MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

WAPI – MAMA AFRIKA

Posted by Bob Sankofa on August 27, 2007

Kwa mara nyingine tena lile libenenge la utamaduni wa WAPI umetikisa tena jiji la Dar es Salaam. Kwa kifupi ni kuwa utamaduni wa WAPI ni utamaduni ambao umejikita katika kuhakikisha vijana wa Kitanzania, wenye vipaji mablimbali wanakutana mara moja kila mwezi na kuonyeshana uwezo. Wengi ya vijana hawa ni wale wanaoitwa “undergorunds”, wale ambao vyombo vikubwa vya habari havitaki kuwatangaza ipasavyo (kwa sababu hawana kashfa). Nitajitahidi kukuletea picha kadhaa ili na wewe ambaye hukuweza kuhudhuria mwezi huu upate kujionea haswa yaliyojiri. Fuatana nami katika mfululizo huu. 

hapa-ndipo-shughuli-za-wapi-hufanyika-kila-wikiendi-ya-mwisho-wa-mwezi.jpg

Hapa ndipo Shughuli za utamaduni wa WAPI hufanyika kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, British Council, Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwezi huu ilikuwa ni “Mama Afrika” na utamaduni ulichukua mkondo tarehe 25/8 kuanzia saa saba za mchana hadi kumi na mbili ya jioni.

zavara-rhymson-akishukuru-watu-kwa-kujitokoza-huyu-ndiye-mwanzilishi-wa-utamaduni-wa-wapi-tanzania-utamaduni-huu-upo-pia-nairobi-kenya-na-lagos-nigeria.jpg

Zavara (Rhymson) akishukuru watu kwa kujitokeza kuhudhuria WAPI. Huyu ndiye hasa mwanzilishi wa utamaduni wa WAPI hapa Tanzania. Utamaduni huu upo pia Nairobi, Kenya na Lagos, Nigeria. Kenya ndipo hasa utamaduni huu ulipoanzia, wao wameshafanya matamasha kumi na mbili. Hapa Tanzania WAPI – MAMA AFRIKA lilikuwa ni tamasha la tano.

mejah-mmoja-wa-waanzilishi-na-waratibu-wa-mradi-wa-wapi-akitoa-zawadi-ya-kitabu-kwa-mshindi-wa-uandishi-wa-insha-wa-mwezi-uliopita.jpg

Mejah, mmoja wa waanzilishi washiriki na mratibu wa mradi wa WAPI akitoa zawadi ya kitabu kwa mshindi wa uandishi wa insha wa mwezi uliopita, Kitabu kinaitwa Beast of No Nation kimeandikwa na Uzodinma Iweala, kijana wa Kinigeria mwenye umri wa miaka 24, hiki ni kitabu chake cha kwanza. Mejah ni mkufunzi wa sanaa ya grafiti na pia mhamasishaji mkubwa wa utamaduni wa kujisomea. Jamaa ana vitabu vingi kuliko maktaba ya shule yangu ya msingi, Muhimbili 🙂

dada-karola-kinasha-alikuwa-ndiye-msemaji-mkuu-kwa-mwezi-huu-katika-utamaduni-wa-wapi-kauli-mbiu-mwezi-huu-ilikuwa-ni-mama-afrika-karola-ni-mwanamuziki-wa-kujitegemea.jpg

Dada Karola Kinasha, alikuwa ndiye msemaji mkuu kwa mwezi huu katika utamaduni wa WAPI. Kama nilivyosema kauli mbiu mwezi huu ilikuwa ni Mama Afrika hivyo dada Karola, kama mama na msanii mkongwe, alikuwa ndiye msemaji mkuu katika makutano ya mwezi huu. Dada Karola ni mwanamuziki wa kujitegemea, kwa maana nyingine yeye ni mmoja wa wasanii wachache sana Tanzania ambao wanaishi kwa kutegemea fani ya muziki. Anawezaje? Labda tufanye nae mahojiano siku moja

img_1085.jpg

Utamaduni wa WAPI huhusisha vitu vingi sana lakini kuna kitu kimoja huunganisha vitu vyote hivyo, Muziki. Muziki huwaleta watu pamoja, hufanya watu wanaofanya sanaa mbalimbali kama ubunifu wa mavazi, ushairi, uigizaji, uchoraji na muziki kukaa na kuzungumza lugha moja.

Tafadhali endelea kufuatilia sehemu ya pili ya picha za WAPI – Mama Afrika.

UHURU!

Advertisements

3 Responses to “WAPI – MAMA AFRIKA”

  1. luihamu said

    Bob unajuwa kwanini naipenda sanaa,kwasababu sanaaa zote lazima utakuta rangi za ushindi,rangi zinazo tumika kuitambua Afrika.Bob umewaona manabii hao,sijui kwanini sikuudhuria.

  2. Itabidi uhudhurie mwezi ujao. Nafikiri pale ni mahali poa sana kwa wanablogu kukutana.

  3. Najaribu kuangalia mavazi ya Dada Karola Kinasha na hao wadada wa pembeni yake,Sipati jibu.Bado najiuliza

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: