MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for the ‘Elimu’ Category

KILABU CHA USHAIRI CHAPATA UGENI

Posted by Bob Sankofa on March 5, 2008

img_0241_3_1.jpg
Jumanne ya mwisho ya mwezi wa uliopita kile kilabu chetu cha ushairi japa Bongo kilitembelewa na mwandishi mkubwa wa vitabu vya riwaya toka kule Afrika ya Kusini. Mwandishi huyu anakwenda kwa jina la Ms. Koenings. Wanachama walifurahia nafasi hiyo kwani waliweza kumuuliza mwandishi huyu maswali kadha wa kadha.
 img_0239_1_1.jpg
Koenings akisoma sehemu ya kitabu chake alichotoa hivi karibuni. Kitabu kinakwenda kwa jina la “The Blue Taxi”.
Picha kwa hisani ya kamera ya simu ya kiganjani ya Sandra Mushi.
Advertisements

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

HERI KWA MWAKA MPYA NA A NOVEL IDEA MPYA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

heri-ya-mwaka-mpya.jpg 

Washairi wakitakiana mwaka mpya wenye mafanikio kwa kilabu na wakitoa shukrani kwa duka la A Novel Idea kwa kuwapa sapoti ya kutosha kwa mwaka wa tatu sasa. Moja ya lengo ililojiwekea kilabu kwa mwaka huu ni kuhakikisha kinachapishwa kitabu cha ushairi kilichoandikwa na wanakilabu. Heri ya Mwaka mpya.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

PAUL MATATA SANA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

paul-na-mvinyo.jpg

Paul ana vituko sana, yani jamaa akiona bilauri lako limepungua kidogo tu ana wewe, saa nyingine anakucheki machoni halafu anajua unataka kuongeza mvinyo lakini unaona aibu hivi, basi anakuibukia fasta na chupa mkononi. Hapa ni baada ya Neema kuingia na kutekwa na majadiliano ya ushairi hadi kujisahau kujihudumia hivyo ikabidi Paul amkumbushe kuwa kuna mvinyo, kwa staili hii. Safi sana ukiwa na wenyeji wa hivi sio unakuwa kama kina sisi, tunakukaribisha one time ukijivunga sisi tunasonga.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

USHAIRI NA MVINYO NI CHANDA NA PETE

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

curthbet.jpg 

Mratibu msaidizi wa Kilabu cha ushairi na pia mtunzaji wa blogu ya kilabu, kaka Curthbet, akisoma shairi liloandikwa na dada Caroline. Ni shairi fupi lakini inabidi ulisome mara kadha kuweza kung’amua mwandishi alikuwa wakiwasilisha kitu gani, mvinyo unafungua ubongo wako kwa haraka ndio maana kaka alihakikisha hachezi nao mbali. Pale kushoto ni mchpishaji maarufu wa vitabu, mama Demere.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

SAMAHANINI NIMECHELEWA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

samahani-nimechelewa.jpg 

Mratibu mkuu wa kilabu cha washairi hapa Bongo, Neema Kambona, aliingia amechelewa kidogo, nafikiri ni sababu ya ile kitu inaitwa foleni za magari. Aliingia tayari shairi moja likiwa limeshasomwa. Aliomba radhi kwa kuchelewa kwake “kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake” 🙂 na pia tulimpatia nafasi ya kulisikia shairi lililompita tayari. Paul na Sarah, wamiliki wa maduka ya A Novel Idea, wakimsikiliza Neema akiomba msamaha.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

UNAPOZUNGUMZIA NAFASI YA KUTOSHA…

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

washairi-na-2008.jpg 

Duka hili la A Novel Idea ambalo limekuwa na msukumo mkubwa sana kuhakikisha kilabu cha washairi kinakuwa hapa nyumbani linavyoonekana kwa ndani. Huu ni upande mmoja tu wa duka sasa fanya ukubwa huu mara nne ndio upate duka zima. Cheki hawa jamaa walivyojiachia.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

WASHAIRI BONGO WAPATA MAKUTANO MAPYA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

a-novel-idea-mpya.jpg 

Hatimaye wanaklabu wa ushairi wa Bongo, Fanani Flavor Club, wamekutana kwa mara ya kwanza jana tangu mwaka huu uanze katika duka jipya la A Novel Idea lililofunguliwa pale Shopper’s Plaza. Zamani walikuwa wakikutana kule Sleep Way. Makutano haya ya sasa yana nafasi kubwa zaidi kwa washairi kukuruka wanavyoka na ni rahisi kufikika kwa watu wasio na usafiri binafsi. Shukrani kwa A Novel Idea.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

HAKUNA WAPI BILA GRAFITI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

grafiti_dec.jpg
Moja ya alama nyingine ya mafanikio ya WAPI ni katika suala zima la uendelezaji wa vipaji vya wasanii wa sanaa ya grafiti. Hivi ni vipaji vilivyokuwa vimejificha kule mitaani na walikuwa wakifanya kazi zao kwa kuchafua kuta za nyumba za watu kwa kificho hadi pale utamaduni wa WAPI ukishirikiana na British Council walipoamua kutoa nafasi ya bure kwa vijana kuifanya sanaa hii bila kificho katika kuta za BC. Mwezi huu grafiti ilikuwa ikizungumzia WAPI TWENDAKO.

Posted in Africa, Art, Blogu za Kiswahili, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kazi, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Siasa, Tanzania | Leave a Comment »

MPOTO TULIKUWA NAYE TENA

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

mpoto_des.jpg
Katika kufunga mwaka na utamaduni wa WAPI tulifanikiwa ‘kumtia nguvuni’ mshahiri matata hapa nyumbani, Mrisho Mpoto na tulifanikiwa pia ‘kumshurutisha’ atupe utenzi japo mmoja. Hakutukopesha akafanya mambo na akanyuka shairi lake lenye urefu wa kama dakika kumi na tano hivi, ile kumaliza tu watu wote vinywa wazi kwa jinsi jamaa alivyo na uwezo mkubwa wa kukariri mashairi yenye urefu wa kukatisha tamaa. Cheki jamaa alivyo na mzuka hadi kobadhi limemvuka.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

MAKTABA YA WATU

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

maktaba-ya-watu.jpg
Unaweza kupima vipi mafanikio ya WAPI katika mwaka 2007? Katika vitu ambavyo utamaduni wa WAPI imefanikiwa kuvianzisha katika miezi hii michache hapa nyumbani ni Maktaba ya Watu. Maktaba hii inaitwa Maktaba ya Watu kwa sababu inaundwa na watu ambao hubadilishana nakala zao za vitabu ili kujiongezea maarifa. Vingi ya vitabu vilivyopo katika Maktaba hii ya Watu ni vile ambavyo huwezi kuvipata tena katika maduka ya vitabu hapa Tanzania, mfano vitabu vya kina Shaaban Robert, Mwalimu Nyerere, maarifa ya kina Asante Kelefi na Cheikh Anti Diop. Unacho kitabu au maarifa fulani nyumbani kwako ambayo ungependa yawafikie watu wengine? Njoo navyo katika Maktaba ya Watu

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

FUNGA MWAKA YA UTAMADUNI WA WAPI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

funga-mwaka-ya-wapi.jpg

Hatimaye Jumamosi ya wiki iliyopita, wakazi wa Dar ambao pia ni wadau wa utamaduni wa WAPI walijitokeza kwa mara nyingine tena pale British Council ili kuufunga mwaka kwa utamaduni huu unaoota mizizi kwa haraka hapa nyumbani, Tanzania. WAPI ni uwanja wetu wa kujieleza na kusikiliza wenzako wanasema nini, lakini zaidi ya yote ni uwanja wa wewe kusikilizwa kuwa una nini cha kusema. Kauli mbiu ya WAPI hii ya mwisho wa mwaka ilikuwa ni “WAPI TWENDAKO?”

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

WE UNAONAJE?

Posted by Bob Sankofa on December 16, 2007

dscf0234.jpg

Kuna watu wanamaindi kishenzi wakiona makinda wametinga vijoho namna hii, wanasema wanawafunika jamaa wa vyuo vikuu bila sababu za msingi. Kuna wengine wanaona ‘mzuka’ tu kwani wanadai hivi vijoho huwaongezea makinda hawa munkari wa kupiga buku hadi huko juu kabisa ili wawe wakivaa vijoho (huko mbele yanakuwa majoho au sio?) kila baada ya mafanikio fulani. We una mtazamo gani?

Kamependeza lakini eeeh? Cheki kanavyojiamini.

Picha kwa msaada mkubwa wa kaka Simbadeo.

Posted in Africa, Bongo, Elimu, Fotografia, Photography, Tanzania, Vijimambo, Wadau | Leave a Comment »

UNAMKUMBUKA ASHA?

Posted by Bob Sankofa on December 14, 2007

wamkumbuka-asha.jpg

Asha Mtwangi. Ushawahi kulisikia hilo jina? Wapi? Unamfahamu Asha? Unamfahamu kama nani? Ulimsikia kwa mara ya kwanza wapi? Unajua anapendelea nini baada ya kazi? Anasoma vitabu vya aina gani na anasikiliza muziki upi? Chakula akipendacho je? Tafadhali kuwa wa kwanza kutujibia maswali haya na hiyo ndio itakuwa moja ya zawadi yako kwetu kwa sikukuu ya Noeli na ile ya Mwaka Mpya 🙂

Posted in Africa, Art, Bongo, Elimu, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi, Wadau | 6 Comments »

IRENE SANGA NA ONYESHO LA “UTANDAWAZI”

Posted by Bob Sankofa on December 4, 2007

utandawazi-poster.jpg

Irene Sanga, mtunzi na mghani mashairi ya Kiswahili baada ya kutamba sana na mashairi yake ya SALAMU KWA MJOMBA na PANGISHENI katika radio na televisheni za Afrika ya Mashariki sasa anatukaribisha kwenye onesho lake la jukwaani litakalofanyika pale kituo cha utamaduni wa watu wa Ufaransa, ufuatao ndio mwaliko rasmi;

UNAKARIBISHWA KWENYE ONESHO LA IRENE SANGA LA “UTANDAWAZI”

MAHALI: ALLIANCE FRACAISE

SIKU: IJUMAA, 7/12/2007

MUDA: SAA 8.30 – 11.30 USIKU

KIINGILIO: BURE

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kazi, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 3 Comments »

BALOZI KILABUNI

Posted by Bob Sankofa on December 1, 2007

balozi_poetry.jpg

Mkutano wa washairi wa Bongo (Wanafanani) ulibahatika kutembelewa na Mh. Balozi wa Palestina nchini Tanzania (katikati). Balozi huyu nimekuwa nikigongana naye sehemu kadhaa zenye matukio ya burudani yenye nia ya kusaidia jamii. Balozi na yeye ni mshahiri, mashaihiri yake ni ya kimapinduzi zaidi ya kiu kingine chochote, nafikiri sababu ya historia pia. Balozi meahidi udhamini wa hali na mali kwa kilabu cha Wanafanani.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kimataifa, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

WASHAIRI WAKUTANA TENA NOVEMBER

Posted by Bob Sankofa on December 1, 2007

wanafanani_nov.jpg

Utamaduni wa ushairi unazidi kukua taratibu, kila mwezi kilabu cha ushairi kinazidi kupata wajumbe wapya wawili au watatu. Kilabu hiki chenye umri wa miaka miwili kinajivunia mno washairi wake ilionao ambao wanajitolea kwa moyo wote kuhakikisha sanaa ya ushairi haibaki pweke. Kumbuka wajumbe na viongozi wa kilabu hiki wamefanikiwa kwa miaka miwili kuikuza kilabu bila malipo yeyote, ni Watanzania wachache sana waliobaki na moyo huu. Hongera Wanafanani (washairi) kwa kukutana tena. Maudhui ya mwezi Novemba yalikuwa ni “Growth”

Pia kuna habari njema, mwaka 2008, Januari ni mwaka mpya na kila kitu kinakuwa kipya. Kilabu kinaamia kwenye ukumbi mkubwa zaidi wa duka la vitabu la A Novel Idea pale Shoppers Plaza. Karibuni nyote, mwambie na rafiki.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 3 Comments »

USIKU MWINGINE WA USHAIRI

Posted by Bob Sankofa on November 23, 2007

poetry.pngDear Lovers, (of poetry I mean! what did you think?)

Poetry nite is here once more. We meet on Tuesday 27th NOVEMBER 2007, from 19H00 at A Novel Idea Slipway. Theme for the nite is “GROWTH”.

Swahili poems are strongly encouraged, or a poem in any language for that matter. We shall listen as you read, and probably ask for a translation.

We love to sit on the floor, so please bring a mat or cushion along, plus that friend who could get inspired somehow.

COME TO POETRY NITE
“Come one, come all,
Come read, or discuss,
the magical bliss,
of poetry’s kiss…

Come grab and munch,
Sip on wine or punch,
while we sit in a bunch,
on a big round couch…

All faces are happy,
broad and shiny,
lovely and ready,
To knock down poetry…

all the same thou,
if I were you Lou?,
Or Lisa Patlou?,
I wouldnt miss out,
on poetry nite…”

by Clara Swai
@2007

* Reminding each member to contribute TShs. 3,500/= for refreshments and drinks.
* Also visit our blog at http://fananiflava.blogspot.com for more insight into what we are all about.
* Mucho gracias to “A Novel Idea” staff and management, for sharing their space and time with us all. We
continue to enjoy the 10% discount on any book purchase

Asanteni,

Clara

co co coordinator

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

WAFIA DINI

Posted by Bob Sankofa on November 19, 2007

kanisa-la-wafia-dini.jpg 

Hili ni kanisa la Wafia Dini wa Uganda, liko Kampala. Kanisa hili limejengwa kuwakumbuka watu 22 ambao walitiwa kiberiti wakiwa hai na Kabaka kwa kosa la kumpokea Yesu kama Mfalme wao wa Mbinguni na kuuasi utwala wa Kabaka. Wakristo huja kuhiji hapa wakitembea kwa mguu toka Nairobi na hata Afrika ya Kati. Mambo ya dini tuyaache kama yalivyo.

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Kimataifa, Photography, Safari | Leave a Comment »

HEKALU LA BAHAI

Posted by Bob Sankofa on November 19, 2007

hekalu-la-bahai2.jpg

Dini kubwa kabisa katika Uganda ni ile ya Wakristo, lakini nchi inatoa fursa ya kuamini na kuabudu dini yeyote uipendayo ilhali huvunji sheria za nchi zilizowekwa. Basi hapa kuna hekalu kubwa kabisa katika Afrika la dini ya watu wa Bahai. Sikuruhusiwa kupiga picha ndani ya hekalu. Hekalu hili ni kivutio kikubwa sana hapa Uganda.

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Kimataifa, Photography, Safari | Leave a Comment »

IKULU YA KABAKA

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

kabaka-nje.jpg 

Naelekekea Jinja lakini mwenyeji wangu ananiambia haitakuwa vyema kwenda huko kwanza kabla ya kupita kwenye himaya ya Kabaka ama Mfalme Mutesa na nduguze na kutoa salamu pale. Basi tunaingia hapa kupata historia ya siasa za Uganda kabla na baada ya ujio wa watu weupe katika nchi hii nzuri.

kabaka-ndani.jpg

Hapa ni ndani ya Ikulu ya himaya ya Kabaka. Tunaambiwa Kabaka Mutesa alikuwa na wake 85 tu. Jamaa aliruhusiwa kuoa katika koo zote kasoro ile aliyokuwa akitoka mama yake mzazi. Lakini kuna kitu kinanishtua, Wafalme karibu wote wa himaya hii ya Buganda walikuwa wakifariki vijana wadogo kabisa, hakuna aliyezidi miaka 55. Hapakuwa na Ukimwi kipindi hicho kwa hiyo mimi nahitimisha kwa kusema labda vifo vile vilisababishwa na kufanya ngono sana na hivyo kupoteza nguvu nyingi mwilini, totoz 85 si mchezo ati.

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari, Siasa, Tanzania | 1 Comment »

WARSHA YA WASANII WA GRAFITI – ZAWADI YA KOOR

Posted by Bob Sankofa on November 9, 2007

koor2.jpg

Huyu ndiye mkufunzi wa warsha ya sanaa ya grafiti iliyodumu kwa siku tatu hapa Dar es Salaam, Kool Koor. Jamaa hafundishi kwa maneno matupu, ni mtu wa vitendo hasa. Ukifika pale kwenye lango la mbele kabisa la British Council, utaona kazi hii aliyoifanya huyu jamaa. Ni kazi matata kwelikweli, hii ni zawadi yake kwa wasanii wenzake wa hapa Tanzania. Tembelea pale uone mwenyewe. Koor anaondoka leo usiku kurudi zake nyumbani, anasema atarejea tena mwezi Desemba kwa Warsha matata zaidi.

Posted in Africa, Art, Bongo, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

WARSHA YA WASANII WA GRAFITI – WASANII KAZINI

Posted by Bob Sankofa on November 9, 2007

wasanii-kazini.jpg

Wasanii waliohudhuria warsha ya siku tatu ya sanaa ya grafiti wakiwa katika suala zima la harakati la ‘kuchafua’ ukuta wa British Council. Asante British Council kwa kuruhusu vijana kufanya mambo uani kwenu. Uzuri wa warsha hii ni kuwa huwezi kutoka kitambi kwani ni tofauti sana na zile tulizozoea za kulala kwenye viti huku mtu fulani akitoa hotuba ndeeeefu, na pengine kunywa chai ya maziwa na sambusa kila baada ya masaa mawili na mwisho wa siku hakuna kinachofanyika. Hapa ni kazi kazi tu, jua lote la Dar linakuishia mwilini lakini mwisho wa siku kuna kitu unaweza onyesha kwa uliowaahidi. Big-up wasanii wa grafiti, kazi nzuri.

Posted in Africa, Art, Bongo, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Photography, Sanaa | 2 Comments »

WARSHA YA WASANII WA GRAFITI YAFIKA TAMATI

Posted by Bob Sankofa on November 9, 2007

warsha-imekwisha.jpg

Hawa ni baadhi ya wasanii waliohudhuria warsha ya siku tatu ya sanaa ya grafiti. Warsha hii ilikuwa ikiendeshwa na mkufunzi toka Marekani, Kool Koor (mwenye kofia na fulana ya rangi ya udongo). Kwa upande wa kushoto unaweza kuniona nikitoa tabasamu utafikiri na mimi nilikuwa mmoja wa wasanii wale kumbe wapi blablah tu, mi nilikuwepo kuwasaidia kuweka kumbukumbu tu ya warsha yao. Kool Koor anarudi tena mwezi Desemba kwa Warsha nyingine. Kaa tayari.

Posted in Africa, Art, Bongo, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

ASANTE DADA RAHEL – WASANII WA MACHATA

Posted by Bob Sankofa on November 7, 2007

dada-rahel.jpg

Huyu ndie dada Rahel ambaye amejitolea ukuta wa nyumba yake (gereji anakopaki gari) ili wasanii waweze kufanya warsha yao kwa siku ya leo, hapa likuwa anafurahia kazi nzuri iliyofnywa na wasanii, kaka Mejah anamaliziamalizia mchoro.

Dada Rahel anamiliki duka la sanaa (gallery) inayokwenda kwa jina la Mawazo, iko pale YMCA. Tafadhali mtembelee na uwaunge mkono wasanii ambao dada anawasaidia kuwauzia kazi zao. Acha kununua picha za wanasesere toka China kanunue picha za wasanii wa Kitanzania pale. Kwa niaba ya wasanii wa machata (grafiti), http://www.mwenyemacho.com inapenda kutoa shukrani za pekee kwa dada, ASANTE SANA.

Kesho warsha inaendelea pale British Council kuanzia saa tatu asubuhi, Karibu.

Posted in Africa, Art, Bongo, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania | 2 Comments »

WARSHA YA WASANII WA MACHATA (GRAFITI)

Posted by Bob Sankofa on November 7, 2007

almost-done.jpg

Wasanii wa fani ya machata (grafiti) wakiwa kazini baada ya kupata maelekezo toka kwa mkufunzi wao, Koor, ambaye leo amewafundisha namna ya kukamata vyema makopo ya rangi pamoja na uchanganyaji bora wa rangi katika kazi zao. Mejah, mwezeshaji wa warsa hii aliniambia kuwa aliwapigia simu wasanii lukuki ili waje kweye warsha hii wakaitikia wito vinywani lakini wameshindwa kutimiza ahadi zao za kutokea hapa. Mejaha anawaambia wasanii wenzake waliofika hapa, “Wameitwa wengi, mmekuja wachache na nyie ndio mliochaguliwa, tupige kazi”. Leo walikuwa nyumbani kwa dada Rahel, ambaye alijitolea ukuta wa nyumbani kwake bure ili vijana wajimwage.

Posted in Africa, Art, Bongo, Elimu, Fotografia, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

KARIBU KWENYE WARSHA YA WASANII WA MACHATA (GRAFITI)

Posted by Bob Sankofa on November 7, 2007

koor.jpg

Jijini Dar sanaa ya kuchora kuta (grafiti) kwa rangi za kupuliza (spray cans) imeshika moto kwelikweli. Wasanii wa fani hii walianza kwa kujichorea tu katika kuta chafuchafu kule mitaani halafu baadae British Council kwa kupitia mradi wa WAPI, ambao huwa nauzungumzia kila mwezi, wakaamua kufadhili sanaa ile ili watu waifanye kwa ufanisi zaidi.

Sasa kuna mradi mwingine unaoitwa UMMA PROJECT, mradi ule unasimamiwa na mtu anaitwa Mejah (ni huyo mwenye kilemba cha Kirasta kichwani). Mradi wa Umma umefanikiwa kuwakutanisha wasanii wa bongo na msanii maarufu kabisa wa fani hii toka Marekani, Kool Koor (huyo mwenye fulana ya njano). Koor ni msanii wa kulipwa wa fani ya Grafiti na pia ni mtayarishaji wa muziki toka Marekani lakini kwa sasa anafanyia kazi zake Ubelgiji.

Koor yuko Tanzania kwa siku tatu na anaendesha warsha ya kufundisha mbinu za kutengeneza sanaa bora zaidi za Grafiti. Warsha ile itadumu hadi siku ya Alhamisi. Leo Koor ameendesha warsha hii nyumbani kwa dada Rahel ambaye amejitolea ukuta wa nyumbani kwake ili upigwe chata. Kesho Koor na wasanii wa kibongo wanahamishi warsha pale British Council na keshokutwa watakuwa pale pia. Iwapo wewe ni msanii na ungependa kushiriki, karibu, ni bure kabisa na jamaa ni msanii mkali sana. Utapata elimu babkubwa. Leo amefundisha namna ya kushika makopo ili kuoata mistari yenye unene tofauti na namna ya kuchanganya rangi tofauti kwenye mchoro mmoja.

Posted in Africa, Art, Bongo, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

TANGAZO, TANGAZO, TANGAZO

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

vicensia-shule.jpgSankofa,

kuna mdau anatafuta makala, magazeti/majarida yenye habari za Lance Spearman ambaye alikuwa muhusika wa makala/tamthiliya za picha (photo novel/photo play/photo comic) zilizochapishwa kati ya miaka ya 1960 na 1970 na kampuni ya ucapishaji magazeti ya Afrika Kusini “Drum Publications Ltd”.

Mhusika alikuwa anajulikana kama “The Spear” au “Spia”. Pia kwa Afrika Mashariki kuna magazeti yaliyochapishwa Kenya yanayoitwa “Film” au “African Film” yaliyokuwa na mhusika huyu kama hilo analosoma mdau pichani.
Pia kuna wahusika wengine kama “Fearless Fang”, an African “Tarzan” na wengineo pia kama kuna mtu mwenye kumbukumbu zozote hizo pia zinahitajika. Mdau yuko tayari kununua nakala hizo zilizotumika kwa ajili ya kuweka kumbukumbu katika maktaba.

Kulingana na ubora na idadi mdau yuko tayari kulipa Euro 5 mpaka 20 Kwa watu wanaofahamu jarida/gazeti linaloitwa “Film Tanzania” na kama kuna mtu analijua na anafahamu namna ya upatikanaji wake mdau anaomba amfahamishe kupitia vicensiashule@hotmail.com

shukran kibao!

Picha na Issa Michuzi

Posted in Africa, Art, Biashara, Bongo, Burudani, Elimu, Filamu, Fotografia, Kimataifa, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MIAKA MIWILI YA KILABU CA USHAIRI BONGO – TUNAMALIZA KAMA TUNAANZA

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

ufungaji.jpg

Basi ilipotimu usiku wa manane siku ile ya Jumamosi tukawa tunaelekea ukingoni mwa shughuli ile nzito. Jamaa wa Simba Theatre hawakuwa na hiyana kutusindikiza majumbani mwetu kama walivyotukaribisha, wakanyuka mdundiko. Watu kuja kustuka wamefika majumbani kwao kwa mguu angali magari yao wameyaacha Alliance Fracaise. Mdundiko una nguvu ya ajabu sana ndio maana ukipita mitaani watoto huwa wanapotea sana. Nimetia chumvi kidogo hapo 🙂 . Hadi wakati mwinginge.

UHURU!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MIAKA MIWILI YA KILABU CHA USHAIRI BONGO – BAADA YA USHAIRI…

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

tatu-and-the-band.jpg

Nimewahi kusema mara nyingi hapa bloguni kwamba uzuri wa kilabu cha ushairi bongo ni kwamba huwa kuna zaidi ya ushairi. Dada Tatu alikuwepo, yeye si mshairi kwa sana, yeye ni mwanamuziki zaidi anapiga gitaa kavu. Dada Tatu alijumuika jukwaani na wanajumuiya wengine, Caroline, Asha, na Clara na wakatupa wahudhuriaji wengine vibao motomoto vya kuifagilia kilabu. Una kipaji ambacho kinaendana na ushairi kidogo, njoo tujumuike tafadhali.

msosi.jpg

Nikisema kilabu kina zaidi ya ushairi sitanii, kulikuwa na wakati wa kutosha pia kwa watu kujinafasi kwa maji ya madafu, mvinyo na mishkaki ya samaki, kwa wala majani (vejetarianz) kama sisi tulitafuna karoti na matango kama sungura. Nafikiri mkutano ujao utakuwa wa kuotea mbali. Big up Fanani Flava.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MIAKA MIWILI YA KILABU CHA USHAIRI BONGO – WAUNGA MKONO

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

waunga-mkono.jpg

Huyo mzungu wa kiume ni Paul na huyo wa kike ni Sarah. Hawa jamaa wanaiunga sana mkono jamii ya ushairi ya Bongo. Jamaa wametoa duka lao la vitabu la A Novel Idea liwe sehemu ya kilabu kukutania kila Jumanne ya mwisho ya mwezi, bure kabisa. Pia kila mwanajumuiya ya ushairi akienda kununua kitabu pale anapata punguzo la 10% ya bei ya kitabu chochote atakachonunua. Jamaa wanafungua duka kubwa zaidi pale Shoppers Plaza ili jumuiya iwe na ukimbi mkubwa zaidi, tunahamia kule muda si mrefu. Karibu!

Posted in Africa, Art, Biashara, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »