Mimi ni Nani?
Bob Sankofa (a.k.a. Philemon Msangi). Hilo ndio jina langu haswa.
Mtanzania. Huo ndio utaifa wangu. Na ninaishi hapahapa Tanzania.
Tarehe ya Kuzaliwa: 29/04/1980, huwa sisherehekei kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa. Huwa nafanya kazi zaidi kwani najua muda wa kuishi umezidi kupungua.
Mahusiano: Sijaoa ila nimeshachukuliwa
Mwanafotografia, mtengeneza filamu, mwanablogu, mjasiriamali, mfasiri na mwanablogu. Hizo ndizo kazi zinazoniweka hapa duniani.
+255 713 223 345 au +255 763 809 377. Sijawahi kuzizima tangu nilipozinunua.
Barua pepe: babukadja@hotmail.com. Nakaa tarakilishini si chini ya msaa matano kila siku. Ukiandika, nitasoma, nitakujibu pia.
Jina la kwenye Skype: babukadja. Naipenda kwa sababu ni ya bure
Jina la kwenye MSN: babukadja@hotmail.com
Jina la kwenye Yahoo Messenger: babukadja@yahoo.com
Sanduku la Posta. Usijisumbue, sijaenda posta mwaka wa pili sasa.





msangimdogo said
Singe & Human!! hapo tu ndipo nilipopapenda.
Nimefurahi kutembelea hapa.