MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for the ‘Fashion’ Category

FATMA NA MAMBO YA FESTIVE COLLECTIONS

Posted by Bob Sankofa on March 7, 2008

sauti-day-3-146.jpg
Fatma Amour wa lebo ya mitindo ya Famour kesho usiku katika hoteli ya Move n Pick atafanya onesho la mitindo ya kazi zake alilolibatiza jina la Festive Collections. Wewe umepanga kwenda wapi kesho? Basi katika mitoko yako anza na huu. Njoo na shilingi elfu ishirini za kiingilio, uje kuona mambo mazito ya dada Fatma.
modelsbc.jpg
Hawa ni wanamitindo watakovaa nguo za Famour kesho pale hotel ya Move n Pick. Usikose kumuunga dada Fatma mkono.
Advertisements

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

HAPA NDIPO HASA SHUGHULI YENYEWE ILIPOKUWEPO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mustafa-ndani.jpg

Mustafa Hasanali, mwanamitindo maarufu hapa nyumbani akijivuta taratibu kujisevia chakula kilichoandaliwa na mke wa balozi wa Palestina. Umemuona K-lyn na muonekano mpya? Amekata nywele, ametoka poa.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, mitindo, Sanaa, Tanzania | 3 Comments »

MH. SIMBA KUMBE ANAJUA KUNADI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mh-simba-na-mnada.jpg

Mh. Waziri Simba naye hakuwa na muda wa kupiga blablah, alipopewa kipaza tu akaanza kazi ya kutunisha mfuko wa kusaidia watoto wetu wanaoishi katika mazingira magumu. Mfuko unasimamiwa na Tanzania Mitindo House.

Picha hii iliuzwa kwa shilingi za kitanzania milioni tatu. 

Hujakosea, kule kulia kabisa, anayecheka kwa nguvu ni Jokate Mwegelo, msimamizi wetu wa shughuli kwa siku hiyo.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MAMA BALOZI AKIKARIBISHA WAGENI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mama-balozi-speech.jpg 

Baada ya mgeni rasmi kutia timu, Mama Balozi hakuwa na muda wa kupoteza. Alitoa hotuba iliyodumu kwa takribani dakika tatu hivi, alikaribisha na kuelezea dhumuni la shughuli. Poa sana, hasa ukizingatia watu walikuwa na njaa.

Hujakosea, kule kushot kabisa ni Richa Adhia, Miss Tanzania wetu. Alikuwepo pia.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MGENI RASMI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mh-simba.jpg
Mgeni rasmi katika shughuli hii alikuwa ni Mheshmiwa Waziri wa maswala ya Wanawake na Watoto, Mh. Simba. Hapa ndio alikuwa anatia timu, mvua ilitaka kuharibu ikabidi balozi mwenyewe ajitose na mwavuli kumuokoa waziri.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

FIDELINE BADO YUMO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

fideline-iranga-ndani.jpg

Fideline Iranga (katikati), mmoja wa wanamitindo wakongwe bado yuko juu kwenye fani hii ya ulimbwende. Na yeye alikuja kuunga mkono juhudi za Balozi na Tanzania Mitindo House katika shughuli hii ya chakula cha mchana kwa watoto wanaoishi katika mazingira  magumu.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MABADILIKO HUANZIA KWA MTU FULANI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

balozi-wa-palestina-na-mtoto.jpg

Balozi wa Palestina anaamini kuwa mabadiliko yanaweza kabisa kuletwa hata na mtu mmoja na wengine wakaunga mkono baadae. Hapa alikuwa na mmoja wa watoto 30 wanaoishi katika mazingira magumu. Ni muda mfupi kabla ya chakula cha mchana kilichoandalaiwa na mkewe.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

BALOZI WA PALESTINA NA CHAKULA KWA WATOTO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

balozi-na-mkewe-na-warioba.jpg 

Jumamosi iliyopita mke wa balozi wa Palestina pamoja na mumewe waliwaandalia chakula cha mchana watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na kuachwa yatima na wazazi wao waliofariki kwa ugonjwa wa Ukimwi. Chakula kiliandaliwa kwa ushirikiano mkubwa wa Tanzania Mitindo House ambayo nilishawahi kuizungumzia hapa.

 Pichani ni Waziri mkuu mstaafu akikaribishwa na Balozi pamoja na mkewe kwenye shughuli hiyo nyumbani kwao Oysterbay.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

8020 FASHIONS + MWENYEMACHO DOT COM = USIPIME

Posted by Bob Sankofa on December 6, 2007

macho.jpg

Kwenye uzinduzi wa Tanzania Mitindo House nilikutana na dada mwanablogu, Shamim wa 8020 Fashions. Dada tumekuwa tukikutana kwenye mtandao tu, ni mtu mmoja poa sana, anajua kusaka picha za maana kwa ajili ya blogu yake. Mcheki kwa kubofya hapa.

Posted in Africa, Art, Blogu za Kiswahili, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Wadau | 1 Comment »

LEO NDIO LEO

Posted by Bob Sankofa on December 1, 2007

ri1.jpg

Kule Sanya, China fainali za Malkia wa Urembo wa Dunia zimekaribia kuanza hii leo. Tanzania tunawakilishwa na dada Richa Adhia. Wadau wote wa Mwenye Macho Dot Com tunamtakia dada yetu kila la heri katika swala zima la kupeperusha bendera ya taifa lake na letu. Kuna vitu miamoja kuhusu Umalkia wa Urembo Duniani, unataka kuvifahamu? Bofya hapa uone vile blogu ya Bongo Celebrity wameviainisha

Picha kwa hisani ya http://www.issamichuzi.blogspot.com

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

KAZI ZA MWANZO KABISA ZA TMH

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

film-screening.jpg

Kabla hata ya kuzinduliwa rasmi TMH wameshafanya kazi nyingi za kusaidia watoto yatima wanaoshi katika mazingira magumu, tena si jijini Dar pekee, hadi vijijini wameshakwenda. Wanamitindo wanaounda shirika lile, kwa kushirikiana makampuni kadhaa ya kibiashara na vyombo kadhaa vya habari, wamefanikiwa kutengeneza filamu fupi inayoonyesha kazi kadha wa kadha ambazo wameshazifanya katika harakati zao za kuhakikisha watoto yatima nao wanapata japo nafuu ya maisha. Hapa walikuwa wakituonesha filamu ile.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

UZINDUZI WA TMH – HOTUBA

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

speech-guest-of-honor.jpg

Naibu Waziri wa Ulinzi, mzee Aboud, akitoa hotuba ya uzinduzi wa Tanzania Mitindo House huku baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba hiyo na paparazi wakihangaika kukamata kumbukumbu za kila jambo lililojiri katika hafla ile fupi iliyofanyika Coral Beach Hotel, Msasani.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

WANAMITINDO WA TMH

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

designers_tmh.jpg

Hawa ni baadhi ya wanamitindo wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Mitindo House ambao wameungana ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu baada ya kuachwa yatima na wazazi wao waliofariki kutokana na gonjwa la Ukimwi. Shirika linaundwa na wanamitindo saba na ukumbini siku hiyo walikuwemo wanne, watatu walikuwa nje ya Jiji na nchi kwa shughuli za kikazi, kwa mfano Masoud Kipanya wa kampuni ya mitindo ya KP, alikuwa Dodoma.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

TANZANIA MITINDO HOUSE YAZINDULIWA

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

cake_tmh.jpg

Hatimaye siku ya Jumamosi ya tarehe 23, shirika lisilo la kiserikali (NGO) linalokwenda kwa jina la Tanzania Mitindo House (TMH) lilizinduliwa rasmi pale hoteli ya Coral Beach, Msasani. THM ni NGO inayoundwa na wanamitindo wa Kitanzania, wakiongozwa na Khadija Mwanamboka (mwenye kitenge pichani).

Wanamitindo hawa wanaamini kwamba jamii imewapa sapoti kubwa sana kufikia mafanikio yao na kwa hivyo wanawajibika kurudisha kitu kwa jamii. Wanamitindo hawa wameungana na kuanzisha shirika hili ili kusaidia watoto walioachwa yatima, na wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na gonjwa la UKIMWI. Hadi siku ya uzinduzi shirika lilikuwa na watoto 30, walio katika mazingira mgumu kupindukia, ambao inawasaidi kwa hali na mali.

Mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Ulinzi, mzee Aboud (anayekata keki). Pia alikuwepo balozi wa Palestina (mwenye nguo nyeupe). Wanaoshudia ukataji keki kwa nyuma kule ni baadhi ya wanamitindo wengine wa shirika hilo. Tarehe1/12/2007 shirika limeandaa onesho la mitindo linalokwenda kwa jina la RED RIBBON FASHION GALA pale hoteli ya Move n Pick ambapo wanamitindo wataonesha kazi zao na asilimia 95 ya pesa zitakazopatikana zitakwenda kuchangia malezi ya watoto wale wanaoishi katika mazingira magumu. Tiketi za onesho ni TSHs. 100,000 kwa kichwa. KARIBU!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Tanzania | Leave a Comment »