MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

LUCKY DUBE AFARIKI DUNIA

Posted by Bob Sankofa on October 19, 2007

lucky-dube.jpg

Lucky Dube, mwanamuziki maarufu wa mtindo wa reggae, amefariki dunia Jo’berg, Afrika ya Kusini kwa kupigwa risasi siku ya Alhamisi ya tarehe 18 Oktoba, 2007. mauaji hayo yalitokea katika kitongoji cha Rosettenville ambako wauaji wake walitaka kumpora gari yake na hatimaye kuishia kumpiga risasi na kumuua, Polisi wa hapa wamesema.

Dube, alizaliwa  Johannesburg Agosti 3, 1964. Amefariki akiwa na umri wa miaka 43. Aliwahi kurekodi album karibu 20 hivi, zikiwemo Rastas Never Die, Think about the Children, Soul Taker na Trinity. Albamu yake mpya kabisa ni ile aliyoitoa 2006, ambayo aliita Respect. Dube alikuwa na mashabiki kibao nyumbani na duniani kote pia.

Watu wengi walipata taabu sana kumtambulisha Dube kama Rastafarian wa “kweli”, yeye mwenyewe alipokuwa akiulizwa alikuwa akisema, “Kama kuwa rasta maana yake ni kufuga nywele msokoto, kuvuta bangi na kuamini kwamba Haile Sellasie ni Mungu basi mimi si Rastafarian lakini iwapo Urastafari ni njia ya kujikomboa kisiasa, kijamii na kimawazo basi mimi ndiye.”

Inasemekana kuwa mtu aliyechangia sana kwa Dube kupiga muziki wa Reggae ni Peter Tosh, amabye naye aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 1989. Dube anasema mirindimo ya Tosh ndiyo hasa aliyojifunza kwayo lakini bado anakubali kuwa Bob Marley ndiye hasa mfalme wa miondoko ya Reggae duniani. Anasema, “Isingekuwa Bob labda tusingeifahamu reggae duniani kama tunavyoifahamu leo.”

Ni kitu cha kustaajabisha na kusikitisha kwa kuona ni kwa namna gani mwanadamu anazidi kuwa mnyama siku baada ya siku. Sote tutakufa siku moja lakini kifo cha Dube, ambaye alichangia kwa kiasi fulani kufanya watu wa rangi tofauti kuweza kuishi kwa kusikilizana pale Kusini, ni sawa na shukrani ya punda ambayo mara nyingi huwa ni mateke. Miziki yake siku zote ilisimamia heri, wamechukua roho yake kwa shari.

Jah amlaze mahala pema peponi Ras Luck Dube.

5 Responses to “LUCKY DUBE AFARIKI DUNIA”

  1. bella said

    PAIN, PAIN , PAIN wamechukua roho yake lakini mawazo yake yataishi milele kwa kupitia nyimbo zake. Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, AMINA.

  2. luihamu said

    Kwakweli mimi siamini kama huyu bwana ni rastafarian kwasababu ya mambo mengi.Naamini ukombozi wa mtu mweusi Afrika kusini ulianza zamani kipindi chakina Steve Biko na wengine,je kwanini Dube alisubiri mpaka baada ya uhuru wa Afrika kusini ndio akaanza kuimba Reggae?wengine wanasema Dube alikuwa anaimba zamani lakini sidhani.Pili miaka ya karibuni alipiga vibao vya mapenzi sana wakati sisi binadamu tunahitaji ujumbe wa kuponya sio wakuburudisha.Nakumbuka maneno ya Nabii Peter Tosh,LET THE DEAD BURY THEIR OWN DEATH.JAH LIVE.

  3. Aniceth Jonathan said

    Hey!!!
    I was speechless when i heard about the tragedy, it was real appalling sort of dealth, i felt like i’m dreaming when i got a call from my friend.

    After coming back to my senses, i felt disgusted and ashamed, a real son of Africa, who willingly and democratically tried his level best to speak for the voiceless through his songs,who informed the World about what was going-on especially on the dark side of normal human life, and look today is being paid by murdering him in front of his two kids…….that was so harsh, he didn’t deserve this.

    Now the World is changing, we are witnessing the increasing number of heartless people than ever b4, the World now is full of bad people and i’m afraid to say that because of their abundance, they are now representing normal and if you can join me and be one of those few rest to air and say more about them, still our voice need a boost up that we need to get so as to rise and be heard.

    It is real disgusting and brothers and sisters let us unite to expose those heartless people in our societies.

    May the almight God, who helped him from the real source of his name ‘Lucky’, to be World reknown figure, rest him in peace.
    AMEN

  4. Dan dan said

    Nataka kusema kitu tu kwa ndugu yangu Lihamu, apitie kwa kusoma au kusikiliza upya nyimbo za Lucky Dube, ataikanusha kauli yake kuwa Dube aliimba kuhusu mapenzi siku za karibuni. Nyimbo za Mapenzi unazozizungmzia bila shaka ni I have got u baby, I wanna know wahat love is, lovers in dangerous time na Baby dont cry, fuatilia utagundua kuwa ni wimbo mmoja tu alioimba mapenzi unayofikiria wewe nao ni I have got u baby, zingine alitumia fasihi kufikisha ujumbe kwa dunia. Fuatilia kwa makini

    Kuhusu kuimba baada ya uhuru, umepotosha historia, Dube kaanza kuimba kabla ya uhuru, pili dube kaanza kupigania uhuru kabla ya kuanza kuimba.

    Kwa maelezo zaidi niandikie ilovejesustz@yahoo.com au nipigie 0713 550 778

  5. Angela Kasamala said

    Lucky,

    This is to you….ever since i heard of your death, i play your songs in the office and in the car….i dont believe people can be so heartless….whether we do wrong or not, no man has the right over another man’s life (and even thier own life).

    I remember when i was young and i heard you were coming to Tanzania, i was so happy, i knew you would see me and marry me…yes, that’s how much i valued you and your music even since i was a kid.

    I pray for your family’s strength and yes, Lucky, there will be no one like you..love you…reggae for life…lucky dube for life…

Leave a comment