MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for January, 2008

HERI KWA MWAKA MPYA NA A NOVEL IDEA MPYA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

heri-ya-mwaka-mpya.jpg 

Washairi wakitakiana mwaka mpya wenye mafanikio kwa kilabu na wakitoa shukrani kwa duka la A Novel Idea kwa kuwapa sapoti ya kutosha kwa mwaka wa tatu sasa. Moja ya lengo ililojiwekea kilabu kwa mwaka huu ni kuhakikisha kinachapishwa kitabu cha ushairi kilichoandikwa na wanakilabu. Heri ya Mwaka mpya.

Advertisements

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

PAUL MATATA SANA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

paul-na-mvinyo.jpg

Paul ana vituko sana, yani jamaa akiona bilauri lako limepungua kidogo tu ana wewe, saa nyingine anakucheki machoni halafu anajua unataka kuongeza mvinyo lakini unaona aibu hivi, basi anakuibukia fasta na chupa mkononi. Hapa ni baada ya Neema kuingia na kutekwa na majadiliano ya ushairi hadi kujisahau kujihudumia hivyo ikabidi Paul amkumbushe kuwa kuna mvinyo, kwa staili hii. Safi sana ukiwa na wenyeji wa hivi sio unakuwa kama kina sisi, tunakukaribisha one time ukijivunga sisi tunasonga.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

USHAIRI NA MVINYO NI CHANDA NA PETE

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

curthbet.jpg 

Mratibu msaidizi wa Kilabu cha ushairi na pia mtunzaji wa blogu ya kilabu, kaka Curthbet, akisoma shairi liloandikwa na dada Caroline. Ni shairi fupi lakini inabidi ulisome mara kadha kuweza kung’amua mwandishi alikuwa wakiwasilisha kitu gani, mvinyo unafungua ubongo wako kwa haraka ndio maana kaka alihakikisha hachezi nao mbali. Pale kushoto ni mchpishaji maarufu wa vitabu, mama Demere.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

SAMAHANINI NIMECHELEWA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

samahani-nimechelewa.jpg 

Mratibu mkuu wa kilabu cha washairi hapa Bongo, Neema Kambona, aliingia amechelewa kidogo, nafikiri ni sababu ya ile kitu inaitwa foleni za magari. Aliingia tayari shairi moja likiwa limeshasomwa. Aliomba radhi kwa kuchelewa kwake “kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake” 🙂 na pia tulimpatia nafasi ya kulisikia shairi lililompita tayari. Paul na Sarah, wamiliki wa maduka ya A Novel Idea, wakimsikiliza Neema akiomba msamaha.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

UNAPOZUNGUMZIA NAFASI YA KUTOSHA…

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

washairi-na-2008.jpg 

Duka hili la A Novel Idea ambalo limekuwa na msukumo mkubwa sana kuhakikisha kilabu cha washairi kinakuwa hapa nyumbani linavyoonekana kwa ndani. Huu ni upande mmoja tu wa duka sasa fanya ukubwa huu mara nne ndio upate duka zima. Cheki hawa jamaa walivyojiachia.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

WASHAIRI BONGO WAPATA MAKUTANO MAPYA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

a-novel-idea-mpya.jpg 

Hatimaye wanaklabu wa ushairi wa Bongo, Fanani Flavor Club, wamekutana kwa mara ya kwanza jana tangu mwaka huu uanze katika duka jipya la A Novel Idea lililofunguliwa pale Shopper’s Plaza. Zamani walikuwa wakikutana kule Sleep Way. Makutano haya ya sasa yana nafasi kubwa zaidi kwa washairi kukuruka wanavyoka na ni rahisi kufikika kwa watu wasio na usafiri binafsi. Shukrani kwa A Novel Idea.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

HAPA NDIPO HASA SHUGHULI YENYEWE ILIPOKUWEPO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mustafa-ndani.jpg

Mustafa Hasanali, mwanamitindo maarufu hapa nyumbani akijivuta taratibu kujisevia chakula kilichoandaliwa na mke wa balozi wa Palestina. Umemuona K-lyn na muonekano mpya? Amekata nywele, ametoka poa.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, mitindo, Sanaa, Tanzania | 3 Comments »

MH. SIMBA KUMBE ANAJUA KUNADI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mh-simba-na-mnada.jpg

Mh. Waziri Simba naye hakuwa na muda wa kupiga blablah, alipopewa kipaza tu akaanza kazi ya kutunisha mfuko wa kusaidia watoto wetu wanaoishi katika mazingira magumu. Mfuko unasimamiwa na Tanzania Mitindo House.

Picha hii iliuzwa kwa shilingi za kitanzania milioni tatu. 

Hujakosea, kule kulia kabisa, anayecheka kwa nguvu ni Jokate Mwegelo, msimamizi wetu wa shughuli kwa siku hiyo.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MAMA BALOZI AKIKARIBISHA WAGENI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mama-balozi-speech.jpg 

Baada ya mgeni rasmi kutia timu, Mama Balozi hakuwa na muda wa kupoteza. Alitoa hotuba iliyodumu kwa takribani dakika tatu hivi, alikaribisha na kuelezea dhumuni la shughuli. Poa sana, hasa ukizingatia watu walikuwa na njaa.

Hujakosea, kule kushot kabisa ni Richa Adhia, Miss Tanzania wetu. Alikuwepo pia.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MGENI RASMI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mh-simba.jpg
Mgeni rasmi katika shughuli hii alikuwa ni Mheshmiwa Waziri wa maswala ya Wanawake na Watoto, Mh. Simba. Hapa ndio alikuwa anatia timu, mvua ilitaka kuharibu ikabidi balozi mwenyewe ajitose na mwavuli kumuokoa waziri.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

FIDELINE BADO YUMO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

fideline-iranga-ndani.jpg

Fideline Iranga (katikati), mmoja wa wanamitindo wakongwe bado yuko juu kwenye fani hii ya ulimbwende. Na yeye alikuja kuunga mkono juhudi za Balozi na Tanzania Mitindo House katika shughuli hii ya chakula cha mchana kwa watoto wanaoishi katika mazingira  magumu.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MABADILIKO HUANZIA KWA MTU FULANI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

balozi-wa-palestina-na-mtoto.jpg

Balozi wa Palestina anaamini kuwa mabadiliko yanaweza kabisa kuletwa hata na mtu mmoja na wengine wakaunga mkono baadae. Hapa alikuwa na mmoja wa watoto 30 wanaoishi katika mazingira magumu. Ni muda mfupi kabla ya chakula cha mchana kilichoandalaiwa na mkewe.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

BALOZI WA PALESTINA NA CHAKULA KWA WATOTO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

balozi-na-mkewe-na-warioba.jpg 

Jumamosi iliyopita mke wa balozi wa Palestina pamoja na mumewe waliwaandalia chakula cha mchana watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na kuachwa yatima na wazazi wao waliofariki kwa ugonjwa wa Ukimwi. Chakula kiliandaliwa kwa ushirikiano mkubwa wa Tanzania Mitindo House ambayo nilishawahi kuizungumzia hapa.

 Pichani ni Waziri mkuu mstaafu akikaribishwa na Balozi pamoja na mkewe kwenye shughuli hiyo nyumbani kwao Oysterbay.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

MPIGIE KURA IMAM

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

mpe-shavu-imam.jpg 

Sasa basi, kabla sijasahau, waandaaji wa shindano hili walitudokeza kwamba Watanzania tunaweza kupeleka washiriki wawili kule bondeni na mshiriki anayepewa nafasi kubwa ni Imam Abbas, mshindi wa pili kwa hapa nyumbani. Kumpeleka Imam kule bondeni bonyeza hapa na umpigie kura ili tuwe na wawakilishi wawili pale kusini na kujiwekea nafasi kubwa ya kushinda ile mizawadi. Ni hayo tu!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 2 Comments »

FULL SHANGWE

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

mashabiki-wa-rage.jpg 

Mashabiki wa Rage wakimpa jamaa sapoti wakati wa mpambano

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

MAMBO YA KURA BWANA…

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

mshindi-ni-rage.jpg 

Rage alipomaliza kura zikapigwa ili kumpata mshindi. Kura za mapilato wote watatu zikamwangukia Rage. Kwa mantiki hiyo Rage ndiye mwakilishi wetu kule “bondeni” katika shindano hili la SPRITE EMCEE AFRICA. Hongera sana Rage, tunategemea utarudi na ushindi huo mnono

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

RAGE AKAJIBU

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

rage-akimchana-imam.jpg 

Baada ya Imam kumaliza ikawa ni zamu ya Rage kutoa vidonge vyake

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

KAZI IKAWA KAZI

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

imam-akilianzisha.jpg 

Fainali ikawadia, kutoka watu 71 wakabaki hawa jamaa wawili, kushoto ni Rage na kulia ni Imam Abbas. Ikarushwa shilingi na Imam akalianzisha. Cheki anavyompasha Rage. Yaani huu mchezo ni kama ule tuliokuwa tunauita malani wakati tuko wadogo, kwa waliosoma Muhimbili shule ya msingi watakuwa wanajua nazungumzia nini.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

WAKONGWE WALIOWAKILISHA

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

 wakongwe-waliowakilisha.jpg

Hawa ni baadhi ya wakongwe wengi waliokuja kushuhudia mpambano huu wa kumtafuta kinara wa mitindo huru kwa hapa Tanzania. Kushoto ni Adili wa Chapa Kazi na mwenye nywele msokoto ni Joh Makini au Mfalme

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

NUSU FAINALI YA SPRITE EMCEE AFRICA

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

watu-8-kwenye-battle.jpg 

Baada ya mchujo wa kwanza wakabaki hawa jamaa 8 ambao ndio waliingia nusu fainali, na ili kufika fainali ilibidi washiriki wawili-wawili kupambana kwa mtindo wa kurushiana maneno, kwa kizungu wanaita “Battle”. Ambaye alifanikiwa kumtupia mwenzake maneno yenye nguvu na kejeli zaidi na kuwapagawisha washabiki na kina pilato ndiye aliyesonga mbele.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

KINA PILATO THEMSELVES

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

pilato.jpg

Cheki kina pilato walivyolamba ndimu, hawacheki na kima, ni mwendo wa kulima wazugaji na kuwapa shavu halali washiriki wote waliofanya vyema. Kutoka kushoto ni pilato Lindu, pilato Profesa Jay na pilato Lufunyo. Walikuwa na kazi ya kuhakiki washiriki 71 ili kupata washiriki 8 ambao wangeingia nusu fainali na hatimaye wawili ambao wangeingia fainali. Haikuwa kazi ndogo, kazi za lawama hizi.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

CHEKI “VIFANYIO” VYA CHANNEL O

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

kamata-matukio.jpg 

Bado una swali kuhusu swala zima la Channel O kuwa na vipindi venye ubora wa hali ya juu? Angalia mashine wanazotumia, kamera HD, halafu angalia mtu anayeselebuka nayo, babu wa miaka iliyotosha. Nina hakika huyu babu atakuwa na uzoefu wa kuselebuka na kamera kwa miaka isiyopungua 30. Upo?

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

DJ STEVE B

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

dj-steve-b.jpg 

DJ Steve B ndiye alikuwa kwenye mitambo jana ili kuhakikisha washiriki wanasikika vizuri na wanakwenda sawa na mirindimo ya Hip Hop. Jamaa yuko safi katika swala zima la kuwapagawisha watu na mirindimo ya haja.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

SHINDANO SPRITE EMCEE AFRICA LIMEJIRI

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

sprite-emcee-imefanyika.jpg 

Hatimaye jana lile shindano la kumtafuta mkali wa mitindo huru, SPRITE EMCEE AFRICA, lilifanyika katika viwanja vya TCC, Dar es Salaam ili kumpata mwakilishi wa Tanzania atakayekwenda kupambana na wakali wengine wa Africa na hatimaye kujinyakulia kitita cha dola elfu 10 pamoja na mkataba wa kurekodi wimbo na video, iwapo atashinda lakini. Hao hapo jukwaani ni waendesha shughuli ya shindano, kaka Ncha Kali wa Clouds FM na dada Lee wa Channel O.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

WENYEWE HAO

Posted by Bob Sankofa on January 11, 2008

 zavara-ruge.jpg

Zavara Mponjika, kinara wa utamaduni wa WAPI alikuwepo pia. Hapa amepozi na Ruge Mutahaba wa Clouds FM. Clouds ni radio yenye mchango mkubwa sana kwa muziki wa hapa nyumbani, nadhani ndiyo radio inayosikilizwa kuliko zote kwa mijini. Clouds FM wametoa pia mchango mkubwa sana wa kulitangaza shindano la SPRITE EMCEE.

Tafadhali ungana nasi kesho kwa shindano lenyewe.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

SUALA ZIMA LA VITAFUNWA

Posted by Bob Sankofa on January 11, 2008

sprite-emcee-_-misosi.jpg 

British Council safi sana aisee. Hawawezi kabisa kukuita kwenye kongamano bila kukusabahi na chochote kitu. Hapa ni katika mapumziko ya warsha watu wakaenda kupata chochote kitu. Nadhani unamuona Emelda, mhariri mkuu wa jarida la Bang na Fid Q kule nyuma.Nakaya, niliwahi kumzungumzi hapa, naye alikuwepo pia. Hapa anabadilishana mawili matatu na wadau wengine wa muziki wa Hip Hop hapa nyumbani.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MEJAH MZEE WA TOTOZ!

Posted by Bob Sankofa on January 11, 2008

 mejah-lee.jpg

Mejah, mzee wa grafiti alikuwepo pia na hakupoteza muda sana kabla hajamkamata dada Lee, mtangazaji wa Channel O na msimamizi wa shindano la SPRITE EMCEE. Mejah amekuwa na mchango mkubwa sana katika harakati za kuendeleza sanaa ya grafiti Tanzania. Kumbuka Grafiti na Hip Hop ni kama kuku na yai, huwezi kuviachanisha hata kidogo.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

EVANS NA ADAM FULL KUZINGUANA

Posted by Bob Sankofa on January 11, 2008

evans-adam.jpg 

Kushoto ni Evans, mdau mkubwa na mwendesha shughuli za WAPI, jamaa yuko kama Chris Rock akikutana na wewe lazima akupe dongo. Hapa sijui alikuwa ashamzingua kitu gani Adam Juma, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kutengeneza video za muziki za Visual Lab. Hawa ni wadau wa muziki wa Hip Hop ambao wanahusika sana na shindano la SPRITE EMCEE.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

BONNY LUV NAYE NDANI!

Posted by Bob Sankofa on January 11, 2008

bonny-luv-ambros.jpg 

Leo asubuhi tulikuwa naye pia mtayarishaji wa siku nyingi wa miziki ya kibongo, Bonny Luv (Kushoto). Huyu jamaa mwingine anaitwa Ambros, ni mtayarishaji wa muziki pia toka studio za Mandugu Digital na pia Block 41

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

FID Q ALIKUWEPO PIA

Posted by Bob Sankofa on January 11, 2008

sprite-emcee-_-interview-fid-q.jpg 

Fid Q, mwanamuziki machachari wa muziki wa kizazi kipya alifanyiwa mahojiano na jamaa wa Channel O. Kumbe jamaa wanamnyaka sana tu huyu mshikaji. Safi sana Fid.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »