MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

HAPA NI DOZI JUU YA DOZI

Posted by Bob Sankofa on June 6, 2007

Rokia amemaliza kutukaribisha, ameimba kwa lugha moja wapo ya kule kwao Mali. Wengi hatujaelewa neno kwa neno kwa kile alichoimba lakini kwa uelewa wa jumla amtukaribisha Afrika.

Inapita kama dakika moja na nusu halafu kwenye jukwaa anakaribishwa mwongozaji wa sinema na mpiga picha wa siku nyingi, bwana Andrew Dosunmu, yeye anatoka Nigeria.

Ameshaongoza ” filamu ya “Hot Irons” (1999), ameongoza pia mchezo wa luninga huko Afrika ya Kusini uitwao “Yizo-Yizo”. Ila katika kazi zote za huyu jamaa iko moja amabyo imenimaliza kabisa, yeye ndiye aliyetengeneza video ya muziki wa “Birima” wa Yossou N’dour. N’dour naye ilikuwa awepo hapa leo lakini ana shughuli za kibinafsi.

Dosunmu anasema wapiga picha na watengeneza filamu wa kiafrika tunawajibika kuonyesha upande wa pili wa maisha ya mwafrika kwa mtazamo wetu wenyewe, CNN na BBC na FOX TV hawalazimiki kufanya hivyo kwani kwao habari mbaya kuhusu Afrika ndiyo inayouza. Duh! Jamaa anaongea ile pidgin ya Kinigeria, simpati kila neno.

Nashindwa kujizuia, namsaka Dosunmu na kupiga naye picha. Tafadhali tembelea tovuti yake ya www.andrewdosunmu.com ujionee kazi zake.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: