MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for the ‘Mikutano’ Category

KILABU CHA USHAIRI CHAPATA UGENI

Posted by Bob Sankofa on March 5, 2008

img_0241_3_1.jpg
Jumanne ya mwisho ya mwezi wa uliopita kile kilabu chetu cha ushairi japa Bongo kilitembelewa na mwandishi mkubwa wa vitabu vya riwaya toka kule Afrika ya Kusini. Mwandishi huyu anakwenda kwa jina la Ms. Koenings. Wanachama walifurahia nafasi hiyo kwani waliweza kumuuliza mwandishi huyu maswali kadha wa kadha.
 img_0239_1_1.jpg
Koenings akisoma sehemu ya kitabu chake alichotoa hivi karibuni. Kitabu kinakwenda kwa jina la “The Blue Taxi”.
Picha kwa hisani ya kamera ya simu ya kiganjani ya Sandra Mushi.
Advertisements

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

HERI KWA MWAKA MPYA NA A NOVEL IDEA MPYA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

heri-ya-mwaka-mpya.jpg 

Washairi wakitakiana mwaka mpya wenye mafanikio kwa kilabu na wakitoa shukrani kwa duka la A Novel Idea kwa kuwapa sapoti ya kutosha kwa mwaka wa tatu sasa. Moja ya lengo ililojiwekea kilabu kwa mwaka huu ni kuhakikisha kinachapishwa kitabu cha ushairi kilichoandikwa na wanakilabu. Heri ya Mwaka mpya.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

PAUL MATATA SANA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

paul-na-mvinyo.jpg

Paul ana vituko sana, yani jamaa akiona bilauri lako limepungua kidogo tu ana wewe, saa nyingine anakucheki machoni halafu anajua unataka kuongeza mvinyo lakini unaona aibu hivi, basi anakuibukia fasta na chupa mkononi. Hapa ni baada ya Neema kuingia na kutekwa na majadiliano ya ushairi hadi kujisahau kujihudumia hivyo ikabidi Paul amkumbushe kuwa kuna mvinyo, kwa staili hii. Safi sana ukiwa na wenyeji wa hivi sio unakuwa kama kina sisi, tunakukaribisha one time ukijivunga sisi tunasonga.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

WASHAIRI BONGO WAPATA MAKUTANO MAPYA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

a-novel-idea-mpya.jpg 

Hatimaye wanaklabu wa ushairi wa Bongo, Fanani Flavor Club, wamekutana kwa mara ya kwanza jana tangu mwaka huu uanze katika duka jipya la A Novel Idea lililofunguliwa pale Shopper’s Plaza. Zamani walikuwa wakikutana kule Sleep Way. Makutano haya ya sasa yana nafasi kubwa zaidi kwa washairi kukuruka wanavyoka na ni rahisi kufikika kwa watu wasio na usafiri binafsi. Shukrani kwa A Novel Idea.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

HUYU NI NANI TENA? ALIKUWEPO PIA

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

mtumbuizaji-wa-mwezi.jpg

Ni mdogo wa aliyewahi kuwa mmoja wa warembo waliofanikiwa sana Tanzania, amewahi kuingia katika shindano la wanamuziki Afrika Mashariki na akafika mbali, sasa ana nyimbo kadhaa zinawika radioni hapa nyumbani. Namzungumzia dada mwenye nguo ya kata mikono hapo, je unamfahamu? Pembeni yake ni mshikaji anaitwa Gaid, mwanaharakati wa fikra za mtu mweusi, anatoka kule kwa Joji Kichaka na yuko Bongo kwa mishemishe fulani hivi. Sina hakika kama anajua maana ya neno lililoko kwenye fulana yake, atakua anajua mbona anatabasamu?

mtumbuizaji-wa-mwezi2.jpg

Nilisahau kusema hapo juu kuwa dada alikuwa ndiye mtumbuizaji wetu mkuu wa mwezi huu. Hapa alikuwa anaimba ule wimbo maarufu wa Bob Marley, “Nyimbo za Ukombozi” au “Redemption Songs” kwa lugha ya kikoloni.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | 2 Comments »

HAKUNA WAPI BILA GRAFITI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

grafiti_dec.jpg
Moja ya alama nyingine ya mafanikio ya WAPI ni katika suala zima la uendelezaji wa vipaji vya wasanii wa sanaa ya grafiti. Hivi ni vipaji vilivyokuwa vimejificha kule mitaani na walikuwa wakifanya kazi zao kwa kuchafua kuta za nyumba za watu kwa kificho hadi pale utamaduni wa WAPI ukishirikiana na British Council walipoamua kutoa nafasi ya bure kwa vijana kuifanya sanaa hii bila kificho katika kuta za BC. Mwezi huu grafiti ilikuwa ikizungumzia WAPI TWENDAKO.

Posted in Africa, Art, Blogu za Kiswahili, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kazi, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Siasa, Tanzania | Leave a Comment »

MANYANI NANI NAO NDANI!

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

manyani-nani_des.jpg

Wadau wa WAPI waliona haitakuwa vyema iwapo mwaka wa shughuliza za WAPI utafungwa bila kuwaalika Manyani Nani Band ‘ku fasi ya steji’ (nimeongea Kicongo hapo). Jamaa nao hawakulaza damu, wakalisakanyua jukwaa vilivyo. Unamuona Fujo anavyoiadhibu hiyo ngoma, Paul na gitaa lake kama kawa, Hussein ‘ku fasi ya drums’. Hapakukalika.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Tanzania | 1 Comment »

KIVAZI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

kivazi.jpg
Vijana wa Zawose ni matata sana. Cheki hawa jamaa vivazi vyao. Hivi vivazi ni zaidi ya vivazi, ni vyombo vya muziki pia. Jamaa wakiruka juu na kurudi chini vivazi hivi vinatoa mlio fulani murua sana, lakini inabidi uwe na sikio la kimuziki kuweza kutumia ala hii la sivyo ukipewa kama huna hicho kipaji utaishia kuharibu muziki mzima kwa kukosa kitu wataalamu wanaita ‘tempo’ au mwendokasi wa muziki.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Mikutano, mitindo, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

DAKTA ZAWOSE BADO ANAISHI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

familia-ya-zawose.jpg

Kila utamaduni wa WAPI unapojiri familia ya marehemu mzee wetu, Dakta Hukwe Zawose huwa wanajumuika na wana-WAPI na kutoa burudani ya asili. Hii ni namna bora kabisa ya kutunza kazi na historia ya mzee hasa ukizingatia Watanzania wengi hatuna utamaduni wa kusoma vitabu, basi hii ni namna rahisi ya kumfahamu Dakta Zawose na kazi zake kupitia uzao wake. Hawa ni watoto na wajukuu wake. Zawose bado anaishi.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MPOTO TULIKUWA NAYE TENA

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

mpoto_des.jpg
Katika kufunga mwaka na utamaduni wa WAPI tulifanikiwa ‘kumtia nguvuni’ mshahiri matata hapa nyumbani, Mrisho Mpoto na tulifanikiwa pia ‘kumshurutisha’ atupe utenzi japo mmoja. Hakutukopesha akafanya mambo na akanyuka shairi lake lenye urefu wa kama dakika kumi na tano hivi, ile kumaliza tu watu wote vinywa wazi kwa jinsi jamaa alivyo na uwezo mkubwa wa kukariri mashairi yenye urefu wa kukatisha tamaa. Cheki jamaa alivyo na mzuka hadi kobadhi limemvuka.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

MAKTABA YA WATU

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

maktaba-ya-watu.jpg
Unaweza kupima vipi mafanikio ya WAPI katika mwaka 2007? Katika vitu ambavyo utamaduni wa WAPI imefanikiwa kuvianzisha katika miezi hii michache hapa nyumbani ni Maktaba ya Watu. Maktaba hii inaitwa Maktaba ya Watu kwa sababu inaundwa na watu ambao hubadilishana nakala zao za vitabu ili kujiongezea maarifa. Vingi ya vitabu vilivyopo katika Maktaba hii ya Watu ni vile ambavyo huwezi kuvipata tena katika maduka ya vitabu hapa Tanzania, mfano vitabu vya kina Shaaban Robert, Mwalimu Nyerere, maarifa ya kina Asante Kelefi na Cheikh Anti Diop. Unacho kitabu au maarifa fulani nyumbani kwako ambayo ungependa yawafikie watu wengine? Njoo navyo katika Maktaba ya Watu

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

FUNGA MWAKA YA UTAMADUNI WA WAPI

Posted by Bob Sankofa on December 27, 2007

funga-mwaka-ya-wapi.jpg

Hatimaye Jumamosi ya wiki iliyopita, wakazi wa Dar ambao pia ni wadau wa utamaduni wa WAPI walijitokeza kwa mara nyingine tena pale British Council ili kuufunga mwaka kwa utamaduni huu unaoota mizizi kwa haraka hapa nyumbani, Tanzania. WAPI ni uwanja wetu wa kujieleza na kusikiliza wenzako wanasema nini, lakini zaidi ya yote ni uwanja wa wewe kusikilizwa kuwa una nini cha kusema. Kauli mbiu ya WAPI hii ya mwisho wa mwaka ilikuwa ni “WAPI TWENDAKO?”

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

BABA WA BLOGU ZA KISWAHILI AIBUKIA DAKAR

Posted by Bob Sankofa on December 16, 2007

ndesanjo-dakar.jpg

Yamesemwa mengi kuhusu muasisi wa blogu za Kiswahili, Ndesanjo Macha. Wapo waliosema kwa kuwa hakuna malipo ya fedha katika kublogu, jamaa amekata tamaa na kazi ya kujitolea na hivyo amaecha kublogu bila kuaga. Wapo waliosema anapumzika, japo yeye mwenyewe alishasema kuwa mapumziko yamekwisha. Wapo waliosema amepata kimwana mpya Afrika ya Kusini na amembana kwelikweli kiasi kwamba hata kublogu hawezi tena. Halafu ghafla! Jamaa anaibukia Dakar. Anasambaza “injili”. Ni kweli Ndesanjo amekuwa “mwinjilisti”? Bonyeza hapa kupata jibu

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Tanzania, Teknolojia, Wadau | 1 Comment »

BALOZI KILABUNI

Posted by Bob Sankofa on December 1, 2007

balozi_poetry.jpg

Mkutano wa washairi wa Bongo (Wanafanani) ulibahatika kutembelewa na Mh. Balozi wa Palestina nchini Tanzania (katikati). Balozi huyu nimekuwa nikigongana naye sehemu kadhaa zenye matukio ya burudani yenye nia ya kusaidia jamii. Balozi na yeye ni mshahiri, mashaihiri yake ni ya kimapinduzi zaidi ya kiu kingine chochote, nafikiri sababu ya historia pia. Balozi meahidi udhamini wa hali na mali kwa kilabu cha Wanafanani.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Kimataifa, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

USIKU MWINGINE WA USHAIRI

Posted by Bob Sankofa on November 23, 2007

poetry.pngDear Lovers, (of poetry I mean! what did you think?)

Poetry nite is here once more. We meet on Tuesday 27th NOVEMBER 2007, from 19H00 at A Novel Idea Slipway. Theme for the nite is “GROWTH”.

Swahili poems are strongly encouraged, or a poem in any language for that matter. We shall listen as you read, and probably ask for a translation.

We love to sit on the floor, so please bring a mat or cushion along, plus that friend who could get inspired somehow.

COME TO POETRY NITE
“Come one, come all,
Come read, or discuss,
the magical bliss,
of poetry’s kiss…

Come grab and munch,
Sip on wine or punch,
while we sit in a bunch,
on a big round couch…

All faces are happy,
broad and shiny,
lovely and ready,
To knock down poetry…

all the same thou,
if I were you Lou?,
Or Lisa Patlou?,
I wouldnt miss out,
on poetry nite…”

by Clara Swai
@2007

* Reminding each member to contribute TShs. 3,500/= for refreshments and drinks.
* Also visit our blog at http://fananiflava.blogspot.com for more insight into what we are all about.
* Mucho gracias to “A Novel Idea” staff and management, for sharing their space and time with us all. We
continue to enjoy the 10% discount on any book purchase

Asanteni,

Clara

co co coordinator

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

MATOKE

Posted by Bob Sankofa on November 19, 2007

matoke.jpg 

Ukifika na kuondoka Uganda bila kula Matoke ni sawa na kutofika nchi hii na wenyeji wako watajisikia vibaya kwelikweli. Hakuna aina ya chakula kinachozalishwa kwa wingi katika nchi hii kama matoke na ni biashara kubwa sana inayopeleka mkono wa Waganda wengi kinywani. Hivi chakula kikuu cha Tanzania ni nini tena vile?

Posted in Africa, Biashara, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari, Tanzania | 1 Comment »

BODABODA

Posted by Bob Sankofa on November 19, 2007

bodaboda.jpg 

Usafiri wa pikipiki, maarufu kama bodaboda hapa Uganda ni almaarufu kwelikweli. Usafiri huu ni maarufu kwa sababu unawafikisha abiria wanakotaka kwenda kwa haraka. Barabara za hapa Kampala ni nyembamba na zina makorongo mengi kwa hiyo magari yanakwenda taratibu na kwa kusongamana sana. Ukitaka kufika ofisini au nyumbani kwa haraka chukua bodaboda, zinapita hadi uani mwa nyumba za watu. Tatizo zinabeba mtu mmoja tu kwa wakati kwa hiyo kama uko na my wife wako umeumia.

Posted in Africa, Burudani, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari | Leave a Comment »

IKULU YA KABAKA

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

kabaka-nje.jpg 

Naelekekea Jinja lakini mwenyeji wangu ananiambia haitakuwa vyema kwenda huko kwanza kabla ya kupita kwenye himaya ya Kabaka ama Mfalme Mutesa na nduguze na kutoa salamu pale. Basi tunaingia hapa kupata historia ya siasa za Uganda kabla na baada ya ujio wa watu weupe katika nchi hii nzuri.

kabaka-ndani.jpg

Hapa ni ndani ya Ikulu ya himaya ya Kabaka. Tunaambiwa Kabaka Mutesa alikuwa na wake 85 tu. Jamaa aliruhusiwa kuoa katika koo zote kasoro ile aliyokuwa akitoka mama yake mzazi. Lakini kuna kitu kinanishtua, Wafalme karibu wote wa himaya hii ya Buganda walikuwa wakifariki vijana wadogo kabisa, hakuna aliyezidi miaka 55. Hapakuwa na Ukimwi kipindi hicho kwa hiyo mimi nahitimisha kwa kusema labda vifo vile vilisababishwa na kufanya ngono sana na hivyo kupoteza nguvu nyingi mwilini, totoz 85 si mchezo ati.

Posted in Africa, Elimu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari, Siasa, Tanzania | 1 Comment »

MIUNDO MBINU

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

flyovers.jpg 

Naweza sema hadi sasa, Dar imewapiga bao Kampala kwa barabara nzuri lakini kuna hatari baada ya miaka mitano kama hatutafanya kitu hawa jamaa watasawazisha na kuongeza mabao kadhaa. Jamaa si kwamba wanaota tu kuhusu barabara za ghorofa, tayari wanafanya kitu. Yote hii ni harakati za kupunguza msongamano wa magari ili uchumi ukue haraka.

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari, Tanzania, Teknolojia | Leave a Comment »

KAMPALA FULL MISHEMISHE

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

kuchomekeana-tu.jpg 

Nilikuwa nadhani Bongo ndio inaongoza kwa kuchezeana rafu barabarani (uendeshaji mbaya). Kampala ni zaidi, hadi baiskeli na waenda kwa miguu “huchomeka” mtu wangu. Kila mtu anawahi sehemu fulani. Dereva wangu ananiambia  hapa gari lako linaweza kukamatwa na kusamehewa kwa makosa mengine yote lakini si makosa ya kutokuwa na breki na honi mbovu. Vitu hivyo viwili ni lazima viwe vizima ama sivyo ni mwendo wa faini tu. Hapa ni katikati ya Kampala, naelekea Jinja.

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari | Leave a Comment »

WANAMKUTANO WA TELEVISHENI NA MAZINGIRA

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

mkutano.jpg

Mataifa kumi na sita ya Afrika kila mwaka hukutana kujadili nguvu ya televisheni katika kutoa elimu ya mazingira kwa umma. Mwaka huu tumekutana hapa Uganda na mwakani tunakutana tena kule Sierra-Leon. Hawa ni wahudhuriaji wa wa mkutano huo. Wale wazungu wawili, wakinamama, ndio watoa fedha wenyewe, huyo wa kiume ni Mreno wa Msumbiji. Naupenda mkutano huu kwa sababu suti na tai sio lazima

Posted in Africa, Filamu, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari, Tanzania | Leave a Comment »

NIKO KAMPALA

Posted by Bob Sankofa on November 18, 2007

niko-kampala.jpg

Niko hapa tangu tarehe 14 jioni. Kama nilivyosema hapo awali niko hapa kuhudhuria mkutano mkubwa wa Watu wa Jumuiya ya Madola lakini pia niko hapa kuhudhuria mkutano wa Televisheni na Mazingira. Basi hawa jamaa wa Televisheni na Mazingira walikuwa wametutupa mahala fulani ambako kupata mtandao ilikuwa ni ndoto. Eti walitaka tuweke mawazo yetu yote kwenye mkutano.

Uganda, mara yangu ya kwanza hapa. Nchi poa sana, milima, miti ya kutosha na mvua za kutosha pia. Naweza kutembea hata saa saba ya usiku bila wasiwasi. Watu hawalali hapa. Poa sana, tatizo ni kuwa wanasiasa wamekuwa “wakiibaka” nchi hii tena na tena.

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography, Safari | 1 Comment »

HODI HODI KAMPALA

Posted by Bob Sankofa on November 12, 2007

39499420img_0211.jpg

Haya wadau na marafiki wa Uganda, ni wakati mwingine wa mikutano na kukutana. Nitakuwepo jijini Kampala kwa mkutano wa Jumuiya ya Madola pamoja na mkutano mwingine wa masuala ya Televisheni na Mazingira kuanzia keshokutwa, 14/11 hadi 21/11. Susan Bamutenda nitafurahi sana ukinipeleka mtaa huu kwenda kukutana na Waganda pamoja na kupata matoke na halafu baada ya hapo, Uganda by night. Sanaa Gateja nitapenda sana kutembelea duka la sanaa zako, Andrew Mwenda tukutane kwa kikombe cha chai (nimestaafu mvinyo kwa muda 🙂 na tuzungumzie siasa kidogo). Hodi hodi Kampala!

Picha kwa msaada wa Google

Posted in Africa, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Mikutano, Photography | 2 Comments »

MIAKA MIWILI YA KILABU CA USHAIRI BONGO – TUNAMALIZA KAMA TUNAANZA

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

ufungaji.jpg

Basi ilipotimu usiku wa manane siku ile ya Jumamosi tukawa tunaelekea ukingoni mwa shughuli ile nzito. Jamaa wa Simba Theatre hawakuwa na hiyana kutusindikiza majumbani mwetu kama walivyotukaribisha, wakanyuka mdundiko. Watu kuja kustuka wamefika majumbani kwao kwa mguu angali magari yao wameyaacha Alliance Fracaise. Mdundiko una nguvu ya ajabu sana ndio maana ukipita mitaani watoto huwa wanapotea sana. Nimetia chumvi kidogo hapo 🙂 . Hadi wakati mwinginge.

UHURU!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MIAKA MIWILI YA KILABU CHA USHAIRI BONGO – BAADA YA USHAIRI…

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

tatu-and-the-band.jpg

Nimewahi kusema mara nyingi hapa bloguni kwamba uzuri wa kilabu cha ushairi bongo ni kwamba huwa kuna zaidi ya ushairi. Dada Tatu alikuwepo, yeye si mshairi kwa sana, yeye ni mwanamuziki zaidi anapiga gitaa kavu. Dada Tatu alijumuika jukwaani na wanajumuiya wengine, Caroline, Asha, na Clara na wakatupa wahudhuriaji wengine vibao motomoto vya kuifagilia kilabu. Una kipaji ambacho kinaendana na ushairi kidogo, njoo tujumuike tafadhali.

msosi.jpg

Nikisema kilabu kina zaidi ya ushairi sitanii, kulikuwa na wakati wa kutosha pia kwa watu kujinafasi kwa maji ya madafu, mvinyo na mishkaki ya samaki, kwa wala majani (vejetarianz) kama sisi tulitafuna karoti na matango kama sungura. Nafikiri mkutano ujao utakuwa wa kuotea mbali. Big up Fanani Flava.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MIAKA MIWILI YA KILABU CHA USHAIRI BONGO – WAUNGA MKONO

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

waunga-mkono.jpg

Huyo mzungu wa kiume ni Paul na huyo wa kike ni Sarah. Hawa jamaa wanaiunga sana mkono jamii ya ushairi ya Bongo. Jamaa wametoa duka lao la vitabu la A Novel Idea liwe sehemu ya kilabu kukutania kila Jumanne ya mwisho ya mwezi, bure kabisa. Pia kila mwanajumuiya ya ushairi akienda kununua kitabu pale anapata punguzo la 10% ya bei ya kitabu chochote atakachonunua. Jamaa wanafungua duka kubwa zaidi pale Shoppers Plaza ili jumuiya iwe na ukimbi mkubwa zaidi, tunahamia kule muda si mrefu. Karibu!

Posted in Africa, Art, Biashara, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MIAKA MIWILI YA KILABU CHA USHAIRI BONGO – MRISHO MPOTO

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

mrisho-akitukuza-kiswahili.jpg

Katu huwezi kufanya shughuli ya ushairi hata siku moja halafu usimshirikishe Mrisho Mpoto, maana watu huwa wakifika tu kwenye shughuli hiyo swali la kwanza utakaloulizwa ni “Mrisho yupo?”. Na watu wakishaingia shughulini hawaondoki hadi wamuone huyu jamaa. Mrisho alikuwepo shughulini na kama kawaida alitema tenzi kwa Kiswahili. Cha kushangaza hata wageni (Wazungu na Waasia) walikuwa wakimshangilia. Kumbe basi ushairi ni zaidi ya lugha fulani, kwani inatuuganisha sote.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

MIAKA MIWILI YA USHAIRI BONGO – KIPAZA SAUTI HURU

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

mshairi-mdogo-kuliko-wote.jpg

Kule ughaibuni katika kilabu za ushairi kuna kitu wanaita “Open Mic Session”, hapa tunaita Kipaza Sauti Huru. Unapofika muda huu basi mtu yeyote ambaye analo shairi analotaka kulisoma kwa wenzie hupewa jukwaa na kipaza na kufanya habari zake. Kuishi kwini ni kuona mengi, amini usiamini, mtu wa kwanza kabisa kuitumia nafasi ile alikuwa ni mjukuu wa kiongozi wa siku nyingi wa nchi hii, Iddi Simba. Kabinti haka kana miaka 10 tu lakini kanaghani mashairi kama vile Maya Angelou. Huyu binti atakwenda mbali sana katika swala zima la sanaa za maonyesho.

active-audience.jpg

Si unaona hata hadhira inavyomstaajabia? Raha ya ushairi uketi sakafuni, iwapo unajisikia 🙂

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MIAKA MIWILI YA USHAIRI BONGO – HOSTORIA

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

historia-ya-ushairi-wa-kiswahili.jpg

Huyu ni dada Elizabeth Mahenge, mshairi na mwalimu wa Kiswahili, nilikuwa nae darasa moja pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka ile. Kwa sasa dada anafanya utafiti juu ya historia ya Ushairi wa Bongo. Hapa alikuwa anatupa dondoo chache za utafiti wake ambao amekuwa akiufanya kwa takribani mwaka moja sasa. Ametusaidia sana kujua tulikotoka, tulipo na tunakokwenda.

asha-fanya-mambo.jpg

Na huyu ni dada Asha Mtwangi, hapa anatoa wasifu wa Sitti Binti Saad, mshairi na mwanamirindimo ya Kipwani ambaye hata Shaaban Robert hakuweza kujizuia kuandika kitabu kizima chenye Wasifu wa Binti Saad. Asha anasema katu huwezi kuzungumzia ushairi Bongo bila kumtaja Sitti Binti Saad. Anasema pia kuwa Sitti amekufa laikini amekufa na uzuri wake kama kanga.

 

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MIAKA 2 YA KILABU CHA USHAIRI – TUSELEBUKE

Posted by Bob Sankofa on November 5, 2007

tuselebuke.jpg

Kikundi cha ngoma cha Simba Thatre kilikuwepo kuhakikisha kinatushirikisha vyema katika swala zima la mirindimo. Kikundi kiko chini ya ya uongozi safi wa Kaka Mbungu na wanapatikana pale Nyumba ya Sanaa, hawana mtimanyongo kawacheki siku moja, wanatwanga saundi kila wiki. Sunday, Neema na Asha Mtwangi hawakuwa na hiyana katika swala zima la kujiachia, selebuka mpaka chini!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »