MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

MWENYEMACHO AONJA PASI

Posted by Bob Sankofa on December 1, 2007

gari.jpg

Huyu ni ‘punda’ wangu ninayemtegemea kwa kila kitu. Jana asubuhi ya saa kumi na mbili alikuwa akitumuvuzisha kuelekea Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kumwahisha ‘better half’ kukamata pipa ili kuelekea sehemu fulanifulani na ndipo zahma hili lilipomkuta ‘punda’ huyu. Gari kubwa ya kubeba mizigo, ambayo hadi sasa sijafahamu ilikuwa ikitokea wapi na kwenda wapi ilinichomekea kwa ghafla na katika harakati hizo jamaa akajikuta akininyuka pasi ya kutosha na kunibamiza kwenye ukingo wa barabara. Kama unavyoona, upande huu wa kushoto ndivyo hivyo ulivyo, ule upande wa kulia rim ya tairi imepinda na kutokana na kupinda kule nikashindwa hata kumtoa jamaa baruti maana hakusimama baada ya sekeseke lile.

Nashukuru Rabuka bado macho yangu na vidole vyangu vi hai na ninaweza kublogu bado na tayari punda yuko kwa ‘sangoma’.

PAMOJA!

Advertisements

6 Responses to “MWENYEMACHO AONJA PASI”

 1. Duh! Pole sana Mkuu.Mimi huwa najiuliza kama madereva wa Bongo wangekuja hapa basi ingekuwa mizinga kila dakika.Maana kwenye round about mwenye kuwahi kuingia ndio anapita na ni nadra sana kukuta watu wanapigana pasi namna hii

 2. Miriam said

  Poleni, tumshukuru aliye Juu kuwa ilikuwa ajali ndogo.

 3. Egidio na Miriam, nawashukuru sana. Namshukuru zaidi Mungu kwa kututoa salama salmini bila hata mkwaruzo.

 4. Gervas kasiga said

  pole sana kaka,twashukuru u mzima wa afya.

 5. irene sanga said

  pole sana kwa kipigo cha punda wako lakini mtima wako upo salama punda yuko kwa sangoma basi mungu azidi kukaa juu daima kama tunavyo amini kwani akikaa chini aya mkini asione mambo mengine yakitendeka kimakosa
  poa mtu wake
  irene

 6. Gervas na dada Irene, nawashukuru sana kwa kunijali. BAdo tuko pamoja na Inshalah tutaendelea kuwa pamoja. Asanteni.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: