MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for December, 2007

HUYU NI NANI TENA? ALIKUWEPO PIA

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

mtumbuizaji-wa-mwezi.jpg

Ni mdogo wa aliyewahi kuwa mmoja wa warembo waliofanikiwa sana Tanzania, amewahi kuingia katika shindano la wanamuziki Afrika Mashariki na akafika mbali, sasa ana nyimbo kadhaa zinawika radioni hapa nyumbani. Namzungumzia dada mwenye nguo ya kata mikono hapo, je unamfahamu? Pembeni yake ni mshikaji anaitwa Gaid, mwanaharakati wa fikra za mtu mweusi, anatoka kule kwa Joji Kichaka na yuko Bongo kwa mishemishe fulani hivi. Sina hakika kama anajua maana ya neno lililoko kwenye fulana yake, atakua anajua mbona anatabasamu?

mtumbuizaji-wa-mwezi2.jpg

Nilisahau kusema hapo juu kuwa dada alikuwa ndiye mtumbuizaji wetu mkuu wa mwezi huu. Hapa alikuwa anaimba ule wimbo maarufu wa Bob Marley, “Nyimbo za Ukombozi” au “Redemption Songs” kwa lugha ya kikoloni.

Advertisements

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | 2 Comments »

HAKUNA WAPI BILA GRAFITI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

grafiti_dec.jpg
Moja ya alama nyingine ya mafanikio ya WAPI ni katika suala zima la uendelezaji wa vipaji vya wasanii wa sanaa ya grafiti. Hivi ni vipaji vilivyokuwa vimejificha kule mitaani na walikuwa wakifanya kazi zao kwa kuchafua kuta za nyumba za watu kwa kificho hadi pale utamaduni wa WAPI ukishirikiana na British Council walipoamua kutoa nafasi ya bure kwa vijana kuifanya sanaa hii bila kificho katika kuta za BC. Mwezi huu grafiti ilikuwa ikizungumzia WAPI TWENDAKO.

Posted in Africa, Art, Blogu za Kiswahili, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kazi, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Siasa, Tanzania | Leave a Comment »

MANYANI NANI NAO NDANI!

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

manyani-nani_des.jpg

Wadau wa WAPI waliona haitakuwa vyema iwapo mwaka wa shughuliza za WAPI utafungwa bila kuwaalika Manyani Nani Band ‘ku fasi ya steji’ (nimeongea Kicongo hapo). Jamaa nao hawakulaza damu, wakalisakanyua jukwaa vilivyo. Unamuona Fujo anavyoiadhibu hiyo ngoma, Paul na gitaa lake kama kawa, Hussein ‘ku fasi ya drums’. Hapakukalika.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Tanzania | 1 Comment »

KIVAZI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

kivazi.jpg
Vijana wa Zawose ni matata sana. Cheki hawa jamaa vivazi vyao. Hivi vivazi ni zaidi ya vivazi, ni vyombo vya muziki pia. Jamaa wakiruka juu na kurudi chini vivazi hivi vinatoa mlio fulani murua sana, lakini inabidi uwe na sikio la kimuziki kuweza kutumia ala hii la sivyo ukipewa kama huna hicho kipaji utaishia kuharibu muziki mzima kwa kukosa kitu wataalamu wanaita ‘tempo’ au mwendokasi wa muziki.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Mikutano, mitindo, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

DAKTA ZAWOSE BADO ANAISHI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

familia-ya-zawose.jpg

Kila utamaduni wa WAPI unapojiri familia ya marehemu mzee wetu, Dakta Hukwe Zawose huwa wanajumuika na wana-WAPI na kutoa burudani ya asili. Hii ni namna bora kabisa ya kutunza kazi na historia ya mzee hasa ukizingatia Watanzania wengi hatuna utamaduni wa kusoma vitabu, basi hii ni namna rahisi ya kumfahamu Dakta Zawose na kazi zake kupitia uzao wake. Hawa ni watoto na wajukuu wake. Zawose bado anaishi.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MPOTO TULIKUWA NAYE TENA

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

mpoto_des.jpg
Katika kufunga mwaka na utamaduni wa WAPI tulifanikiwa ‘kumtia nguvuni’ mshahiri matata hapa nyumbani, Mrisho Mpoto na tulifanikiwa pia ‘kumshurutisha’ atupe utenzi japo mmoja. Hakutukopesha akafanya mambo na akanyuka shairi lake lenye urefu wa kama dakika kumi na tano hivi, ile kumaliza tu watu wote vinywa wazi kwa jinsi jamaa alivyo na uwezo mkubwa wa kukariri mashairi yenye urefu wa kukatisha tamaa. Cheki jamaa alivyo na mzuka hadi kobadhi limemvuka.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

MAKTABA YA WATU

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

maktaba-ya-watu.jpg
Unaweza kupima vipi mafanikio ya WAPI katika mwaka 2007? Katika vitu ambavyo utamaduni wa WAPI imefanikiwa kuvianzisha katika miezi hii michache hapa nyumbani ni Maktaba ya Watu. Maktaba hii inaitwa Maktaba ya Watu kwa sababu inaundwa na watu ambao hubadilishana nakala zao za vitabu ili kujiongezea maarifa. Vingi ya vitabu vilivyopo katika Maktaba hii ya Watu ni vile ambavyo huwezi kuvipata tena katika maduka ya vitabu hapa Tanzania, mfano vitabu vya kina Shaaban Robert, Mwalimu Nyerere, maarifa ya kina Asante Kelefi na Cheikh Anti Diop. Unacho kitabu au maarifa fulani nyumbani kwako ambayo ungependa yawafikie watu wengine? Njoo navyo katika Maktaba ya Watu

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

FUNGA MWAKA YA UTAMADUNI WA WAPI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

funga-mwaka-ya-wapi.jpg

Hatimaye Jumamosi ya wiki iliyopita, wakazi wa Dar ambao pia ni wadau wa utamaduni wa WAPI walijitokeza kwa mara nyingine tena pale British Council ili kuufunga mwaka kwa utamaduni huu unaoota mizizi kwa haraka hapa nyumbani, Tanzania. WAPI ni uwanja wetu wa kujieleza na kusikiliza wenzako wanasema nini, lakini zaidi ya yote ni uwanja wa wewe kusikilizwa kuwa una nini cha kusema. Kauli mbiu ya WAPI hii ya mwisho wa mwaka ilikuwa ni “WAPI TWENDAKO?”

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

PILAU LA EID

Posted by Bob Sankofa on December 21, 2007

pilau-idd.jpg

Cheki watu walivyofanyiza huko mitaa ya kati katika suala zima la kufagilia Eid. Ni mwendo wa Pilau na ngamia tu, hii inaitwa kula hadi ujipake.

Posted in Fotografia, Kimataifa, Photography, Sherehe, Vijimambo | 7 Comments »

HERI YA EID

Posted by Bob Sankofa on December 20, 2007

eid-004.jpg

Raha ya Eid huku nyumbani, Tanzania, ni kutembeleana wakati wa sherehe fulani. Leo asubuhi na mapema nimeamshwa na mirindimo ya madufu na sauti safi za kaswida toka kwa vijana wa msikiti wa Tambaza, ambao wanatembea siku nzima ya leo kumwaga baraka katika nyumba za watu wa hapa. Kila nyumba wanaimba na kupiga dufu kwa kama dakika moja na sekunde kadhaa hivi halafu wanahamia nyumba nyingine. Hii ni zawadi safi sana toka kwa ndugu zetu Waislamu kwenda kwa Waislamu wenzao na hata wale wasio Waislamu, kama mie.

Posted in Africa, Bongo, Burudani, Fotografia, Photography, Sherehe, Tanzania | 3 Comments »

MWANZA KUNANI?

Posted by Bob Sankofa on December 18, 2007

nuru_mwanza.jpg

Mdau Nuru katutumia hii. Nuru anauliza ukisikia Mwanza ni picha gani inakujaa akilini kwa ghafla bin vuu? Bila shaka utasema Sangara. Nuru anakubaliana na hilo ila picha yake inakwenda mbali zaidi kwa kuonyesha kuwa Mwanza ni pamoja na mitaa iliyopangwa ikapangika na barabara zenye staha pia. Picha hii amepiga Jumapili asubuhi mchana, jiji limetulia na hii ni barabara ya kuelekea Mwanza hoteli.

Posted in Africa, Fotografia, Photography, Tanzania, Teknolojia, Wadau | 3 Comments »

BABA WA BLOGU ZA KISWAHILI AIBUKIA DAKAR

Posted by Bob Sankofa on December 16, 2007

ndesanjo-dakar.jpg

Yamesemwa mengi kuhusu muasisi wa blogu za Kiswahili, Ndesanjo Macha. Wapo waliosema kwa kuwa hakuna malipo ya fedha katika kublogu, jamaa amekata tamaa na kazi ya kujitolea na hivyo amaecha kublogu bila kuaga. Wapo waliosema anapumzika, japo yeye mwenyewe alishasema kuwa mapumziko yamekwisha. Wapo waliosema amepata kimwana mpya Afrika ya Kusini na amembana kwelikweli kiasi kwamba hata kublogu hawezi tena. Halafu ghafla! Jamaa anaibukia Dakar. Anasambaza “injili”. Ni kweli Ndesanjo amekuwa “mwinjilisti”? Bonyeza hapa kupata jibu

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Tanzania, Teknolojia, Wadau | 1 Comment »

WE UNAONAJE?

Posted by Bob Sankofa on December 16, 2007

dscf0234.jpg

Kuna watu wanamaindi kishenzi wakiona makinda wametinga vijoho namna hii, wanasema wanawafunika jamaa wa vyuo vikuu bila sababu za msingi. Kuna wengine wanaona ‘mzuka’ tu kwani wanadai hivi vijoho huwaongezea makinda hawa munkari wa kupiga buku hadi huko juu kabisa ili wawe wakivaa vijoho (huko mbele yanakuwa majoho au sio?) kila baada ya mafanikio fulani. We una mtazamo gani?

Kamependeza lakini eeeh? Cheki kanavyojiamini.

Picha kwa msaada mkubwa wa kaka Simbadeo.

Posted in Africa, Bongo, Elimu, Fotografia, Photography, Tanzania, Vijimambo, Wadau | Leave a Comment »

UMUHIMU WA BUSTANI JIJINI

Posted by Bob Sankofa on December 14, 2007

 

bustani-posta-ya-zamani.jpg

Kaka Simbadeo katutumia hii jioni hii. Hapa ni bustani ya Posta ya Zamani ambako ni kimbilio kubwa kwa waenda kwa miguu wengi wa Jijini Dar. Bongo sasa hivi kuna jua balaa, basi watu wakizunguka huku na huko wanakuja kupiga kambi hapa kwa dakika kama kumi na tano kabla ya kuendelea na mishemishe zao.

Hao kina dada unaweza kusema wanataka kuvuka barabara lakini kumbe wameshasimama hapo dakika karibu ya ishirini sasa kuikimbia adhabu ya jua. Hiyo ni moja ya pozi nyingi ya kukaa hapo bustanini. Pozi nyingine ni ile ya kujifanya wewe na mshikaji wako mnasalimiana, yani kama vile hamjaonana siku nyingi. Maana ukikaa kama wale jamaa pale kushoto watu wanaweza wakakuhukumu fasta kwamba wewe ni JOBLESS (Huna kazi) kumbe maskini ya Mungu unakimbia jua tu.

Serikali ifufue zile bustani zingine. Asante Simbadeo kwa foto

Posted in Africa, Bongo, Fotografia, Photography, Tanzania, Vijimambo, Wadau | 1 Comment »

UNAMKUMBUKA ASHA?

Posted by Bob Sankofa on December 14, 2007

wamkumbuka-asha.jpg

Asha Mtwangi. Ushawahi kulisikia hilo jina? Wapi? Unamfahamu Asha? Unamfahamu kama nani? Ulimsikia kwa mara ya kwanza wapi? Unajua anapendelea nini baada ya kazi? Anasoma vitabu vya aina gani na anasikiliza muziki upi? Chakula akipendacho je? Tafadhali kuwa wa kwanza kutujibia maswali haya na hiyo ndio itakuwa moja ya zawadi yako kwetu kwa sikukuu ya Noeli na ile ya Mwaka Mpya 🙂

Posted in Africa, Art, Bongo, Elimu, Fotografia, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi, Wadau | 6 Comments »

SIMAMA NA UPIGE SALUTI KWA CPWAAA

Posted by Bob Sankofa on December 10, 2007

02122006809.jpg

Ukiona msanii wa fani ya muziki anaingia katika fani ya kublogu ujue mapinduzi ya teknolojia yanakamata kasi Tanzania. CPWAAA, mwanabongo flavour mashuhuri Tanzania amezama ulingoni, anatumia simu yake kublogu. Simu ya CPWAAA ni zaidi ya simu. Mtembelee na umuunge mkono kwa kubonyeza hapa halafu uniambie blogu yake inaitwa nini.

Pichani ni CPWAA kulia akiwa na mcheza filamu anayefunika kuliko wote kwa sasa hapa Bongo, Kanumba.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Teknolojia, Wadau | 2 Comments »

RADIO YA WATU NA JAMII YA WATU YAPOTEZA MTU

Posted by Bob Sankofa on December 10, 2007

odi2.jpg

Clouds FM, radio ya watu imepoteza meneja wake Godfrey Odhiambo, aliyefariki jana saa kumi jioni katika hospitali ya Agah Khan, jijini Dar es Salaam. Habari hizi zimetolewa rasmi na mkurugenzi wa radio ya watu, Ruge Mutahaba.

Odhiambo, raia wa nchini Kenya, anaagwa kesho kuanzia saa sita za mchana kwenye kanisa la Pentekoste, Kinondoni. Kanisa linatizamana na soko la TX. Baadae atasafirishwa kwenda kwao Kenya.

Blogu ya Mwenye Macho, inatoa pole nyingi kwa wafiwa. Rabuka ametoa, Rabuka ametwaa, na aiweke roho ya marehemu Odhiambo mahala pema peponi, Amin

Posted in Africa, Art, Bongo, Fotografia, Kazi, Mabalaa, Msiba, Sanaa, Tanzania, Wadau | Leave a Comment »

TWASHUKURU TUMEIONA YA 46

Posted by Bob Sankofa on December 9, 2007

m.jpg

Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili uwanja wa Jamhuri, Dodoma, asubuhi leo kuongoza maadhimisho ya kilele cha siku ya miaka 46 ya uhuru wa Tanganyika, akiwa na mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Davies Mwamunyange.

Kwa mijipicha na habari zaidi cheki http://www.issamichuzi.blogspot.com

Posted in Africa, Bongo, Fotografia, Siasa, Tanzania | Leave a Comment »

IRENE HANA UTANI

Posted by Bob Sankofa on December 8, 2007

irene-wanamakumbusho.jpg

Irene Sanga na wanangoma wa kijiji cha Makumbusho wakifunga kazi. Kama ulikuwepo jana jioni utakubaliana nami kuwa Irene alipiga shoo utadhani tumelipia. Hii ni dalili nzuri kuwa siku tukiambiwa tulipie onesho la dada hatatuangusha.

Irene huwa hapendi kuitwa mwanamuziki kwani huwa anasema yeye ni zaidi ya hapo. Unajua kuwa dada mbali ya kufanya muziki na ushairi, pia ana diploma ya kucheza ngoma za asili toka pale Chuo cha Sanaa Bagamoyo? Ndio ujue sasa. Kwenye picha hii ndio alikuwa anamaliza onesho. Dada anamaliza onesho utadhani ndio anaanza.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 6 Comments »

WANAMAKUMBUSHO TULIKUWA NAO PIA

Posted by Bob Sankofa on December 8, 2007

makumbusho.jpg

Pia wacheza ngoma za asili toka kijiji cha Makumbusho walikuwepo kumpa tafu Irene. Hivi Simbadeo na Luihamu mmeshawahi kuingia pale kijijini au kama ilivyo kwa wengi huwa tunakiona kijiji kwa nje tu tukisubiri basi pale kituoni, Makumbusho? Basi pale kijijini kuna hawa jamaa, hapa walikuwa wakikamua ngoma maarufu toka Zanzibar inayokwenda kwa jina la Kibati. Unacheki mambo ya kuselebuka mpaka chini hayo?

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Music, Muziki, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 10 Comments »

VITALIS WA MAEMBE

Posted by Bob Sankofa on December 8, 2007

maembe.jpg

Irene jana hakuwa peke yake, alisindikizwa na jabali la muziki wa sasa wa Tanzania, si mwingine bali mzee wa “Sumu ya Teja”, Vitalis wa Maembe. Jamaa alipiga vibao vipya viwili jana. Ila kuna kitu hakikunipendeza, na lawama napeleka kwa waandaaji wa onesho hili. Swala zima la utayarishaji wa jukwaa halikukaa vyema na kwa kiasi kikubwa lilishusha morali ya watumbuizaji wetu. Kwa mfano, hivi inakugharimu pesa ngapi kukodisha mlingoti wa kipaza sauti (Microphone stand)? Haya mambo ya kushikiana vipaza sauti yani sio kabisa, inakuwa kama vile tuko kwenye mazoezi ya onesho na si onesho halisi. Samahani kaa nimewakwaza.

Well done Maembe.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

WAUNGA MKONO WA IRENE

Posted by Bob Sankofa on December 8, 2007

sehemu-ya-nyomi.jpg

Hii ni sehemu ya nyomi lililojitokeza kumuunga mkono dada Irene Sanga. Unajua mirindimo ya muziki wa Irene inatia midadi vibaya mno lakini kuna maneno huwa anayasema kwenye mashari yake ambayo huwa ni mazito kuliko mirindimo ya muziki wake. Basi ikifikia hali hiyo hadhira hutulia tuli na kusikiliza tungo zile. Wala rushwa hutamani kutoka ukumbini lakini ndo washalipia tiketi, wezi hutamani kuejesha walichoiba lakini huona aibu, wapenzi hutamani dunia isifike tamati. We cheki jamaa walivyotega sikio zao, kudadadeki Irene!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

IRENE AADABISHA USHAIRI JUKWAANI

Posted by Bob Sankofa on December 8, 2007

irene.jpg

Irene Sanga, mtunzi na mghani mashairi wa Kitanzania, jana usiku kwenye kituo cha utamaduni wa watu wa Ufaransa kama vile alivyotuahidi katika mwaliko wake, kwamba atalichakaza jukwaa, ndivyo alivyofanya. Hakupoteza muda mwingi kuomba kupigiwa makofi kama ilivyo kwa wasanii wengi wa muziki wa kibongo. Aliingia jukwaani mitaa ya saa tatu kasorobo usiku na kuturusha kisawasawa na mashairi yake yaliyoundwa yakaundika.

Ukimsikiliza kwa undani unaweza ukasema Irene ndiye Bi. Kidude wa wakati wetu, ila sina hakika kama yeye mwenyewe analifahamu hilo, si unajua manabii huwa hawajitambui. Picha hii yuko na Elidadi Msangi, mshirika wake mkubwa katika masuala ya muziki na pia mtayarishaji wake wa sauti.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

8020 FASHIONS + MWENYEMACHO DOT COM = USIPIME

Posted by Bob Sankofa on December 6, 2007

macho.jpg

Kwenye uzinduzi wa Tanzania Mitindo House nilikutana na dada mwanablogu, Shamim wa 8020 Fashions. Dada tumekuwa tukikutana kwenye mtandao tu, ni mtu mmoja poa sana, anajua kusaka picha za maana kwa ajili ya blogu yake. Mcheki kwa kubofya hapa.

Posted in Africa, Art, Blogu za Kiswahili, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Wadau | 1 Comment »

NINI JIKO, BANANA KUPATA NA ‘KIBARAZA’ KABISA MWEZI HUU

Posted by Bob Sankofa on December 6, 2007

banana_10.jpg

Unamfahamu huyu? Unayo habari kuhusu mustakabali wake wa mahusiano ya kimapenzi?

Tarehe 30 mwezi huu atawaumiza kina dada kibao roho, kina dada wale waliokuwa wakimpimia kimtindo badala ya kusonga front na kumweleza kinagaubaga yaliyo moyoni mwao. Dada mwenzao amewapiga bao la kisigino, si mwingine ni Suzy Walele.

Suzy anamchukua Banana Zorro jumla, unaweza ukasema sentensi hiyo kinyumenyume. Kwa habari zaidi cheki Bongo Celebrity.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Sanaa, Tanzania, Vijimambo, Wadau | Leave a Comment »

KWA NINI?

Posted by Bob Sankofa on December 6, 2007

paul-na-robi.jpg

Ushawahi kujiuliza kwa nini ndege wa aina moja huruka pamoja? Kwa mfano kule Hollywood, mara nyingi utasikia mcheza sinema akioana na mcheza sinema mwenzie, mkata nyasi atajimuvuzisha na mkata nyasi mwenzake. Kwa hapa Tazania pia hali si tofauti sana. Huyu ni Paul, mchoraji mkubwa sana wa katuni na picha zingine, pia ni mwanamuziki, bofya hapa ucheki. Pembeni ya Paul ni ‘better half’ wake, Robi. Robi ni mbunifu wa mitindo na yeye na Paul kwa pamoja wanaunda lebo ya ubunifu wa mitindo inayokwenda kwa jina la Mapozi. Sasa swali linakuja, kwa nini mara nyingi wasanii huwa wanajichagua na kujimuvuzisha wao kwa wao? Mi huwa nikiwauliza hawa jamaa huwa wanabaki wanachekacheka tu. Nipe jibu fasta.

kazi-za-robi.jpg

Kushoto ni moja wapo ya kazi za Robi kutoka lebo ya Mapozi. Hii ilikuwa siku ya kumtafuta mbunifu chipukizi wa Redds. Robi alialikwa kama mbunifu msindikizaji, hakuwa akishindana. Cheki kanga ilivyoundwaundwa hadi kupata kivazi mbadala. Upo?

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo, Wadau | 9 Comments »

IRENE SANGA NA ONYESHO LA “UTANDAWAZI”

Posted by Bob Sankofa on December 4, 2007

utandawazi-poster.jpg

Irene Sanga, mtunzi na mghani mashairi ya Kiswahili baada ya kutamba sana na mashairi yake ya SALAMU KWA MJOMBA na PANGISHENI katika radio na televisheni za Afrika ya Mashariki sasa anatukaribisha kwenye onesho lake la jukwaani litakalofanyika pale kituo cha utamaduni wa watu wa Ufaransa, ufuatao ndio mwaliko rasmi;

UNAKARIBISHWA KWENYE ONESHO LA IRENE SANGA LA “UTANDAWAZI”

MAHALI: ALLIANCE FRACAISE

SIKU: IJUMAA, 7/12/2007

MUDA: SAA 8.30 – 11.30 USIKU

KIINGILIO: BURE

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kazi, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 3 Comments »

SIRI YA WAZUNGU KUFAGILIA JUA LA AFRIKA HII HAPA

Posted by Bob Sankofa on December 3, 2007

taa-za-krismasi.jpg

Wadau wenzetu wa kule Ufini wametutumia hii. Wanasema hii ni saa tisa alasiri kuelekea saa kumi ya jioni, giza totoro! Nimewahi kuulizana na wadau wengi kwamba kwa nini wazungu wakitia timu Bongo huwa wanafagilia sana swala zima la kujianika juani tukawa tunadanganyana eti kwa sababu wanataka kuwa na ngozi kama ya mtu wa Afrika. Lakini sasa tumepata jibu lenye TBS zaidi toka Ufini. Jibu ni kuwa kule Ufini katika majira ya baridi kama sasa, mchana huwa ni usiku na usiku huwa ni usiku kwa mantiki hiyo jamaa wa pale wakiona jua huwa ni full chereko.

Wadau wa Ufini wanatuambia pia kuwa sikukuu ya Noeli imeshaanza kule, si unacheki bibiye fuko la shopin’g mkononi na mataa barabarani (Sisi huwa tunaweka pamba kwenye miti ya Noeli kwa sababu hatumudu kununa taa na hatuna theluji).

Posted in Africa, Burudani, Fotografia, Kimataifa, Photography, Vijimambo, Wadau | 1 Comment »

TUMEGALAGAZWA LAKINI HATUKO PWEKE

Posted by Bob Sankofa on December 1, 2007

miss-china.jpg

Ni bibiye Zhang Zilin, mtoto kutoka China, akiwa na miaka 23 na urefu wa futi sita (mrembo mrefu kuliko wengine wote) amegalagaza warembo wengine 106 akiwemo mrembo toka Angola aliyekuwa wa pili na mwingine toka Mexico aliyekuwa wa tatu.

Yule wa Angola hana tofauti sana na dada yetu Richa, ambaye Wabongo kibao walileta soo kabinti kalipochaguliwa kuwa Miss Tanzania. Dada wa Angola yeye ni mzaliwa wa Portugal lakini amepewa uraia wa Angola na hatimaye ameitoa kimasomaso Angola na Afrika kwa ujumla.

Kwa mara nyingine tumegalagazwa lakini hatuko pweke kwani mrembo wetu ni kati ya wengine 105 waliopigwa chini. Asante Richa kwa kupeperusha bendera letu la Tanzania.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | 4 Comments »

LEO NDIO LEO

Posted by Bob Sankofa on December 1, 2007

ri1.jpg

Kule Sanya, China fainali za Malkia wa Urembo wa Dunia zimekaribia kuanza hii leo. Tanzania tunawakilishwa na dada Richa Adhia. Wadau wote wa Mwenye Macho Dot Com tunamtakia dada yetu kila la heri katika swala zima la kupeperusha bendera ya taifa lake na letu. Kuna vitu miamoja kuhusu Umalkia wa Urembo Duniani, unataka kuvifahamu? Bofya hapa uone vile blogu ya Bongo Celebrity wameviainisha

Picha kwa hisani ya http://www.issamichuzi.blogspot.com

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Tanzania | Leave a Comment »