MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for August, 2007

TUNAKUINUA TUKITAKA, TUNAKUDONDOSHA TUKITAKA!

Posted by Bob Sankofa on August 31, 2007

oj-simpson.jpg

Duka la vitabu la Barnes & Noble Inc. pale Marekani, baada ya kukataa katukatu kuuza kitabu cha O. J. Simpson hatimaye wamebadili msimamo wao na kulamba matapishi yao.

Unamkumbuka OJ, ni yule mchezaji wa mpira wa miguu (japo muda mwingi hutumia mikono) wa Kimarekani, ambaye mwaka 1994 alishutumiwa kumuua mkewe pamoja na mpenzi wa mkewe ambao eti aliwabamba live kwenye gari lake la kifahari “wakiiba” penzi. Kesi yake ilikuwa tata sana, nakumbuka baba yangu alikuwa ni mtu wa mwisho kila siku kulala akiifuatilia kupitia CNN, na siku OJ aliposhinda alifurahi utadhani ni Mmarekani. Nafikiri watu weusi karibu wote duniani walifurahi kwa sababu toka mwanzo kesi ilikuwa ikiendeshwa kwa misingi ya kibaguzi na hivyo kujenga kambi mbili, za watu weusi (waliokuwa upande wa OJ) na watu weupe (waliokuwa upande wa mke wa OJ na hawara yake ambao wote ni wazungu) Read the rest of this entry »

Advertisements

Posted in Biashara, Kimataifa, Siasa, Vijimambo | Leave a Comment »

MUHIMU KWA MASUPASTAA WA BONGO

Posted by Bob Sankofa on August 30, 2007

ny127_people_lil_waynesff.jpg

Watu wa Magharibi ni watu wa ajabu sana, kila kitu wanakigeuza dili. Cheki, eti kuna demu mmoja kaenda kwenye onesho la muziki (concert) la yule mfokaji maarufu Lil’ Wayne kule Morgan State University, mwezi Oktoba mwaka jana, Lil’ kwa kutafuta sifa akawarushia washabiki fedha (nafikri ni maelekezo ya mganga wake), na kwa umasikini wa washabiki, si wakaanza kukanyagana wakirukia hizo njululu na kwa bahati mbaya yule demu akakanyagwa hadi kupoteza fahamu. Read the rest of this entry »

Posted in Burudani, Fotografia, Kimataifa, Photography, Sanaa, Vijimambo | Leave a Comment »

WAPI (MAMA AFRIKA) – NYEPESI

Posted by Bob Sankofa on August 29, 2007

img_1273.jpg

WAPI si mahala pa kuja kujirusha tu, ukizidiwa sana unaumweka pia. Hawa jamaa walipofika tu wakatafuta viti na kuuweka. Walipokuja kuzinduka WAPI imekwisha. Hapa walipokaa si mbali sana na spika zilipo, jamaa sijui waliwezaje ‘kupoteza’ na mziki wote ule. 🙂 Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania, Vijimambo | 4 Comments »

WAPI (MAMA AFRIKA) – NANI ALIKUWEPO?

Posted by Bob Sankofa on August 29, 2007

saigon-mmoja-wa-waasisi-wa-rap-za-kiswahili-alikuwa-na-kundi-la-diplomatz-katika-miaka-ya-90.jpg

Saigon alikuwepo, si unakumbuka lile kundi la Hip Hop la Diplomatz? Lilikuwepo katika miaka ya kati hadi mwishoni mwa ’90, huyu alikuwa ni mmoja wa waliokuwa wanaunda kundi lile. Saigon ni mkali wa miondoko ya Hip Hop maarufu kama mtindo huru (free style). Sasa hivi Saigon anafanya kazi stesheni ya televisheni ya EATV, ana kipindi chake kinaitwa Hip Hop Base. Kati ya vipindi matata vya EATV hiki ni kimoja kati ya vile vinavyoshika nafasi ya juu. Basi jamaa nae alikuwepo kuwapagawisha watu na mtindo huru. Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania | 4 Comments »

WAPI (MAMA AFRIKA) – KILA MTU ANAYO HAKI YA KUSIKIA

Posted by Bob Sankofa on August 27, 2007

img_1206.jpg

Dada huyu (jina lake sikufanikiwa kulipata), yeye alikuja na rafiki zake, hao waliomzunguka, ambao wana ulemavu wa kusikia (viziwi). Dada alihakikisha wote kwa pamoja wanafuatilia utamaduni wa WAPI tangu mwanzo hadi mwisho. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa hao jamaa ni washairi wa kiswahili, kwa hivyo hawakuja kuvuna tu bali kuzalisha pia. Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania | 3 Comments »

WAPI (MAMA AFRIKA) – KILA MTU ANA HAKI YA KUSEMA

Posted by Bob Sankofa on August 27, 2007

img_1182.jpg

Huyu anaitwa Dana, mwanafunzi pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alipewa nafasi ya kueleza, yeye kama mwanazuoni, ameielewa vipi kauli mbiu ya mwezi huu, yaani “Mama Afrika”? Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Burudani, Elimu, Filamu, Fotografia, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania | 3 Comments »

WAPI (MAMA AFRIKA) – ONYESHA UWEZO

Posted by Bob Sankofa on August 27, 2007

 utamaduni-wa-wapi-unampa-kila-mmoja-utamaduni-wa-kuonyesha-kipaji-alichonacho-dada-huyu-yeye-ni-mshairi-wa-kiswahili.jpg

Utamaduni wa WAPI unampa kila mmoja nafasi ya kuonyesha kipaji alichonacho, unachotakiwa ni kujiandikisha mapema kabla ya siku halisi ya utamaduni wa WAPI. Dada huyu yeye ni mshairi wa kiswahili, anachanganya mashairi na kucheza ngoma za Kiafrika ili kupeleka ujumbe kwa hadhira. Hapa alikuwa akighani shairi aliloandika kwa ajili ya kauli mbiu ya mwezi huu, Mama Afrika. Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 2 Comments »

WAPI – MAMA AFRIKA

Posted by Bob Sankofa on August 27, 2007

Kwa mara nyingine tena lile libenenge la utamaduni wa WAPI umetikisa tena jiji la Dar es Salaam. Kwa kifupi ni kuwa utamaduni wa WAPI ni utamaduni ambao umejikita katika kuhakikisha vijana wa Kitanzania, wenye vipaji mablimbali wanakutana mara moja kila mwezi na kuonyeshana uwezo. Wengi ya vijana hawa ni wale wanaoitwa “undergorunds”, wale ambao vyombo vikubwa vya habari havitaki kuwatangaza ipasavyo (kwa sababu hawana kashfa). Nitajitahidi kukuletea picha kadhaa ili na wewe ambaye hukuweza kuhudhuria mwezi huu upate kujionea haswa yaliyojiri. Fuatana nami katika mfululizo huu. 

hapa-ndipo-shughuli-za-wapi-hufanyika-kila-wikiendi-ya-mwisho-wa-mwezi.jpg

Hapa ndipo Shughuli za utamaduni wa WAPI hufanyika kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, British Council, Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwezi huu ilikuwa ni “Mama Afrika” na utamaduni ulichukua mkondo tarehe 25/8 kuanzia saa saba za mchana hadi kumi na mbili ya jioni. Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania | 3 Comments »

UNAPOZUNGUMZIA MAFANIKIO

Posted by Bob Sankofa on August 24, 2007

washkaji.jpg

Hawa ni ‘dada’ zangu, kutoka kulia ni Haika Mawala, Mkurugenzi msaidizi wa CCBRT pale Msasani, Edith Mushi Afsa Utawala hospitali ya KCKMC, Moshi na Fatina Kiluvia, Afsa Mtendaji wa Mradi CAMFED pale Oysterbay, Dar es Salaam. Hawa ni kati ya watu ninawahusudu sana. Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Burudani, Fotografia, Kazi, Photography, Teknolojia, Vijimambo | 5 Comments »

GANDHI, FUNDI NGUO

Posted by Bob Sankofa on August 24, 2007

 gandhi-spinning-wheel.jpg

Picha hii pia ni moja ya picha ninazoweza kusema iliwahi kusimamisha shughuli za ulimwengu mara ilipoingia mitaani. Picha hii ilibatizwa jina la “Gandhi Fundi Nguo”. Ilikuwa ni moja ya picha chache sana ambazo mwanamapinduzi huyu wa Kihindi alipata kupigwa. Inasemekana Gandhi hakupenda kupigwa picha. Mpiga picha maarufu, Margaret Bourke-White, wa jarida maarufu la LIFE alipotaka kumpiga Gandhi picha hii akiwa ameketi nyuma ya gurudumu lake la kufumia nguo wasaidizi wa Gandhi walimzuia na kumwambia iwapo anataka picha hiyo basi hana budi kujifunza kwanza kazi ile ya kufuma nguo. Nilipata kuzungumzia juzijuzi swala zima la kutaka kupiga picha za watu, bonyeza hapa usome. Read the rest of this entry »

Posted in Elimu, Fotografia, Kazi, Photography, Siasa, Tanzania, Teknolojia | 2 Comments »

MAITI YA CHE – MOJA YA PICHA 13 ZILIZOSIMAMISHA ULIMWENGU

Posted by Bob Sankofa on August 23, 2007

che-corpse-freddy-alborta.jpg 

“Mwendawazimu”, “mzuka”, “balaa”, “shujaa”, “mkombozi”. Hayo ni baadhi ya majina ambayo yule mwanaharakati na mwanamapinduzi Ernesto “Che” Guevara alipata kubandikwa. Mwanazuoni Jean-Paul Sartre alipata kusema, “Che ni mwanadamu mkamilifu aliyepata kuishi wakati wetu”. Unaweza usikubaliane katukatu na mwanazuoni huyu lakini katu hutoweza kubisha ya kuwa Ernesto ndiye Baba Mtakatifu wa Kimapinduzi. Nasikia hata yule mbunge wenu waliyemtimua kule Dodoma anamhusudu sana huyu bwana. Sina hakika na hilo, mimi pia nimesikia tu. Sina hakika, walahi tena, sina hakika kabisa. Mimi nakubaliana kabisa na mwanazuoni huyo hapo juu kwa sababu heshima ya Che imejengeka zaidi baada ya kufa kwake kuliko hata wakati alipokuwa akiishi. Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Photography, Siasa | 4 Comments »

NATAKA KUFANYA FOTOGRAFIA YA WATU, NAANZAJE?

Posted by Bob Sankofa on August 21, 2007

mother-and-child.jpg 

Baada ya kwenda kupumzika kule Visiwa vya Karafuu wikiendi iliyopita, na kamera yangu mkononi, niligundua kuwa nimekuwa nikifanya fotografia ya vitu zaidi ya watu na hivyo nadhani nahitaji kufanya fotografia ya watu sasa, yani fotografia ya marafiki wa karibu na wale wa kukutana nao papo kwa hapo.

Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Photography, Tanzania | 6 Comments »

JE NI UHAINI KUULIZA?

Posted by Bob Sankofa on August 20, 2007

img_1036.jpg 

Nilikuwa Zanzibar wikiendi hii, nimekwenda kupumzika baada ya msongo wa kazi kuanza kunitoa umaarufu. Nina rafiki yangu mmoja anaitwa Mejah, niliwahi kumzungumzia huko nyuma wakati fulani, bonyeza hapa kusoma zaidi, basi Mejah anasema, “Iwapo unafanya kazi kwa mwaka mzima, iwe ni kazi yako binafsi ama ya kuajiriwa, halafu unashindwa kwenda kupumzika mbali na nyumbani kwako japo kwa siku moja, basi ujue kuwa hiyo kazi unayofanya ni ya kitumwa.”

Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Photography, Siasa, Tanzania | 1 Comment »

JIFUNZE FOTOGRAFIA KWA KUTUMIA MITANDAO YA PICHA

Posted by Bob Sankofa on August 15, 2007

ethiopian-coffee.jpg 

Zamani ukitaka kujifunza kuwa mwanafotografia ilikuwa ni lazima uende chuo cha mafunzo na ulipe ada kubwa, kweli si kweli? Yuko mwalimu mmoja wa fotografia anaitwa Ibarionex R. Parello, Parello amewahi kuandika insha inaitwa “Learning from Sharing Photos Online”, katika insha ile anasema zamani hakuwahi kuwa na marafiki wengi wa kumhamasisha kupiga picha. Mahala pekee ambapo aliweza kupata hamasa ilikuwa ni ama kwenye jumba la maonyesho ya picha au kwenye majarida aliyokuwa akinunua kila mwezi.  

Read the rest of this entry »

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Photography, Tanzania | 5 Comments »

WANABLOGU WAANZA KUKUTANA

Posted by Bob Sankofa on August 14, 2007

ringo32.jpg 

Muda si mrefu niliandika wazo la wanablogu wa Kitanzania kutembeleana na kukutana. Kaka Luihamu na Da Mija wao tayari wameshalifanyia kazi wazo lile. Picha hii niliombwa na kaka Luihamu kuihariri ili iwe ya Black and White. Nilijaribu kumtumia kwa email lakini ikagoma, nafikiri email yake si sahihi sana. Kwa hivyo kaka Luihamu tafadhali ichukue picha hii kwa kutokea hapa bloguni. Read the rest of this entry »

Posted in Fotografia, Mikutano, Photography, Tanzania, Teknolojia | 7 Comments »

SANKOFA UNATUMIA “BUNDUKI” GANI?

Posted by Bob Sankofa on August 11, 2007

img_0832.jpg 

Nimepata barua pepe kadhaa nikiulizwa huwa natumia “bunduki” gani kufanyia “mauaji” yangu? Barua pepe hizi nyingi ni kutoka kwa rafiki zangu wa kule www.flickr.com/photos/mwenyemacho na wachache kutoka hapa. Kwa mantiki hiyo badala ya kujibu mmoja mmoja nimeamua kuwapa haki sawa wote kwa pamoja humu bloguni.

Kwa haraka ni kuwa natumia “bunduki” inayoitwa Canon Digital Rebel XT, ni kama ile anayotumia kaka Mjengwa lakini ile ni babkubwa zaidi.

UHURU!

Picha na: Bob Sankofa

Model: Bob Sankofa

Mahali: Bafuni kwa Sankofa

Posted in Elimu, Fotografia, Teknolojia | 5 Comments »

USHAWASIKIA MANYANI NANI BAND?

Posted by Bob Sankofa on August 11, 2007

Kuna bendi fulani hapa nyumbani inaitwa “Manyani Nani?”. Bendi hii ni kiboko sana kuanzia kwenye upigaji hadi utunzi wa mashairi. Kuna wakati fulani waliwahi kutoa wimbo wao mmoja unaitwa “Ali Baba”. Muulize Ndesanjo wa www.jikomboe.com, atakupa kisa kizima kuhusu wimbo ule. Nakumbuka Ndesanjo aliwahi kuwa na mazungumzo na Paul Ndunguru ili aurushe ule wimbo kwenye blogu sijui aliishia wapi, eti Ndesanjo. Ukisikiliza ule wimbo unaweza usipige kura Mwaka 2010.

Sasa jana jioni Manyani Nani? Band Walinialika kule katika studio za MFDI, Msasani Peninsular. Wako pale wanarekodi nyimbo zao mbili. Nikaruhusiwa kupata picha kadhaa na nikaona si haba nikishirikiana nanyi ndugu zangu.

paul-ndunguru.jpg

Huyu ni Paul Ndunguru, yeye ndiye Mwimbaji kiongozi na pia mtunzi wa Mashairi ya Manyani Nani? Band. Anapiga gitaa kavu pia. Bonyeza hapa umuulize Tungaraza wa kuhusu vipaji vingine alivyonavyo huyu bwana Read the rest of this entry »

Posted in Burudani, Fotografia | 2 Comments »

KIBLA YA KWANZA TANGANYIKA

Posted by Bob Sankofa on August 10, 2007

kibla-ya-kwanza.jpg

Kaka Charles ni tour guide (Kiswahili chake inakuwaje hapa?) pale magofu ya Kaole Bagamoyo. Jamaa ana umri mdogo lakini akianza kukuhadithia historia ya mahala pale unaweza ukafikiri jamaa aliishi Karne ya Saba baada ya kuzaliwa Yesu Kristo (Jengo hili la msikiti lilijengwa kipindi hicho). Tulikwenda kutembea hapa na Wangui.

Wangui amesomea Mambo ya Kale na Charles naye anakwenda kuanza digrii yake ya kwanza ya Mambo ya Kale pia. Kuna lugha fulani watu wa Masuala ya Kale huwa wanatumia, basi Wangui na Charles walikuwa wanatumia hiyo. Mimi sielewi sana lugha hiyo kwa hiyo nikawa napoteza muda mwingi kuwachabanga mafoto. Charles akinigeukia natingisha kichwa kama ishara ya kukubaliana nae na kwamba naelewa anachosema, walahi angejua 🙂

Ati Charles anatuambia eneo hili ndilo la kwanza kabisa (Kibla) Sheikh wa Kiislamu kusimama na kutoa ibada kwa waumini wa dini ya Kiislamu. Bonge la msikiti mshikaji wangu ila umebaki historia. Asante sana Charles kwa “kuguide”.

Hadi wakati mwingine,

UHURU!

Posted in Elimu, Fotografia | Leave a Comment »

MAVITU NANE KUHUSU MIE

Posted by Bob Sankofa on August 10, 2007

new-image.jpg

Niliwahi kuandikiwa na Serina nikiambiwa niainishe vitu nane kuhusu mimi.

Cheki sasa vile vitu nane kunihusu;

1. Napenda kustaajabia ya Musa na Rabuka pia.

2. Napenda kusafiri.

3. Napenda ajira za mkataba mfupi. Kwa nini? Soma namba mbili

4. Napenda sana teknolojia digitali.

5. Napenda vitabu japo huwa siviamini kwa asilimia mia moja, hasa vikiwa na takwimu ndio kabisa siviamini.

6. Napenda kufanya kazi kama timu.

7. Napenda kujaribu mfupa uliomshinda fisi.

8. Napenda Kamera. Kwa nini? Soma namba moja.

Serina upo hapo?

UHURU!

Posted in Fotografia, Vijimambo | 1 Comment »

IMANI NI JUU YAKO

Posted by Bob Sankofa on August 9, 2007

prayers-works.jpg

Zungumza na waliokutangulia,

Wanasikiliza,

Wakishasikiliza,

Wanazungumza pia.

UHURU!

Picha na: Bob Sankofa

Model: Wangui wa Kimari

Eneo: Magofu ya Kaole, Bagamoyo

Ushairi: Bob Sankofa

Posted in Fotografia, Ushairi | 2 Comments »

MUGONGO MUGONGO YA PWANI!

Posted by Bob Sankofa on August 9, 2007

Ulishawahi kuona ndugu zetu wa visiwa vya karafuu wakiyarudi magoma ya pwani?

Video hii niliipiga kwenye mkutano wa TED pale Arusha mwezi wa sita mwaka huu. Wakinadada hawa ni wanenguaji wa Bi. Kidude, yule mkongwe wa muziki wa mwambao.

Nilikuwa nasikia tu kwamba muziki wa mwambao pia wanakata viuno balaa. Hebu shuhudia kwa macho yako mwenyewe jinsi wakina dada hawa na bendi lao wanavyolisakanyua jukwaa pale Ngurudoto Lodge.

UHURU!

Posted in Burudani, Filamu, Sanaa, videokasti, Vijimambo | Leave a Comment »

MKUTANO WA WANABLOGU WA FOTOGRAFIA – SPAIN

Posted by Bob Sankofa on August 8, 2007

Wanablogu wanaofanya fotografia wa kule Barcelona, Spain walikutana kwa mara ya kwanza, tarehe 17/02/2007. Ni jitihada fulani ya watu wanaofanya kitu kinachofanana kufahamiana, kushirikiana na kuonana.

 Swali linakuja, Mjengwa, Michuzi, Kidevu, lini na sisi tutakutana? Yani pamoja na wanafotografia wengine, hata wale wasio na blogu. Ni vyema tukikutana, ama sivyo?

Cheki video hii, jamaa wanaongea Kispaniola, sielewi kitu lakini picha za video hii zinaeleza kila kitu. Unaona nguvu ya picha mgando na video?

Hadi wakati mwingine,

UHURU!

Posted in Fotografia, Mikutano, videokasti | 1 Comment »

WEWE UKO KAMA MIMI?

Posted by Bob Sankofa on August 8, 2007

Je wewe uko kama Sankofa? Unapenda picha zenye rangi nyeupe na nyeusi pekee? Jumuika nami katika kula darasa hili la jinsi ya kubadili picha yako ya rangi kwenda nyeusi na nyeupe pekee.

Sijui ilkuwaje nikawa napenda mtindo huu wa picha, nilijaribu siku moja nikajikuta nimekamatika kabisa. Twende tukale maarifa.

Posted in Elimu, Fotografia, videokasti | 2 Comments »

MBIONI KUTENGENEZA KITABU

Posted by Bob Sankofa on August 8, 2007

talking-is-good.jpg

Niko katika mchakato wa kuandika kitabu changu cha kwanza. Kitabu kitakuwa ni mkusanyiko wa picha hamsini na mashairi hamsini yanayoelezea mantiki za picha hizo. Kitabu kitakuwa na jumla ya kurasa miamoja

Picha hizo hazitakuwa tofauti sana, nyingi ni hizi ambazo nimewahi kuzirusha humu bloguni na kule www.flickr.com/photos/mwenyemacho.

Kitabu kitaitwaje? Kitabu kitaitwa “REVISITING ME” ama “KUJIDADISI”. Nimegundua kuwa tangu nimeanza kufanya fotografia, nagundua mambo mengi sana kunihusu mimi. Kuna nguvu fulani ilikuwa imelala ndani mwangu kwa muda wa miaka ishirini na saba, sasa imeamka. Kitabu kitaeleza kwa undani.

Hadi wakati mwingine,

UHURU

Posted in Elimu, Fotografia | 6 Comments »

KAZI! KAZI! KAZI!

Posted by Bob Sankofa on August 8, 2007

gvobadge150x50.png

Tafadhali bonyeza hapa kwa haraka sana na uombe kazi pale Global Voices. “Sankofa wewe umeomba?”. Ndio, nimeshaomba. Nasubiri majibu.Nadhani Ndesanjo wa www.jikomboe.com atafafanua juu ya hili muda si mrefu.

Usiache kuomba tafadhali, tarehe ya mwisho kutuma maombi ni tarehe 24/08/2007. Tafadhali, tafdhali, tafadhali, usiache kuomba.

Hadi wakati mwingine,

UHURU!

Posted in Kazi, Teknolojia | Leave a Comment »

TUMESIKIA SANA KUHUSU “STELA” SASA “MICHAEL”

Posted by Bob Sankofa on August 6, 2007

Samahani, hakuna picha leo kwani kisa ninachorusha si changu hasahasa.

Ndesanjo aliwahi kuja na kisa cha Stela kama utani hivi. Sasa hivi kuna mlipuko mkubwa sana wa wanablogu wa Kitanzania katika kuelezea huko walikopita. Nimeona “Stela” wa Ndesanjo, Luihamu na mimi mwenyewe nikaelezea kuhusu “Stela” wangu, nasikia Simon nae karusha wake, sijacheki bado. Lakini akatokea dada Jane Mhando na kudai kuwa hata wao wana kina “Michael” wao na atamrusha bloguni muda si muda.

Cheki jinsi dada Jane alivyokirusha kisa kile kwa ufundi. Yani unajisikia kama vile kisa hiki kinatokea sasa. Dada Jane Anasema; Read the rest of this entry »

Posted in Burudani, Tanzania, Vijimambo | 5 Comments »

NDESANJO NDANI YA WIKIMANI

Posted by Bob Sankofa on August 4, 2007

ndesanjo.jpg

Yule mwanaharakati wa teknolojia digitali na mwanablogu, Ndesanjo Macha, yuko Taiwan kwenye mkutano wa Wikimania. Ametutumia picha hii iliyopigwa na mmoja wa wajumbe wa www.flickr.com. Ndesanjo anatuambia ametua Taiwan lakini “nyundo ” yake (tarakilishi) imegoma kuwaka, pole sana mzee. Kwa mantiki hiyo atakuwa akitupasha habari kwa kutumia tarakilishi za jumuiya, si ndio Ndesanjo?

Bonyeza hapa uunganishwe na www.jikomboe.com kuelekea kwenye www.flickr.com kuupata mkutano mzima kwa njia ya picha na viunganishi vingine vingi.

Tunashukuru sana Ndesanjo kwa kutuunganisha na mkutano huo.

Mpaka wakati mwingine,

UHURU!

Posted in Fotografia, Mikutano, Teknolojia | 1 Comment »