MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

RIHANNA ATOLEWA RESI HARUSINI, HANA ADABU

Posted by Bob Sankofa on November 1, 2007

rihanna-2.jpgDuh! Umaarufu ukipanda kichwani saa nyingine husababisha msiba. Rihanna kahudhuria harusi ya binamu yake huko kwao, visiwa vya Barbados, ila kwa ripoti zilizoenea katika mtandao ni kwamba alitolewa baruti kama mbwa mwizi sababu ya ushenzi wake. Kwa habari zilizoko katika tovuti ya www.mediatakeout.com ni kwamba songombingo hilo lilianza mapema kabisa mara tu baada ya Rihanna kutia timu harusini hapo. Mmoja wa waalikwa alisema, “Nilishtushwa mno nilipoona kivazi alichokuwa ametinga binti. Kila alipokuwa akipiga hatua, matiti yake yalikuwa kama vile yatatoka nje ya nguo muda wowote.” Habari zinasema kuwa familia ya maharusi ni ya Kikristo usipime, kwa mantiki hiyo Rihanna alimtia ‘kichefuchefu’ karibu kila mgeni mualikwa aliyefika kwenye harusi ile.

Songombingo hili haliishi hapo. Kwa habari za waliokuwepo kwenye sakata hilo inasemekana kuwa Rihanna aligoma kabisa kula chakula ambacho walikuwa wametayarishiwa wageni waalikwa akiwemo yeye. Inasemekana alikuwa ametinga harusini hapo na msosi wake, kwani msosi wa pale harusini aliuona kuwa si wa mtu wa hadhi yake. Soo!

Wakati yote hayo yakiendelea, ikafika wakati wahusika wa harusi wakaona imetosha sasa. Mmoja wa wanafamilia anasema, “Rihanna alikkuwa amekuja kuharibu siku ya maharusi wetu kwa hivyo tukaona ni busara iwapo ataondoka zake na kutuacha sie na ushamba wetu na chakula chetu chenye kipindupindu. Alituelewa na kukubaliana na uamuzi wetu”rihanna-1.jpg

Lakini kabla hajatoweka zake, mgeni mwingine anasema kuwa Rihhana hakuondoka bure, aliipa familia ‘vipande’ vyao vya kutosha tu. “Alizozana kwa muda na shangazi yake pamoja na mama yake… walikuwa mbali kidogo na ukumbi wa sherehe lakini tulikuwa tukisikia sakata lote. Rihanna alikuwa akimbwatukia mama yake mzazi.” Alisema mgeni huyo. Mgeni mwingine alisema, “Mama yake huyu binti ni mtu wa kawaida sana na hana makuu, mama yule alikuwa kimya muda wote akingoja binti yake amalize kutoa dukuduku lake… angekuwa ni binti yangu, mama yangu mzazi ningemchuna ngozi angali anapumua, na ingebidi niitiwe polisi, shenzi kabisa!”

Duh! Rihanna unaharibu mtu wangu. Mdau unaonaje hii, je unadhani tunao masupastaa dizaini hizi hapa bongo?

Advertisements

6 Responses to “RIHANNA ATOLEWA RESI HARUSINI, HANA ADABU”

 1. Ebwanaee! Hii noma sana mkuu.Duh na hicho kivazi si utani Maana……

 2. Egidio we acha tu!

 3. zuhmas said

  Mhh!! hiyo ni noma mana huyo alihudhuria kwa minajili ya kuamsha hisia za bwana harusi kabla hata hawajaianza fungate yao!!!!
  Jamani kweli misifa ni noma

 4. j kibaza said

  mambo makubwa hayo

 5. hyvone macha said

  mhm matata kwelikweli hiyo nguo cjajua dhumuni nini

 6. boobs admire said

  mmh, asante binti .. naona ulikuwa unataka kumchanganya bwana harusi..titi la kuua mtu aisee huyu binti usipime.. hapa hata kama mm ningekuwa bwana harusi au ndugu yake ninge mkimbiza hii noma.. kweli masifa NOME SOMETIME.. B.A..CA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: