MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for the ‘mitindo’ Category

FATMA NA MAMBO YA FESTIVE COLLECTIONS

Posted by Bob Sankofa on March 7, 2008

sauti-day-3-146.jpg
Fatma Amour wa lebo ya mitindo ya Famour kesho usiku katika hoteli ya Move n Pick atafanya onesho la mitindo ya kazi zake alilolibatiza jina la Festive Collections. Wewe umepanga kwenda wapi kesho? Basi katika mitoko yako anza na huu. Njoo na shilingi elfu ishirini za kiingilio, uje kuona mambo mazito ya dada Fatma.
modelsbc.jpg
Hawa ni wanamitindo watakovaa nguo za Famour kesho pale hotel ya Move n Pick. Usikose kumuunga dada Fatma mkono.
Advertisements

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

HAPA NDIPO HASA SHUGHULI YENYEWE ILIPOKUWEPO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mustafa-ndani.jpg

Mustafa Hasanali, mwanamitindo maarufu hapa nyumbani akijivuta taratibu kujisevia chakula kilichoandaliwa na mke wa balozi wa Palestina. Umemuona K-lyn na muonekano mpya? Amekata nywele, ametoka poa.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, mitindo, Sanaa, Tanzania | 3 Comments »

MH. SIMBA KUMBE ANAJUA KUNADI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mh-simba-na-mnada.jpg

Mh. Waziri Simba naye hakuwa na muda wa kupiga blablah, alipopewa kipaza tu akaanza kazi ya kutunisha mfuko wa kusaidia watoto wetu wanaoishi katika mazingira magumu. Mfuko unasimamiwa na Tanzania Mitindo House.

Picha hii iliuzwa kwa shilingi za kitanzania milioni tatu. 

Hujakosea, kule kulia kabisa, anayecheka kwa nguvu ni Jokate Mwegelo, msimamizi wetu wa shughuli kwa siku hiyo.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MAMA BALOZI AKIKARIBISHA WAGENI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mama-balozi-speech.jpg 

Baada ya mgeni rasmi kutia timu, Mama Balozi hakuwa na muda wa kupoteza. Alitoa hotuba iliyodumu kwa takribani dakika tatu hivi, alikaribisha na kuelezea dhumuni la shughuli. Poa sana, hasa ukizingatia watu walikuwa na njaa.

Hujakosea, kule kushot kabisa ni Richa Adhia, Miss Tanzania wetu. Alikuwepo pia.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MGENI RASMI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mh-simba.jpg
Mgeni rasmi katika shughuli hii alikuwa ni Mheshmiwa Waziri wa maswala ya Wanawake na Watoto, Mh. Simba. Hapa ndio alikuwa anatia timu, mvua ilitaka kuharibu ikabidi balozi mwenyewe ajitose na mwavuli kumuokoa waziri.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

FIDELINE BADO YUMO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

fideline-iranga-ndani.jpg

Fideline Iranga (katikati), mmoja wa wanamitindo wakongwe bado yuko juu kwenye fani hii ya ulimbwende. Na yeye alikuja kuunga mkono juhudi za Balozi na Tanzania Mitindo House katika shughuli hii ya chakula cha mchana kwa watoto wanaoishi katika mazingira  magumu.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MABADILIKO HUANZIA KWA MTU FULANI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

balozi-wa-palestina-na-mtoto.jpg

Balozi wa Palestina anaamini kuwa mabadiliko yanaweza kabisa kuletwa hata na mtu mmoja na wengine wakaunga mkono baadae. Hapa alikuwa na mmoja wa watoto 30 wanaoishi katika mazingira magumu. Ni muda mfupi kabla ya chakula cha mchana kilichoandalaiwa na mkewe.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

KIVAZI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

kivazi.jpg
Vijana wa Zawose ni matata sana. Cheki hawa jamaa vivazi vyao. Hivi vivazi ni zaidi ya vivazi, ni vyombo vya muziki pia. Jamaa wakiruka juu na kurudi chini vivazi hivi vinatoa mlio fulani murua sana, lakini inabidi uwe na sikio la kimuziki kuweza kutumia ala hii la sivyo ukipewa kama huna hicho kipaji utaishia kuharibu muziki mzima kwa kukosa kitu wataalamu wanaita ‘tempo’ au mwendokasi wa muziki.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Mikutano, mitindo, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

8020 FASHIONS + MWENYEMACHO DOT COM = USIPIME

Posted by Bob Sankofa on December 6, 2007

macho.jpg

Kwenye uzinduzi wa Tanzania Mitindo House nilikutana na dada mwanablogu, Shamim wa 8020 Fashions. Dada tumekuwa tukikutana kwenye mtandao tu, ni mtu mmoja poa sana, anajua kusaka picha za maana kwa ajili ya blogu yake. Mcheki kwa kubofya hapa.

Posted in Africa, Art, Blogu za Kiswahili, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Wadau | 1 Comment »

KWA NINI?

Posted by Bob Sankofa on December 6, 2007

paul-na-robi.jpg

Ushawahi kujiuliza kwa nini ndege wa aina moja huruka pamoja? Kwa mfano kule Hollywood, mara nyingi utasikia mcheza sinema akioana na mcheza sinema mwenzie, mkata nyasi atajimuvuzisha na mkata nyasi mwenzake. Kwa hapa Tazania pia hali si tofauti sana. Huyu ni Paul, mchoraji mkubwa sana wa katuni na picha zingine, pia ni mwanamuziki, bofya hapa ucheki. Pembeni ya Paul ni ‘better half’ wake, Robi. Robi ni mbunifu wa mitindo na yeye na Paul kwa pamoja wanaunda lebo ya ubunifu wa mitindo inayokwenda kwa jina la Mapozi. Sasa swali linakuja, kwa nini mara nyingi wasanii huwa wanajichagua na kujimuvuzisha wao kwa wao? Mi huwa nikiwauliza hawa jamaa huwa wanabaki wanachekacheka tu. Nipe jibu fasta.

kazi-za-robi.jpg

Kushoto ni moja wapo ya kazi za Robi kutoka lebo ya Mapozi. Hii ilikuwa siku ya kumtafuta mbunifu chipukizi wa Redds. Robi alialikwa kama mbunifu msindikizaji, hakuwa akishindana. Cheki kanga ilivyoundwaundwa hadi kupata kivazi mbadala. Upo?

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo, Wadau | 9 Comments »

TUMEGALAGAZWA LAKINI HATUKO PWEKE

Posted by Bob Sankofa on December 1, 2007

miss-china.jpg

Ni bibiye Zhang Zilin, mtoto kutoka China, akiwa na miaka 23 na urefu wa futi sita (mrembo mrefu kuliko wengine wote) amegalagaza warembo wengine 106 akiwemo mrembo toka Angola aliyekuwa wa pili na mwingine toka Mexico aliyekuwa wa tatu.

Yule wa Angola hana tofauti sana na dada yetu Richa, ambaye Wabongo kibao walileta soo kabinti kalipochaguliwa kuwa Miss Tanzania. Dada wa Angola yeye ni mzaliwa wa Portugal lakini amepewa uraia wa Angola na hatimaye ameitoa kimasomaso Angola na Afrika kwa ujumla.

Kwa mara nyingine tumegalagazwa lakini hatuko pweke kwani mrembo wetu ni kati ya wengine 105 waliopigwa chini. Asante Richa kwa kupeperusha bendera letu la Tanzania.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | 4 Comments »

LEO NDIO LEO

Posted by Bob Sankofa on December 1, 2007

ri1.jpg

Kule Sanya, China fainali za Malkia wa Urembo wa Dunia zimekaribia kuanza hii leo. Tanzania tunawakilishwa na dada Richa Adhia. Wadau wote wa Mwenye Macho Dot Com tunamtakia dada yetu kila la heri katika swala zima la kupeperusha bendera ya taifa lake na letu. Kuna vitu miamoja kuhusu Umalkia wa Urembo Duniani, unataka kuvifahamu? Bofya hapa uone vile blogu ya Bongo Celebrity wameviainisha

Picha kwa hisani ya http://www.issamichuzi.blogspot.com

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

KAZI ZA MWANZO KABISA ZA TMH

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

film-screening.jpg

Kabla hata ya kuzinduliwa rasmi TMH wameshafanya kazi nyingi za kusaidia watoto yatima wanaoshi katika mazingira magumu, tena si jijini Dar pekee, hadi vijijini wameshakwenda. Wanamitindo wanaounda shirika lile, kwa kushirikiana makampuni kadhaa ya kibiashara na vyombo kadhaa vya habari, wamefanikiwa kutengeneza filamu fupi inayoonyesha kazi kadha wa kadha ambazo wameshazifanya katika harakati zao za kuhakikisha watoto yatima nao wanapata japo nafuu ya maisha. Hapa walikuwa wakituonesha filamu ile.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

UZINDUZI WA TMH – HOTUBA

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

speech-guest-of-honor.jpg

Naibu Waziri wa Ulinzi, mzee Aboud, akitoa hotuba ya uzinduzi wa Tanzania Mitindo House huku baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba hiyo na paparazi wakihangaika kukamata kumbukumbu za kila jambo lililojiri katika hafla ile fupi iliyofanyika Coral Beach Hotel, Msasani.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

WANAMITINDO WA TMH

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

designers_tmh.jpg

Hawa ni baadhi ya wanamitindo wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Mitindo House ambao wameungana ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu baada ya kuachwa yatima na wazazi wao waliofariki kutokana na gonjwa la Ukimwi. Shirika linaundwa na wanamitindo saba na ukumbini siku hiyo walikuwemo wanne, watatu walikuwa nje ya Jiji na nchi kwa shughuli za kikazi, kwa mfano Masoud Kipanya wa kampuni ya mitindo ya KP, alikuwa Dodoma.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

TANZANIA MITINDO HOUSE YAZINDULIWA

Posted by Bob Sankofa on November 26, 2007

cake_tmh.jpg

Hatimaye siku ya Jumamosi ya tarehe 23, shirika lisilo la kiserikali (NGO) linalokwenda kwa jina la Tanzania Mitindo House (TMH) lilizinduliwa rasmi pale hoteli ya Coral Beach, Msasani. THM ni NGO inayoundwa na wanamitindo wa Kitanzania, wakiongozwa na Khadija Mwanamboka (mwenye kitenge pichani).

Wanamitindo hawa wanaamini kwamba jamii imewapa sapoti kubwa sana kufikia mafanikio yao na kwa hivyo wanawajibika kurudisha kitu kwa jamii. Wanamitindo hawa wameungana na kuanzisha shirika hili ili kusaidia watoto walioachwa yatima, na wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na gonjwa la UKIMWI. Hadi siku ya uzinduzi shirika lilikuwa na watoto 30, walio katika mazingira mgumu kupindukia, ambao inawasaidi kwa hali na mali.

Mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Ulinzi, mzee Aboud (anayekata keki). Pia alikuwepo balozi wa Palestina (mwenye nguo nyeupe). Wanaoshudia ukataji keki kwa nyuma kule ni baadhi ya wanamitindo wengine wa shirika hilo. Tarehe1/12/2007 shirika limeandaa onesho la mitindo linalokwenda kwa jina la RED RIBBON FASHION GALA pale hoteli ya Move n Pick ambapo wanamitindo wataonesha kazi zao na asilimia 95 ya pesa zitakazopatikana zitakwenda kuchangia malezi ya watoto wale wanaoishi katika mazingira magumu. Tiketi za onesho ni TSHs. 100,000 kwa kichwa. KARIBU!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fashion, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

KIKWETE HEBU NJOO TUUZE SURA KIDOGO

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

familia-na-rizwan.jpg

Hili ndio lilikuwa snepu la kufungia usiku wa jana. Hapa tulikuwa tuko kwenye harakati za kukamata usafiri tayari kurudi makwetu, mara Rizwani huyo. Nikamwambia my better half (mwenye kilemba), “Kama hatuwezi kupiga picha na ze prezident himselifu kwa nini tujivunge kunyuka na ze boi himselfu?” Hatukujiuliza mara mbili, fasta tukamkamata jamaa na kunyuka hii. Ze boi iz luk laik faza kabisa 🙂 . Huyo dada wa kizungu ni mmoja wa wadau wa blogu hii ambaye huitumia kujifunza maneno kadha ya Kiswahili kila siku, anaitwa Thea.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | 4 Comments »

IRENE UKO JUU!

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

familia-na-irene.jpg

Huwezi kuzungumzia vicheko, furaha na chereko za shughuli ya jana ya Mbunifu Bora wa Redd’s bila kumtaja Irene Kiwia. Dada na timu yake ndio alikuwa mratibu mkuu wa shughuli nzima. Kabla ya shughuli kufanyika hatukuweza kabisa kula nae snepu maana alikuwa anazunguka kama pia. Foto hili tumenyuka nae baada ya mchakamchaka wa kufa mtu. Kushoto kabisa pale ni my better half, Mwandale Mwanyekwa (the best female sculptor in town), halafu Irene (with a winning smile), halafu mshikaji wangu wa miaka tele, Freddy Halla (the cartoonist of all time), na halafu mimi niko kwa nyuma kule katika harakati za kuhakikisha na mimi natokea kwenye msenepu huu wenye watu muhimu. Hapo nilipo usinione natabasamu, nimesimamia vidole gumba vya mguu, Irene ni mrefu mno, nimetokea lakini.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | 5 Comments »

SAGANDA APATIKANA

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

freddy-na-chris.jpg

Yani nakwambia jana full vituko, full furaha, full vicheko pale Diamond Jubilee. Saganda amezoea kuwatesa watu na urefu wake. Kwa kifupi ni kuwa ni watu wachache sana ambao wanalingana na huyu bwana kwa kimo. Sasa akabugi stepu akidhani urefu ni sawa na ukubwa wa mwili, mara kikatokea kifaa hiki, Chris (mwenye kofia) jamaa ni kipisi cha mtu. Saganda akaanzisha ubishi kuwa yeye anamwili mkubwa kuliko Chris, tukasema tusiandikie mate wakati wino upo. Tukawaweka pamoja ili wapimane, cheki mambo hayo. Saganda anaweza kubishana hata na radio kwani bado haamini kuwa yeye ni kibonde kwa Chriss 🙂

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

K-LYN NA WASHKAJI

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

ntuyabaliwe2.jpg

Vyombo vya habari noma sana, huwa vinakuza watu kupita maelezo kiasi kwamba hata ukikutana na watu wale wanaokuzwa kivile unaweza ukaogopa hata kuwasalimia. K-Lyn, mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo na ambaye pia amewahi kuwa Miss Tanzania, alikuwepo jana kwenye shughuli ya Redd’s. Basi nikajipitisha mara ya kwanza nikitaka kula snepu lakini nikasita kwa kuhofia kutolewa nishai, nikarudi mara ya pili nikatabasamu kidogo na yeye akatabasamu, sikuchelewa nikabaruza hii. Dada hana makuu kabisa, akanipa ruhusa ya kubaruza foto zingine kama tano hivi, nimeziweka maktaba kwa matumizi ya baadae.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

HEE WE NDO MWENYE MACHO!?

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

mwanamboka.jpg

Nimekutana na Khadija Mwanamboka, mbunifu maahiri wa kibongo mwenye lebo la Vitu vya Khadija. Nikajitambulisha, “Dada habari, naitwa Bob Sankofa natoka Mwenye Macho dot com” Dada hakuamini, ukamtoka ukelele uliochanganyika na kicheko, “Hee, wewe ndo Mwenye Macho!? Aisee nilikuwa na taswira ya mtu tofauti kabisa” Kwa maelezo yake ni kuwa alikuwa akidhani kuwa mimi ni bonge la mtu hivi kumbe ni mrefu tu wa wastani tu na mwembamba wa haja. Dada ameniahidi mahojiano, weka masikio tayari.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | 4 Comments »

NIMESTAAFU MIKONOZ – ISSA MICHUZI

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

enough-with-mikonoz2.jpg

Jana pale Diamond warembo kibao mwanangu, yani ushindwe wewe tu kujisevia. Basi ile nakata kona tu, Michuzi huyu, yuko na totoz mbili Flaviana Matata kwa upande wa kushoto na totoz nyingine sikufanikiwa kupata jina lake. Nikamuuliza Michuzi, “Vipi Mikonoz?” akaniambia amestaafu fani hiyo siku hizi. Na snepu hili linathibitisha kwamba kweli jamaa katundika daluga za mikonoz. Kwa wadau, kama hamjui mikonoz ni lile pozi la kumwekea mwezio mkono begani wakati wa kupiga picha. Michuzi alikuwa akiipenda sana hiyo staili.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

NIMEMBAMBA

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

nimembamba.jpg

Raha za kuhudhuria shughuli kama za Mwanamitindo wa Redd’s ni zile fursa za kukutana na watu mliokuwa mnawasiliana tu kwenye mtandao. Nimekutana na guru wa fotoblogu Tanzania, Michuzi himself. Jamaa anapenda sana karoti, cheki anavyoshughulika nayo hapo mkononi. Jana ilikuwa kila tukigongana kwenye mishemishe za kupata snepu poa ananiuliza, “Sankofa umecheki watoto wa Bwawa la Maini (Liverpool) walivyo noma? Wamenyuka mtu nane bila mwanangu.” Nimefurahi sana kukutana na jamaa.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | 3 Comments »

KAKA NA DADA NGOMA DROO

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

maunda-zorro.jpg

Kwa upande wa burudani Redd’s walijipanga vilivyo hasa ukizingatia jinsi walivyohakikisha kuwa viingilio vyetu vinakidhi haja zetu. Jamaa walizama jumla kwa mzee Zahir Zorro na kufumba na kufumbua kaka na dada mtu wakatinga jukwaani, kila mmoja kwa wakati wake kutupa raha. Alianza dada, Maunda Zorro, akakamua vilivyo na kibao chake kinachowika sasa cha “Nataka Uwe Wangu”

banana-zorro.jpg

Dada alipoondoka tu kabla hata watu hawajajipanga vizuri vitini akatinga mzee mzima, Banana Zorro na kibao chake cha “Mama Kumbena”. Alipiga ‘Mama Kumbena original’ halafu baadae akapiga kitu inaitwa ‘Mama Kumbena Michael Jackson Version’. Hii familia, kwa swala zima la muziki ni balaa mtu wangu.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »

MSEMA CHOCHOTE

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

jokate-wetu.jpg

Niliwahi kusema kuwa Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 ni maktaba ya vipaji. Hajafikisa miaka 25 tayari ameshacheza sinema, ameshakuwa mrembo wa Tanzania, ameshakuwa balozi wa Redd’s, ameshafanya matangazo ya radioni na jana kwa kati ya mara zilizo nyingi, ndio alikuwa mwendesha shughuli katika shindano la kumtafuta mbunifu maahiri wa Redd’s. Huyu si mwingine ni Jokate. Ukicheki hiyo posture tu utajua kuwa dada anajiamini. Kanyaga twende Jokate.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | 6 Comments »

NA MSHINDI NI…

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

na-mshindi-ni.jpg

Wabunifu waliokuwa wakishindania nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa kupitia Redd’s walikuwa sita. Wabinifu wote walikuwa safi sana ila Mama Hilda Bandio ndio alikuwa kiboko zaidi. Aliwavisha warembo wake magauni ya mkeka na magome ya mgomba. Hili la mgomba (amevaa mrembo hapo kushoto) ndio lilikuwa funiko la kufa mtu. Mama Hilda anakwenda kutuwakilisha Msumbiji. Hongera sana Mama Hilda, hii staili ya kuwavalisha watu mimea imetulia.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | 1 Comment »

TOTOZ!

Posted by Bob Sankofa on November 10, 2007

warembo.jpg

Jana nilihudhuria fainali za mchakato za kumtafuta mbunifu bora wa mitindo wa Redd’s pale Diamond Jubilee. Mbunifu yule ndiye ataliwakilisha taifa letu baadae kule Msumbiji. Nilikamata siti ya mbele kabisa ili niweze kuzishuhudia ‘totoz’ kwa ukaribu wa kipekee. Cheki maubunifu hayo lakini zaidi cheki totoz mwanangu. Redd’s, itabidi hii kitu iwe inafanyika kila mwezi, ni safi kwa afya.

Posted in Africa, Art, Biashara, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, mitindo, Photography, Tanzania, Vijimambo | Leave a Comment »