MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

HODI HODI LONDON, LEICESTER HADI COVENTRY

Posted by Bob Sankofa on September 27, 2007

zafaa_header.jpg

Ukiangalia ukurasa wa “Mimi ni Nani” hapa bloguni utaona kuwa kazi moja wapo ninayofanya ni kutengeneza filamu. Kwa maana nyingine mimi ni mtengeneza filamu. Mwaka jana nilipata bahati ya kutengeneza filamu fupi ya dakika kumi na tatu inayokwenda kwa jina la “Play Your Part” kwa ushirikiano wa shirika lisilo la kiserikali la White Ribbons Alliance Tanzania. Filamu ile inahusiana na swala zima la afya ya uzazi salama kwa mama na mtoto. Bofya hapa kusoma zaidi kuhusiana na filamu ile na pia unaweza kuitazama filamu hiyo kwenye ukurasa huohuo.

Filamu ya “Play Your Part” imechaguliwa kushindania tuzo za Annual African Film Academy Awards (ZAFAA, 2007), kama filamu fupi bora. Tamasha litafanyika pale London, UK kwa siku sita, yaani tangu tarehe 2 hadi saba. “Mwenye Macho” kama kawaida itakuwepo kuwakilisha, nadhani mambo ya mtandao hayatakuwa kama ilivyokuwa kwenye Digital Indaba pale Kusini. Nimealikwa kwenda kupokea zawadi ile kwa niaba ya timu nzima iliyoshiriki katika uandaaji wa filamu ile.

Napiga hodi kwa wenye jiji la London, kaka Freddy Macha lazima twende kikombe kupata kikombe cha kahawa ya Brazil.

Baada ya siku zile sita pale London nitaomba kuwatembelea wadau pale Leicester tupate mvinyo kidogo na kubadilishana mawazo. Sitakomea hapo, Rabia na Amulo, nakuja Coventry, nataka kukutana na wadau wangu hapo kwa masaa machache kabla ya kurejea tena Leicester tayari kwa kurudi kwa Jakaya tarehe 13/10.

Wadau wa miji mingine mtanisamehe, nimepewa likizo ya siku kumi na nne tu kibaruani kwangu, ila msikonde nina viza ya miezi sita na tayari kuna wadau wameshanialika kwenye sikukuu ya Noeli kwenda kuchezea barafu kwa hiyo tutaonana mwezi wa kumi na mbili.

Advertisements

3 Responses to “HODI HODI LONDON, LEICESTER HADI COVENTRY”

 1. mwafrika said

  FELICITATION!! kifaransa hicho ina maana karibu na CONGRATULATION!!

 2. […] on “WAPI” IMEWADIA TE…Egidio Ndabagoye on JUMUIYA YA WASHAIRI WA BONGO…mwafrika on HODI HODI LONDON, LEICESTER HA…Bob Sankofa on JUMUIYA YA WASHAIRI WA BONGO…Bob Sankofa on USHAIRI MURUA NA MVINYO MURUA… […]

 3. mwangaza said

  Bob!
  unafanya vitu si mchezo! nakupa hongera nyingi sana na nitaendelea kuipigia kura filamu yako!!
  bado kidogo utakuwa maarufu kama KaYUMBA

  BIG UP!
  mwangaza

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: