MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

KAZI NA DAWA

Posted by Bob Sankofa on June 15, 2007

Hivi niliwahi kukuambia kuwa ninafanya kibarua na jamaa fulani wanajiita MEDIA FOR DEVELOPMENT INTERNATIONAL? Kama hapana basi hapo ndipo nilipo, na picha hii nimeipiga majira ya saa kumi kasorobo jioni ya leo. Nilivutiwa na jua lilikuwa linagonga hapo kwenye meza

Huyu aliyemo katika picha hii ni rafiki yangu anaitwa Paul Ndunguru au Baba Paka (Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu hilo jina la pili muulize Ndesanjo Macha wa http://www.jikomboe.com/. Jamaa ni mchoraji wa katuni na mazagazaga mengine. Atakuwa na blogu hivi karibuni, umtembelee tafadhali. Hapa jamaa anapiga kazi huku anapata kababu na machicha ya nazi. Kazi na dawa bwana.

Picha hii pia niemiweka kwenye mtandao wa http://www.flickr.com/, tafadhali tembelea mtandao huu uone kazi za wapiga picha wengine. Huwa napata ideas nyingi sana humu.

Kuna kitu nimegundua baada ya kupiga picha hii, nadhani picha za Black and White bomba sana. Unaonaje nikiendelea kukuletea picha za mtindo huu hapa bloguni? Pale inapobidi tulete za rangi tutafanya hivyo. Naomba maoni

Advertisements

8 Responses to “KAZI NA DAWA”

 1. kifimbocheza said

  ndugu Mwenye Macho, mimi napenda sana black and white. Inaonyesha wazi umuhimu ya giza na ya mwanga pia.

  Asante kwa taarifa zako kutoka kwa TED.

 2. luihamu said

  Kaka badilisha TEMPLATE yako kisha weka picha za black and white la sivyo wengine hatuoni kabisa kama hii picha naona mwanga tu.

  Nuff Nuff Respect.

 3. mwandani said

  Naomba kufikisha salamu kwa Paul… mara ya mwisho New Delhi miaka ileee… sitasahau vichupa vya rangi ulivyoninunulia…sanaa idumu. Joe

 4. Bob Sankofa said

  Kaka Kifimbocheza wewe pia unapiga Picha? Tafadhali tuzidi kushirikiana maujuzi.

  Kaka Luihamu nafikiri inawezekana kuwa tarakilishi yako haikuwa na mwanga. Jaribu kuongeza brightness halafu punguza kidogo contrast.

  Kaka Mwandani, kaka Paul amepokea salamu. Anasema hiyo siku mlikutana Delhi kuna jambo hukutaka kabisa kumuamini japo alikuapia kabisa. Sijui ilikuwa nini ila amefurahi sana pata salamu toka kwako.

 5. kifimbocheza said

  Sankofa, mie siyo bwana picha! Takriban miaka 16 iloyopita, ilikuwa hobby yangu, lakini siku hizi sina hamu sana.

  Nilipenda picha yako. Ulivutiwa na mwanga mezani. Na sisi tulivutiwa na picha.

  Napendekeza picha zako ziwe kubwa zaidi kwenye blogu.

  Pia, niliweka blog yako kwa ‘blogroll’ yangu. Kwa sababu sisi wawili tulianza hivi karibuni, pia nilipenda taarifa zako za TED.

 6. Bob Sankofa said

  Nashukuru kwa kuweka kiunganishi cha blogu hii kwenye blogu yako, nami nitarejesha fadhila muda si mfupi.

  Nashukuru pia kwa wazo la kukuza picha. Ila ukibofya hapo kwenye picha itakupeleka kwenye ukurasa amabo unakuapa ukubwa wa picha halishi.

  Nina mpango wa kuanza kupandisha na video pia muda si mfupi.

 7. Bob Sankofa!!!!? Naamini wewe ni mchapakazi mahiri.Mchagu wangu kwako ni kuleta midahalo inayojenga na kuendeleza creative works…Mh Inglish!! Yaani nikimanisha kutoa michango katika hii timu ya wataalamu wabunifu. Nafikiri itawasaidia wengi ambao watajumuika nasi..

 8. Ni kweli kabisa Dede.

  Nashukuru sana kwa kutembelea blogu hii. Nafikiri mchango wako ni kitu kizuri sana na kikubwa kwa kweli.

  Anzisha mapambano baba, mbele kwa mbele.

  UHURU

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: