahati nzuri wadada wote hawa katika picha hii wamekwenda fainali. Hongera.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

MALKIA WA NGWASUMA – ALONI ALONI

Posted by Bob Sankofa on September 19, 2007

img_2360.jpg

Baada ya ile ngwe ya pili bado mambo yakawa magumu kwa majaji kwa hiyo ikaamuliwa kuwa sasa washiriki wapande mmoja mmoja ili kama kuna mtu alikuwa anajificha nyuma ya wenzake atolewe “umaarufu” hapo hapo. Haikuchukua raundi, waliokuwa wakifanya kazi wakaonekana na wale wenzangu na mimi, ambao pumzi kidogo mgogoro, hawakuchelwa kuondoka jukwaani wakitweta. Uongozi wa blogu hii hauruhusu kuonyesha picha za kudhalilisha watu kwa hiyo hatutaweza kuweka picha za wale waliozingua. Huyu ni mmoja wa wale wadada waliofanya vizuri katika ngwe ya kucheza ‘alone’ kwa steji.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

MISS NGWASUMA – NGWE YA PILI

Posted by Bob Sankofa on September 18, 2007

img_2165.jpg

Baada ya majumuisho ya alama za ngwe ya kwanza ilikuwa dhahiri kuwa watu walikuwa wamebanana makoo kwa karibu mno. Uamuzi wa majaji ungeleta songombingo ukumbini, kwa hivyo ikaamuliwa kuwa mpambano upigwe tena. Wadada wakajimuvuzisha kwa steji bila hiyana na makamuzi yakaanza.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

MISS NGWASUMA – MAPUMZIKO

Posted by Bob Sankofa on September 18, 2007

img_2215.jpg

Baada ya ngwe ya kwanza kukamilika, wadada wakapatiwa dakika kadhaa za kupumua kidogo na majaji ilikuwa ndio muda muafaka wa kujumuisha alama walizopata washiriki katika ngwe hiyo ya kwanza. Katika muda huo, wazee wenyewe, Wazee wa Mujini, Wazee wa Ngwasuma, FM Academia, wakalivamia jukwaa na kuchakatua kwa kwenda mbele.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

MISS NGWASUMA – MAJAJI KAZI ILIKUWEPO

Posted by Bob Sankofa on September 18, 2007

img_2194.jpg

Nyoshi Al-Sadat, sauti ya simba, ndiye alikuwa akiongoza jopo la majaji. Pamoja na uzoefu wa siku nyingi wa kuimba na kulichakaza jukwaa aliokuwa nao Nyoshi, hakuweza kupepesa macho japo kidogo, aliogopa kupitwa, kila move ilikuwa na alama yake. Mchakato ulikuwa mkali sana kiasi kwamba ningekuwa mmoja wa majaji ningesema mabinti wote wameshinda.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Photography, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

MISS NGWASUMA – WACHA POROJO

Posted by Bob Sankofa on September 18, 2007

img_2255.jpg

Hapakuwa na muda wa kupiga blaablaa wala kutajataja majina. Punde si punde patashika nguo kuchanika likaanza. Wadada wakaanza kutoana jasho. Kama kuna mtu alikwenda kuloga basi ulozi haukuona ndani hapa, hapa ilikuwa ni pumzi yako tu. By the time muziki unakwisha hakuna aliyekuwa akihema, watu wote bado walikuwa fiti bovu.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

ILE NUSU FAINALI YA MISS NGWASUMA

Posted by Bob Sankofa on September 18, 2007

img_2259.jpg

Haya mambo yalijiri tarehe 7/9 pale Diamond Jubilee. Sikuwa na muda wa kutosha kuyapandisha mambo haya mapema kwani nilikuwa nakimbizana na safari na mikutano pia. Ngwe hii ilishirikisha kina dada 24 walioshiba kisawasawa. Hapa ndio walikuwa wamepanda jukwaani kwa utambulisho rasmi. Niliahidi kuurusha mchakato huu hapa bloguni, natimiza ahadi.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

HAPPY BIRTHDAY KITO!

Posted by Bob Sankofa on September 17, 2007

mama-kito.jpg

Katika kumbukumbu zote za siku ya kuzaliwa hakuna iliyo ya muhimu kama kumbukumbuku ya mwaka wako wa kwanza hapa duniani. Rafiki yangu Kito ametimiza mwaka mmoja na akanialika pale kwao, mkabala na kijiji cha makumbusho kwenda kushereheka nae. Hapa ni Kito (aliyebebwa), mama yake mzazi, Robi, na katuni, Willy the Pooh wakiwa wamepozi kwa ajili ya foto. Kito ni mtoto wa rafiki yangu Paul Ndunguru. Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »