MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

Archive for the ‘Africa’ Category

KUTANA NA NFITHE

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-1a-050_mozambique-1.jpg

Kundi la muziki wa asili kutoka pale Msumbiji. Jamaa ndio walikuwa wakwanza kabisa kulivamia na kulichakaza jukwaa. Jamaa wanapiga saundi bwana weee!

sauti-1a-052_mozambique-2.jpg

Cheki nyomi linavyowasikilizia jamaa.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

KISIA NI NANI MSIMAMIZI WA SHUGHULI HAPA

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-1a-046_dada-karola-kinasha.jpg

Ni yule mkongwe wa muziki wa Kitanzania, dada Karola Kinasha ndiye anayetumuvuzisha hapa.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

NGOME KONGWE, KILA KITU HAPA.

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-1a-039_tuko-humu.jpg

Huu ndio ukumbi wa Ngome Kongwe ambako tamasha linaendelea. Hapa ni kwa nje. Tutakuwa hapa hadi Jumapili ya jioni tamashalitakapotia nanga.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

MOTO COMBAT

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-1a-015_waongoza-maandamano.jpg

Hawa jamaa wanajiita Moto Combat, ni wasanii wa kudance hapa Zanzibar. Waliongoza maandamano ya ufunguzi jana. Nilijaribu kuangalia kwa karibu ni kitu gani wamejipaka mwilini ila sikupata jibu la haraka. Hapana, si lami, ingekuwa lami si wangeungua?

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | 1 Comment »

VIDOLE NA MACHO MTU WANGU

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

znz-full-chereko.jpg

Kina mama hawa ni baadhi ya wenyeji wa hapa Zanzibar waliojitokeza katika maandamano ya ufunguzi wa tamasha la Sauti za Busara. Watu wa hapa wanapenda sana kuweka vidole juu kama tiara. Mambo haya yana mvuto wake.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

SAUTI ZA BUSARA ZAANZA RASMI

Posted by Bob Sankofa on February 8, 2008

sauti-1a-019_maandamano.jpg

Hatimaye jana majira ya saa tisa za alasiri hapa Mji wa Mawe (Stone Town), Zanzibar, lile tamasha kubwa kabisa la muziki, Sauti za Busara, lilianza rasmi kwa wageni na wakazi wa hapa kujumuika kwa pamoja katika maandamano yaliyoanzia maeneo ya Darajani hadi pale Ngome Kongwe.  Sitegemei kuandika mengi kwani muda ni mchache na nina picha nyingi za kupandisha hapa. Pia usiniulize mbona tamasha limejaa wageni, wenyeji wakowapi. Ukome! 🙂

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Festivals, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Matamasha, Music, Muziki, Photography, Safari, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

HODI HODI ZANZIBARI

Posted by Bob Sankofa on February 6, 2008

stage-prep-kwame-collection.jpg

Haya tena, lile tamasha kubwa la muziki hapa Afrika ya Mashariki na Kati, Sauti za Busara limewadia tena. Linaanza kesho tarehe 7 na litakwisha tarehe 10. Mwenye Macho kama kawa nitakuwepo kukuletea yanayojiri pale.

Napenda kuwashukuru nyote mliotoa maoni kuhusu onesho la Mutukuzi.

Haya mabinti wa pale Zanzibari mnitayarishie maji ya kuoga yenye iliki. Inshaalah Rabuka akijalia tutakuwa pamoja kuanzia kesho asubuhi na mapema, naja na boti la kwanza kabisa.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kazi, Kimataifa, Music, Muziki, Photography, Poetry, Safari, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

TUNAMALIZA KAMA TUNAANZA

Posted by Bob Sankofa on February 3, 2008

tuku-168_maliza-kama-unaanza.jpg 

Kitu kingine cha kufurahisha kuhusu onesho la Tuku ni ile staili yake ya kumaliza maonesho yake utadhani ndio anaanza. Hapa alikuwa anapiga wimbo wa kufungia onesho. Wimbo aliopiga hapa uliwafanya watu wote kuinuka vitini na kulisakata dansi, alipomaliza na kutoweka jukwaani watu wakajua amekwenda kubadili nguo kumbe onesho ndio limeyoyoma. Nimemkubali Tuku, amepiga shoo, ukiondoa waliomsindikiza, kwa takribani masaa mawili, akiimba – kupiga gita – na kucheza, kwa masaa mawili bila hata kuomba maji. Huu ndio uanamuziki. Asante Mtukuzi, asante kwa waliomleta Mutukuzi.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 5 Comments »

HEBU FANYA NYONGEZA KIDOGO.

Posted by Bob Sankofa on February 3, 2008

tuku-118_hadithi.jpg 

Moja ya mambo yanayonifanya nipende maonesho hai ya muziki ni ile hali ya kusikia nyimbo zilezile ulizowahi kuzisikia katika radio nyumbani lakini hapa unapata na nyongeza kidogo. Nimesikiliza albamu kadhaa za Tuku na nyimbo alizopiga hapa zote nimewahi kuzisikia lakini vitu alivyofanya hapa sijawahi kuvisikia kwingine kokote. Kwa mfano hapa muziki unaendelea lakini haimbi maneno ya wimbo ule ambayo tumeyazoea bali anatoa hotuba kuhusu hali ya Zimbabwe kwa sasa. Jinsi anavyotoa hotuba ile hutachoka kumsikiliza, anaitoa kwa namna fulani ya ushairi hivi na ukiwa na akili ndogo unaweza usigundue kuwa anazungumzia Zimbabwe.

tuku-094_mdadi.jpg

Si unacheki wanamuelewa wanavyopanda midadi ya kufa mtu?

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

MUZIKI MAWASILIANO

Posted by Bob Sankofa on February 3, 2008

tuku-093_muziki-mawasiliano.jpg

Juzi kwa vile nilikuwa karibu kabisa na jukwaa niligundua kwa nini muziki wa wasanii wakubwa duniani huwa ni wa kiwangi cha juu hasa katika maonesho hai. Ugunduzi wangu ni kuwa muziki ni sawa na timu ya mpira ni lazima bendi iwasiliane vizuri ili kupata muziki mzuri. Cheki hapa Tuku anavyowasiliana na mpiga marimba wake.

tuku-142_muziki-mawasiliano2.jpg

Halafu cheki hapa Tuku anavyowasiliana na mpiga tumba wake. Yani ni kama vile wanaambizana, “tuzime muziki sasa” na kweli wanazima muziki. Upo?

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

JIKHOMAN “MIKOSI”

Posted by Bob Sankofa on February 3, 2008

tuku-027_manyika.jpg 

Pia alikuwepo Ras Jikhoman toka kule Bagamoyo. Kaka naye alisimama jukwaa moja na kaka Mutukuzi. Jikho kaanza muziki kama miaka kumi na tano hivi na ameshanyuka sound kwenye majukwaa makubwa ya kimataifa lakini bado anaizungumzia ishu ya kusimama jukwaa moja na Mwafrika kama Mutukuzi kama heshima kubwa kuliko hata zawadi ya muziki ya Grammy ya kule Marekani.

tuku-028_jikho.jpg

Jikho kazini.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

MRISHO NI WA KIMATAIFA SASA…

Posted by Bob Sankofa on February 3, 2008

tuku-012_mrisho-meza-moja.jpg

Akiwa ni mshairi wa siku nyingi, anayejituma bila kinyongo, hatimaye Mrisho Mpoto amefanya sanaa yake ya ushairi jukwaa moja na mfalme wa African Pop, Oliver Mutukuzi raia wa Zimbabwe. Ni heshima ya pekee kuona watu (watayarishaji wa sanaa za maonesho) wanaomtambua Mutukuzi wanatambua pia mchango na umaahiri wa kaka Mpoto hadi kufikia kumualika na kusimama jukwaa moja na kaka toka Zimbabwe. Mrisho na Mutukuzi watakutana tena kule Zanzibar katika tamasha la muziki la Sauti za Busara, http://www.mwenyemacho.com haitacheza mbali kukuletea kitakachojiri kule kuanzia tarehe 7 hadi 10 ya mwezi huu wa Februari.

tuku-016_mrisho-wapashe.jpg

Hapa Mrisho alikuwa akilicharanga lile shairi lake la “Nuru”. Nnachompendea Mrisho ni ile roho yake ya kujiamini. Cheki hapa palivyojaa wazungu lakini jamaa ananyuka shairi kwa Kiswahili, waelewe wasielewe watajiju! Cha kushangaza kwenye mikutano yetu mingi kukiwa na Waswahili 20 na mzungu mmoja tunajitahidi kutumia lugha ile ya yule mzungu mmoja, AIBU!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 2 Comments »

NYOMI SI LA KITOTO

Posted by Bob Sankofa on February 3, 2008

tuku-096_nyomi.jpg

Hii ni sehemu tu ya nyomi lililotiririka kwenye onesho la kwanza la Oliver Mutukuzi pale Move n Pick Hotel. Wazungu wa kumwaga, Waswahili wa kuhesabu. Mi ntaendelea tu kusema hadi tubadilike.

tuku-018_haroub.jpg

Kwa nini kila siku useme kwamba una kazi nyingi hivyo sanaa za Waafrika wenzako hazina nafasi kwenye ratiba yako. Wewe ukisema hivyo na Profesa Othman Haroub, mkufunzi wa Sheria katika chuo kikuu cha Dar es Salaam atasemaje? Maana yeye ndo kila siku anakimbizana na tafiti lakini bado hawezi kumkosa “Tuku”, alikuwepo.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 2 Comments »

MFALME WA AFRO-POP NDANI YA BONGO

Posted by Bob Sankofa on February 3, 2008

tuku-082_karibu.jpg

Ni heshima kubwa kwa www.mwenyemacho.com kupewa heshima ya kupiga picha kwa ukaribu za mfalme wa Afro-Pop, Oliver “Tuku” Mutukuzi, raia wa Zimbabwe. Niheshima kubwa pia kwa Watanzania kuona onesho hai la Tuku, mkongwe wa muziki mwenye albamu motomoto 40 hadi sasa. Mutukuzi yuko Tanzania, amefanya maonesho mawili hapa Dar es Salaam na anakwenda Zanzibar kufanya mengine mawili. Atakuwa Zanzibar kuanzia tarehe 7 hadi 11 ya mwezi huu.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Kimataifa, Music, Muziki, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

HERI KWA MWAKA MPYA NA A NOVEL IDEA MPYA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

heri-ya-mwaka-mpya.jpg 

Washairi wakitakiana mwaka mpya wenye mafanikio kwa kilabu na wakitoa shukrani kwa duka la A Novel Idea kwa kuwapa sapoti ya kutosha kwa mwaka wa tatu sasa. Moja ya lengo ililojiwekea kilabu kwa mwaka huu ni kuhakikisha kinachapishwa kitabu cha ushairi kilichoandikwa na wanakilabu. Heri ya Mwaka mpya.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

PAUL MATATA SANA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

paul-na-mvinyo.jpg

Paul ana vituko sana, yani jamaa akiona bilauri lako limepungua kidogo tu ana wewe, saa nyingine anakucheki machoni halafu anajua unataka kuongeza mvinyo lakini unaona aibu hivi, basi anakuibukia fasta na chupa mkononi. Hapa ni baada ya Neema kuingia na kutekwa na majadiliano ya ushairi hadi kujisahau kujihudumia hivyo ikabidi Paul amkumbushe kuwa kuna mvinyo, kwa staili hii. Safi sana ukiwa na wenyeji wa hivi sio unakuwa kama kina sisi, tunakukaribisha one time ukijivunga sisi tunasonga.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

USHAIRI NA MVINYO NI CHANDA NA PETE

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

curthbet.jpg 

Mratibu msaidizi wa Kilabu cha ushairi na pia mtunzaji wa blogu ya kilabu, kaka Curthbet, akisoma shairi liloandikwa na dada Caroline. Ni shairi fupi lakini inabidi ulisome mara kadha kuweza kung’amua mwandishi alikuwa wakiwasilisha kitu gani, mvinyo unafungua ubongo wako kwa haraka ndio maana kaka alihakikisha hachezi nao mbali. Pale kushoto ni mchpishaji maarufu wa vitabu, mama Demere.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

SAMAHANINI NIMECHELEWA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

samahani-nimechelewa.jpg 

Mratibu mkuu wa kilabu cha washairi hapa Bongo, Neema Kambona, aliingia amechelewa kidogo, nafikiri ni sababu ya ile kitu inaitwa foleni za magari. Aliingia tayari shairi moja likiwa limeshasomwa. Aliomba radhi kwa kuchelewa kwake “kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake” 🙂 na pia tulimpatia nafasi ya kulisikia shairi lililompita tayari. Paul na Sarah, wamiliki wa maduka ya A Novel Idea, wakimsikiliza Neema akiomba msamaha.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

UNAPOZUNGUMZIA NAFASI YA KUTOSHA…

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

washairi-na-2008.jpg 

Duka hili la A Novel Idea ambalo limekuwa na msukumo mkubwa sana kuhakikisha kilabu cha washairi kinakuwa hapa nyumbani linavyoonekana kwa ndani. Huu ni upande mmoja tu wa duka sasa fanya ukubwa huu mara nne ndio upate duka zima. Cheki hawa jamaa walivyojiachia.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

WASHAIRI BONGO WAPATA MAKUTANO MAPYA

Posted by Bob Sankofa on January 30, 2008

a-novel-idea-mpya.jpg 

Hatimaye wanaklabu wa ushairi wa Bongo, Fanani Flavor Club, wamekutana kwa mara ya kwanza jana tangu mwaka huu uanze katika duka jipya la A Novel Idea lililofunguliwa pale Shopper’s Plaza. Zamani walikuwa wakikutana kule Sleep Way. Makutano haya ya sasa yana nafasi kubwa zaidi kwa washairi kukuruka wanavyoka na ni rahisi kufikika kwa watu wasio na usafiri binafsi. Shukrani kwa A Novel Idea.

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Elimu, Fotografia, Mikutano, Photography, Poetry, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »

HAPA NDIPO HASA SHUGHULI YENYEWE ILIPOKUWEPO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mustafa-ndani.jpg

Mustafa Hasanali, mwanamitindo maarufu hapa nyumbani akijivuta taratibu kujisevia chakula kilichoandaliwa na mke wa balozi wa Palestina. Umemuona K-lyn na muonekano mpya? Amekata nywele, ametoka poa.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, mitindo, Sanaa, Tanzania | 3 Comments »

MH. SIMBA KUMBE ANAJUA KUNADI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mh-simba-na-mnada.jpg

Mh. Waziri Simba naye hakuwa na muda wa kupiga blablah, alipopewa kipaza tu akaanza kazi ya kutunisha mfuko wa kusaidia watoto wetu wanaoishi katika mazingira magumu. Mfuko unasimamiwa na Tanzania Mitindo House.

Picha hii iliuzwa kwa shilingi za kitanzania milioni tatu. 

Hujakosea, kule kulia kabisa, anayecheka kwa nguvu ni Jokate Mwegelo, msimamizi wetu wa shughuli kwa siku hiyo.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MAMA BALOZI AKIKARIBISHA WAGENI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mama-balozi-speech.jpg 

Baada ya mgeni rasmi kutia timu, Mama Balozi hakuwa na muda wa kupoteza. Alitoa hotuba iliyodumu kwa takribani dakika tatu hivi, alikaribisha na kuelezea dhumuni la shughuli. Poa sana, hasa ukizingatia watu walikuwa na njaa.

Hujakosea, kule kushot kabisa ni Richa Adhia, Miss Tanzania wetu. Alikuwepo pia.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MGENI RASMI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

mh-simba.jpg
Mgeni rasmi katika shughuli hii alikuwa ni Mheshmiwa Waziri wa maswala ya Wanawake na Watoto, Mh. Simba. Hapa ndio alikuwa anatia timu, mvua ilitaka kuharibu ikabidi balozi mwenyewe ajitose na mwavuli kumuokoa waziri.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

FIDELINE BADO YUMO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

fideline-iranga-ndani.jpg

Fideline Iranga (katikati), mmoja wa wanamitindo wakongwe bado yuko juu kwenye fani hii ya ulimbwende. Na yeye alikuja kuunga mkono juhudi za Balozi na Tanzania Mitindo House katika shughuli hii ya chakula cha mchana kwa watoto wanaoishi katika mazingira  magumu.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

MABADILIKO HUANZIA KWA MTU FULANI

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

balozi-wa-palestina-na-mtoto.jpg

Balozi wa Palestina anaamini kuwa mabadiliko yanaweza kabisa kuletwa hata na mtu mmoja na wengine wakaunga mkono baadae. Hapa alikuwa na mmoja wa watoto 30 wanaoishi katika mazingira magumu. Ni muda mfupi kabla ya chakula cha mchana kilichoandalaiwa na mkewe.

Posted in Africa, Art, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, mitindo, Photography, Sanaa, Tanzania | Leave a Comment »

BALOZI WA PALESTINA NA CHAKULA KWA WATOTO

Posted by Bob Sankofa on January 21, 2008

balozi-na-mkewe-na-warioba.jpg 

Jumamosi iliyopita mke wa balozi wa Palestina pamoja na mumewe waliwaandalia chakula cha mchana watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na kuachwa yatima na wazazi wao waliofariki kwa ugonjwa wa Ukimwi. Chakula kiliandaliwa kwa ushirikiano mkubwa wa Tanzania Mitindo House ambayo nilishawahi kuizungumzia hapa.

 Pichani ni Waziri mkuu mstaafu akikaribishwa na Balozi pamoja na mkewe kwenye shughuli hiyo nyumbani kwao Oysterbay.

Posted in Africa, Bongo, Fashion, Fotografia, Kimataifa, Photography, Tanzania | Leave a Comment »

MPIGIE KURA IMAM

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

mpe-shavu-imam.jpg 

Sasa basi, kabla sijasahau, waandaaji wa shindano hili walitudokeza kwamba Watanzania tunaweza kupeleka washiriki wawili kule bondeni na mshiriki anayepewa nafasi kubwa ni Imam Abbas, mshindi wa pili kwa hapa nyumbani. Kumpeleka Imam kule bondeni bonyeza hapa na umpigie kura ili tuwe na wawakilishi wawili pale kusini na kujiwekea nafasi kubwa ya kushinda ile mizawadi. Ni hayo tu!

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 2 Comments »

FULL SHANGWE

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

mashabiki-wa-rage.jpg 

Mashabiki wa Rage wakimpa jamaa sapoti wakati wa mpambano

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | 1 Comment »

MAMBO YA KURA BWANA…

Posted by Bob Sankofa on January 13, 2008

mshindi-ni-rage.jpg 

Rage alipomaliza kura zikapigwa ili kumpata mshindi. Kura za mapilato wote watatu zikamwangukia Rage. Kwa mantiki hiyo Rage ndiye mwakilishi wetu kule “bondeni” katika shindano hili la SPRITE EMCEE AFRICA. Hongera sana Rage, tunategemea utarudi na ushindi huo mnono

Posted in Africa, Art, Bongo, Burudani, Fotografia, Music, Muziki, Photography, Sanaa, Tanzania, Ushairi | Leave a Comment »