NYONGEZA YA MAONESHO
Posted by Bob Sankofa on March 7, 2008

Kama huna uwezo wa kununua sanaa (Vinyago) kubwa-kubwa za kina dada hawa basi unaweza ukanunua poster za moanesho haya kwa shilingi elfu tano au kwa kina mama unaweza kununua vifaa vya urembo vinavyotokana na miti kama bangili, hereni na mikufu. Ni namna fulani ya kujiwekea kumbukumbu kuwa ulihudhuria maonesho haya. Pili ndio alikuwa mezani jana.





simbadeo said
Bob, posts nzuri sana hizi, hasa kuhusu akina dada hawa jasiri. Asante kwa habari juu ya maonyesho hayo. Hakika ntapata walau wasaa mfupi kufika ndani ya siku hizi 21. Sanaa, kisima cha fikra, sanaa chemchem ya mageuzi/mapinduzi. Tuidumishe sanaa.