MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

MRISHO NI WA KIMATAIFA SASA…

Posted by Bob Sankofa on February 3, 2008

tuku-012_mrisho-meza-moja.jpg

Akiwa ni mshairi wa siku nyingi, anayejituma bila kinyongo, hatimaye Mrisho Mpoto amefanya sanaa yake ya ushairi jukwaa moja na mfalme wa African Pop, Oliver Mutukuzi raia wa Zimbabwe. Ni heshima ya pekee kuona watu (watayarishaji wa sanaa za maonesho) wanaomtambua Mutukuzi wanatambua pia mchango na umaahiri wa kaka Mpoto hadi kufikia kumualika na kusimama jukwaa moja na kaka toka Zimbabwe. Mrisho na Mutukuzi watakutana tena kule Zanzibar katika tamasha la muziki la Sauti za Busara, http://www.mwenyemacho.com haitacheza mbali kukuletea kitakachojiri kule kuanzia tarehe 7 hadi 10 ya mwezi huu wa Februari.

tuku-016_mrisho-wapashe.jpg

Hapa Mrisho alikuwa akilicharanga lile shairi lake la “Nuru”. Nnachompendea Mrisho ni ile roho yake ya kujiamini. Cheki hapa palivyojaa wazungu lakini jamaa ananyuka shairi kwa Kiswahili, waelewe wasielewe watajiju! Cha kushangaza kwenye mikutano yetu mingi kukiwa na Waswahili 20 na mzungu mmoja tunajitahidi kutumia lugha ile ya yule mzungu mmoja, AIBU!

Advertisements

2 Responses to “MRISHO NI WA KIMATAIFA SASA…”

  1. luihamu said

    Mkuu Sankofa sahiri la NURU,JE KATI YA MIMI NA MIMI NANI ANAHITAJI NURU?

    RESPECT.

  2. kwa kweli ni aibu. Na mimi nakupongeza kwa kuchangia kwenye ‘ubloguni wa kiswahili’.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: