MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

CHANGIA

 

Unayo kamera Digitali? Unayo simu ya kiganjani yenye Kamera? Unayo skana?

Kama una kimoja kati ya hivyo endelea kusoma hapa chini.

Blogu ya Mwenye Macho inakukaribisha kuwa mmoja wa wachangiaji wa blogu hii. Kauli mbiu ya Mwenye Macho ni “Yanayojiri Nilipo Nawe Upo”. Wadau wa blogu ya Mwenye Macho wanapenda kuwepo ulipo na washirikiane nawe kikamilifu katika yale yanayojiri hapo ulipo. Picha na habari zako zinaweza kuwa za matukio ya zamani au hivi karibuni au ya leo leo.

Unachotakiwa Kufanya:

1. Tumia kamera yako ya digitali au kamera ya simu ya kiganjani kupiga na kututumia picha ya mahali ulipo ukituonyesha yanayojiri.

2. Andika maelezo mafupi au ya kina (uamuzi ni wako) kuhusiana na picha unayotutumia, jina lako, na anuani yako ya barua pepe.

3. Tumia tarakilishi (Computer) au simu yako ya kiganjani kutuma picha yako na maelezo mafupi yanayoelezea tukio limejiri (limetokea) wapi kwa kutumia anuani ya barua pepe babukadja@hotmail.com

4. Mwisho, kwa kutumia kiboksi cha maoni hapo chini tuma ujumbe kwamba umeshatuma picha na habari yako ili iweze kupandishwa ukurasa wa mbele kwa haraka zaidi.

Baada ya muda mfupi habari yako itaonekana katika ukurasa huu tayari kwa wadau wengine kuitolea maoni.

Changia sasa kupitia babukadja@hotmail.com

Advertisements

4 Responses to “CHANGIA”

 1. […] CHANGIA […]

 2. simbadeo said

  Bob, hii poa sana. Ntakutumia picha mbili tatu ili wadau wajiri pale kamera yangu ilipojiri.

  Poa

 3. Caroline said

  greaaaaaaaaaaat stuff

 4. kennedy said

  Huwa ninatembelea blog za nyumbani kwa kupata yanyojiri pale,inafurahisha sana na inapendeza.Kwa mfano nimewaonyesha baadhi ya marafiki zangu hizo picha za Grafic wamependa sana kwa sababu hapa Sweden ni kosa la jinai,na mtuhumiwa hulazimishwa kulipa serikari . Kwa hiyo wameniomba ninaposhusha kikosi hapo bongo niwapatie nafasi ya wao kuchora pia.
  Vipo vingi ambaovyo ni vizuri katika blog yako na ile ya Michuzi,si kwamba nyingine hazina ila huwa ninatembelea hizo mara kwa mara.Mfano kuna mambo mengi ya kusoma kuhusu nchi za nje ,haswa huku ulaya.Mfano swala la kipindi cha winter time kama ulivyo andika kwenye moja ya picha.Kaskazin mwa scandinavia huwa miezi sita giza na miezi sita mwanga.Kwa hiyo ukiangalia nyumbani tunamatatizo ya uchumi lakini Mungu ametupendelea kimazingira.
  Sina mengi tutawasiliana zaidi,nimeweka email yako kwenye mawasiliano yangu,na nikiwa na cha kutuma nitatuma.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: