MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

NANI ALIKUWEPO KUMKUMBUKA MWALIMU?

Posted by Bob Sankofa on October 15, 2007

salim.JPG

Dakta Salim Ahmed Salimu, aliyewahi kuwa katibu mkuu wa OAU na sasa mwenyekiti (kama sijakosea) wa Taasis ya Mwalimu Nyerere alikwepo kumuenzi Mwalimu. Kumbuka Salim aliwahi kupewa kazi ya kuliwakilisha taifa kimataifa angali kijana mdogo kabisa wa miaka kumi na tisa tu. Pembeni ya Dakta Salim ni balozi wa Afrika ya Kusini, kumbuka pia kuwa Afrika Kusini ina deni kubwa sana la fadhila kwa Tanzania kutokana na msaada wa hali na mali Tanzania iliyoipatia Afrika ya Kusini kipindi kile cha vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, ndio maana balozi yuko hapa.

011.JPG

Alikuwepo pia mhadhiri wa siku nyingi hapa chuoni, Profesa Haroub Othman. Niliongea kidogo na Profesa na katika maongezi yetu akaniambia kuwa yeye ni mmoja wa Wajamaa wachache waliobakia katika jamii yetu leo, ambayo kwa kiasi kikubwa ni ya kibepari japo tuna katiba ya kijamaa.

027.JPG

Dakta Martha Qorro (mwenye batiki), mhadhiri pia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ni mkufunzi wa lugha ya Kiswahili huyu, kwa wale waliochukua taaluma ya lugha hiyo kama kina Ndesanjo Macha bila shaka mtakuwa mnamkumbuka mama huyu. Bado yupo na anazidi kuwa kijana. Dakta Qorro ni mmoja wa wahadhiri au wasomi wachache ambao ukiongea nae katu huwezi kumsikia akichanganya lugha mbili kwa wakati mmoja. Akiongea Kiswahili basi ni kiswahili moja kwa moja, akiongea Kikoloni basi ni Kikoloni moja kwa moja.

037.JPG

Maria Shaba, mwanaharakati na mwenyekiti wa TAMWA naye alikuwepo. Alitoa mada katika kumbukumbu hii ya nane ya kumuenzei Mwalimu. Aliitoa jioni sana na mimi nilikuwa nimeshawahi sehemu nyingine kwa hivyo kwa bahati mbaya sikufanikiwa kusikia alizungumzia nini hasa.

049.JPG

Joseph Butiku, huyu ni Katibu wa Taasis ya Mwalimu Nyerere pia ni ndugu wa damu wa Mwalimu. Naye alikuwepo kuwakilisha uwepo wa Taasis ya Mwalimu.

059.JPG

Kutoka katika Serikali ya “Ari, Nguvu, na Kasi Mpya” alikuwepo waziri wako wa Ardhi, Mh. John Pombe Magufuli. Mh. John huwa anakuja kwenye kila maadhimisho ya siku hii, kila mwaka huwa yuko hapa na ana mvuto mkubwa sana kwa wanajumuiya wa hapa chuoni. Huwa akifika wanamkaribisha kule kwenye meza kuu lakini sijui kwa nini huwa anakataa kabisa. Huwa anapenda kukaa safu ya viti vya nyuma nyuma hivi.

Picha na: Bob Sankofa

Mahali: UDSM

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: