MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

MRISHO MPOTO, MWANAMAPINDUZI!

Posted by Bob Sankofa on October 11, 2007

mpoto-2.JPG

Pengine Mrisho Mpoto ndiye mshairi pekee katika Tanzania nzima ambaye anaishi kwa kutegemea sanaa pekee. Mrisho ni msanii wa ushairi, anafanya ushairi wa Kiswahili. Mara yangu ya kwanza kabisa kuweza kuongea na Mrisho ana kwa ana nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2005, tulikutana pale kijiji cha Makumbusho. Sikumbuki sawasawa kulikuwa na shughuli gani pale ila nakumbuka kuwa siku ile ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana na Mrisho.

Nakumbuka katika mazungumzo yetu mafupi neno “Kaka” ndilo neno alilolitaja mara nyingi katika sentensi zake. Kabla hata ya kukutana na Mrisho macho kwa macho nilikwishazisikia sifa zake hapo awali na nilikwishawahi kumuona pia kwenye igizo la “Mfalme Juha” lililoandaliwa na kikundi chake cha Parapanda, pale Russian Cultural Hall, mwaka 2003. Mrisho alicheza kama Mfalme Juha siku ile na kwa mara ya kwanza niliiona hadithi ile ya bwana Farouk Toupan ikiishi.

Nakumbuka tulipokutana na kuzungumza pale Kijiji cha Makumbusho mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kumfuata Mrisho kwenda kumsabahi ila yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kuitamka salamu, “Habari ‘kaka’?”, huku akinipa mkono. Kwa umaarufu aliokuwa nao Mrisho kipindi kile, amabo anao hata sasa, sikutegemea kwamba angeanza yeye kunitamkia salamu. Kwa utamaduni wa kwetu sisi washabiki ndio inabidi tupambane kumsalimu “Superstar”, au nadanganya?

Basi baada ya salamu tukaongea mambo mengi. Kwa kweli nilikuwa nikimstaajabia sana Mrisho kwa kipaji alichonacho. Mrisho amewahi kukariri shairi la Mzee Shaaban Robert, “Titi la Mama”, ambalo lina beti hamsini. Shairi lile si pekee alilonalo kichwani, anayo mengi marefu ambayo washairi wengine huyakimbia kwa kuogopa kuchemsha kwenye steji wakati wa kupafomu. Liko moja linaitwa “Elimu” lilitungwa na mkurugenzi wa Parapanda, kaka Mgunga. Kwa sasa anatamba na “Salamu kwa Mjomba” lilotungwa na Irene Sanga.

Siku zile pale Makumbusho nikamuuliza Mrisho, “Vipi sanaa, inakulipa?”. Akanijibu huku anatabasamu, “Kaka, mimi elimu yangu ni ya shule ya msingi toka nitoke shuleni sikuwahi kufanya kazi nyingine zaidi ya kuigiza na kughani mashairi. Ushairi na sanaa ndio baba yangu na ndio mama yangu. Nina familia na hakuna anayenisaidia kuilea, zaidi ya mke wangu. Kwa hiyo sanaa inanilipa kaka”

mpoto.JPG

Mrisho akazidi kunishangaza, kwanza kwa uwezo wake wa kukariri mashairi marefu kupindukia, pili kwa falsafa kali zilizoko katika kazi zake na wakati huohuo anakwambia elimu yake ni ya msingi, na tatu kwa ‘kutojitambua’ kwake kwamba yeye ni mtu maarufu mno. Mrisho ananishangaza kila kukicha. Ila kuhusu elimu yake akaniambia, “Baada ya kutoka shule sikukoma kuendelea kujisomea, kwa mantiki hiyo vyeti vyangu ni vya ngazi hiyo lakini mtazamo wangu ni zaidi ya hapo”.

Hata hivyo Mrisho anazidi kunishangaza, kwani wakati watu wenye digirii lukuki wanaikimbia teknolojia, yeye anaikimbilia. Amefungua blogu, www.mrishompoto.blogspot.com, mtembelee umkaribishe tafadhali, pia uone kazi zake pia.

Mrisho nimekutana nae tena tarehe 29 ya mwezi uliopita kwenye tamasha la WAPI, pale British Council, ambako utamaduni huu unafanyika kila jumamosi ya mwisho ya mwezi. Kauli mbiu ya WAPI mwezi uliopita ilikuwa ni “Amani Tanzania, Laana au Baraka?”. Kwenye mkutano ule mgeni rasmi alikuwa ni Mpoto.

Hadi wakati mwingine,

Uhuru!

Picha na: Bob Sankofa

Mahali: British Council

Advertisements

3 Responses to “MRISHO MPOTO, MWANAMAPINDUZI!”

  1. Tunashukuru kaanzisha Blogu. Nimemsikia sana Huyu Msanii, lakini nilikuwa sijabahatika kuona shughuli zake.
    Asante kwakututonya Bob!

  2. Tuko pamoja kaka Kitururu.

  3. Nilipata bahati kuona na kusikia salamu toka Mjomba.Ebwana,lile shairi limetulia ile mbaya.Kwa kweli ni mmoja ya wasanii ninaowakubali kazi zake zinadumu mawazoni mwa watu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: