MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

USHAWASIKIA MANYANI NANI BAND?

Posted by Bob Sankofa on August 11, 2007

Kuna bendi fulani hapa nyumbani inaitwa “Manyani Nani?”. Bendi hii ni kiboko sana kuanzia kwenye upigaji hadi utunzi wa mashairi. Kuna wakati fulani waliwahi kutoa wimbo wao mmoja unaitwa “Ali Baba”. Muulize Ndesanjo wa www.jikomboe.com, atakupa kisa kizima kuhusu wimbo ule. Nakumbuka Ndesanjo aliwahi kuwa na mazungumzo na Paul Ndunguru ili aurushe ule wimbo kwenye blogu sijui aliishia wapi, eti Ndesanjo. Ukisikiliza ule wimbo unaweza usipige kura Mwaka 2010.

Sasa jana jioni Manyani Nani? Band Walinialika kule katika studio za MFDI, Msasani Peninsular. Wako pale wanarekodi nyimbo zao mbili. Nikaruhusiwa kupata picha kadhaa na nikaona si haba nikishirikiana nanyi ndugu zangu.

paul-ndunguru.jpg

Huyu ni Paul Ndunguru, yeye ndiye Mwimbaji kiongozi na pia mtunzi wa Mashairi ya Manyani Nani? Band. Anapiga gitaa kavu pia. Bonyeza hapa umuulize Tungaraza wa kuhusu vipaji vingine alivyonavyo huyu bwana

fujo.jpg

Huyu anaitwa Fujo, yeye ni “Percussionist”, yani mambo yote ya mtonya wa kimakonde, Jembe, ngoma zote za marehemu mzee Nyunyusa, manyanga, madufu, na mazagazaga mengineyo ndio eneo la huyu bwana.

freddy.jpg

Freddy Saganda, anapiga gitaa kiongozi na pia ni mwimbaji mwitikiaji. Katika wimbo mmoja wapo wanaotengeneza sasa, unaitwa “Afrika”, jamaa analivurumisha gita kiasi kwamba kama uko mbali unaweza ukafikiri kuna kora linapigwa.

hussein.jpg

Hussein Masimbi, kwa wale waliopita Chuo cha Sanaa Bagamoyo watakuwa wanamfahamu sana huyu bwana. Baba yake alikuwa ni mkuu wa chuo kile, na huyu bwana alizaliwa na kukulia pale na hatimaye na yeye alisoma katika chuo kile. Unajua ni pale katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo ndipo bendi hii ilipoundwa, wanabendi hii wote wamepita pale. Inasemekana Hussein alianza kupiga ngoma akiwa na umri wa miaka mitano.

yusufu.jpg

Yusuph, jamaa anaungurumisha lile gita zito. Yusuph mbali na kupiga gita zito pia ni fundi wa kupangilia sauti za vyombo vya muziki. Amefanya kazi sana pale studio za Marimba. Jamaa yuko katika mchakato wa kufungua studio pia. Amewahi kupiga na Wananjenje pale Njenje plaza, Njenje Plaza sasa imebaki historia, msome Mjengwa na Michuzi wanazo habari zake.

hermis-na-rick.jpg

Hawa ni mafundi mitambo katika studio za MFDI kule Msasani. Huyo mzungu anaitwa Rick yeye ni Mzimbabwe lakini anakaa Marekani kwa sasa baada ya mambo kuwa HOT kule kwa mzee Bob. Huyo bwana mwingine yeye ni wa kunyumba, anaitwa Hermis, aliwahi kufanya kazi Magic FM. Rick ni mkali wa program ya muziki inayoitwa Pro Tools wakati Hermis yeye ni mkali wa Logic na Fruitloops, patamu hapo.

Nnachoweza sema ni kwamba hii bendi ni babkubwa na inahitaji airtime tu iweze kuanza kukimbizana na watu kama kina Ismael Lo, Yossou Ndou na Hadja Nin. Kaa mkao wa kula jamaa wataanza kugalagaza muda si mrefu.

Hadi wakati mwingine

UHURU!

Picha na: Bob Sankofa

Mahali: Studio za MFDI-TZ

Advertisements

2 Responses to “USHAWASIKIA MANYANI NANI BAND?”

  1. mwandani said

    Namuona Paul pale juu. Picha ziko safi sana – clear – contrast na vivuli vya black and white vina ladha nyingine

  2. Tungaraza kuna furaha fulani huwa Paul anaipata kila anapoona picha zako katika blogu, huwa anaishia tu kwa kusema, “Dah! kweli wakati umeenda”. Paul ameoa siku hizi na ana watoto wawili wa kiume, 🙂

    Asante kwa kutembelea humu na kuona yanayojiri nilipo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: