MWENYEMACHO DOT COM

Yanapojiri Nilipo na Wewe Upo

MWENYE MACHO AUZA PICHA YA KWANZA

Posted by Bob Sankofa on July 3, 2007

Hatimaye Mwenye Macho ameuza picha yake ya kwanza katika maisha yake ya upigaji picha kwenye jarida moja huko Ufaransa kupitia wakala wa picha aitwaye Cedric Galbe. Cedric Galbe ni mpiga picha wa Kifaransa ambaye ameanzisha tovuti iitwayo www.Galbe.com. Tovuti hii ni wakala wa wapiga picha toka Africa, Scandinavia, Mashariki ya Kati, na Marekani ya Kusini.

Picha aliyouza ni hiyo hapo juu ya mtaalamu wa hesabu aitwaye Ron. Ron alitoa mada kwenye mkutano wa TED uliofanyika Arusha mwezi uliopita. Mada yake ilikuwa inaonyesha ni kwa jinsi gani hesabu zinavyothibitisha kuwa maisha yalianzia Afrika. Kwa habari zake zaidi tembelea www.jikomboe.com, Ndesanjo alimwandika vizuri zaidi. Mimi sikumwelewa sawasawa kwani mimi na hesabu hatukuwahi kuwa marafiki hata kidogo.

Mpaka wakati mwingine, naelekea benki mara moja kuona kama dola zangu zimeingia.

8 Responses to “MWENYE MACHO AUZA PICHA YA KWANZA”

  1. mwandani said

    babu kubwa. endeleza mapambano.

  2. Hongera sana Sankofa,
    Huu ni mfano mzuri na ushuhuda kwamba blogs sio tu chanzo cha habari bali pia utajiri.Endelea na mwendo huo huo.

  3. Serina said

    hongera.

  4. ndesanjo said

    hongera sana Sankofa

  5. ndesanjo said

    hongera sana Sankofa

  6. Kaka imetulia sana hii.Endeleza mapambano.

  7. Nawashukuruni nyote, asanteni sana

  8. [...] Tanzanian blogger, Sankofa, has sold a photo he posted on his blog from TEDGlobal 2007. Share [...]

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Connecting to %s

 
Follow

Get every new post delivered to your Inbox.